Ticker

6/recent/ticker-posts

Madhara ya kuongeza matiti,apata madhara baada ya Upasuaji wa kuinua Matiti



Madhara ya kuongeza matiti,apata madhara baada ya Upasuaji wa kuinua Matiti

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 22 aliondoka na kwenda hadi Uturuki kwa ajili ya kufanya upasuaji wa kuinua matiti ambao ‘ulikwenda vibaya’ (Picha).

Mwanamke huyo raia wa Uingereza ameachwa katika uchungu mkubwa na chuchu kuharibika kabsa kutokana na kufanyiwa upasuaji wa kuinua matiti ambao ‘ulikwenda vibaya’

Chloe Rose, mwenye umri wa miaka 22, ambaye anaishi Halifax, West Yorkshire, alifanya upasuaji huo nchini Uturuki baada ya kulipa £2,800 kwa ajili ya kuinua matiti.

Mama huyo wa mtoto mmoja alizinduka kutoka kwenye upasuaji wa saa nne na kupata shida baada ya upasuaji kwenda ‘Vibaya sana’.

Kulingana na Mail Online, marafiki na Chloe huko Istanbul wanadai madaktari wa upasuaji walichukua ngozi nyingi kutoka kwa matiti yake na kusababisha kupoteza mzunguko wa damu kwenye chuchu zake, na kusababisha necrosis, tatizo la kufa kwa tishu za mwili.

Familia na marafiki zake wameanzisha rufaa ya GoFundMe kwa ajili ya kumsafirisha Chloe kwa ndege kurejea Uingereza kwa matibabu baada ya kudaiwa na kuambiwa alipe pesa za kukaa katika hospitali ya Uturuki, ambapo madaktari wamesema kuwa walikana uzembe huo.

Rafiki Rachel Mucha, mwenye umri wa miaka 22, ambaye yuko Istanbul na Chloe, aliiambia MailOnline:

‘Chloe alitaka kuwa na muonekano bora kuhusu yeye mwenyewe. Alichukia jinsi matiti yake yalivyoonekana hivyo akaamua kufanyiwa upasuaji Uturuki, ambako ni nafuu zaidi kuliko Uingereza.

‘Tuliondoka Jumatatu na alifanyiwa upasuaji Jumanne.

‘Madaktari walisema upasuaji ulikwenda sawa lakini Chloe alipokuja alikuwa akipiga kelele kwa uchungu – alijua mwili wake haujisikii sawa.

‘Ameachwa na necrosis ya chuchu ambapo chuchu zake zinakufa. Sasa, tumekwama katika nchi ya kigeni hatujui la kufanya.

‘Daktari aliendelea kutuambia ‘ni sawa’ lakini si sawa. Chloe yuko katika uchungu – anahisi kama atakufa.

‘Tuliondoka hospitalini kwa sababu hatukuweza kumudu kukaa.

Tunataka kuruka nyumbani lakini hatujui kama ataruhusiwa.’

Marafiki wa Chloe waliweka picha kwenye mitandao ya kijamii za matiti yake baada ya upasuaji wake. Zinaonyesha tishu zake za chuchu zikiwa nyeusi kutokana na ukosefu wa mtiririko wa damu.

Dada Collette Pickering alisema operesheni hiyo ‘ilikwenda vibaya sana’.

Aliandika hivi: ‘Je, kuna mtu yeyote anaweza kutupa ushauri au kutafuta msaada?

‘Tuko Uturuki na Chloe aliinuliwa matiti – tangu kufanyiwa upasuaji chuchu zake zimepoteza mzunguko wa damu na kufa.

‘Madaktari hawajawahi kukiri kuwa na tatizo kwa muda wote wamesema kila kitu ni kawaida.

“Wamefungua mshono wake kwa blade,bila kutuliza maumivu nilipomtazama na kumwacha akiwa na majeraha kwa saa 48.”

Collette alisema matabibu ‘walizirejesha kwa kiasi’ chuchu za Chloe lakini akaongeza: ‘Zinakufa zaidi kadri saa zinavyosonga.

“Wana jukumu la kuwatunza, alilipa pesa zote hizo kwa ajili ya operesheni salama na ameachwa afe.”

Aliongeza: ‘Kila kitu ni cha kawaida kulingana na wao.

‘Sijawahi kuona mtu yeyote mwenye umri mdogo hivi akionekana kutokuwa sawa katika maisha yangu.

‘Upasuaji ulipaswa kuchukua dakika 45, ilichukua saa tano. Ilipaswa kuwa rahisi sana.

‘Dada yangu alitoka nje kwa mshtuko ambapo alikuwa akitetemeka kitandani. Tangu wakati huo na kuendelea Matiti yote yalikuwa yakiteremka.’

Familia ya Chloe ilisema operesheni hiyo iliwekwa kwenye mtandao wa Instagram na kampuni yenye ‘five star reviews’.



Post a Comment

0 Comments