Ticker

6/recent/ticker-posts

Madhara ya kuongeza matiti,Hizi ndyo athari za kuongeza Matiti



Madhara ya kuongeza matiti,Hizi ndyo athari za kuongeza Matiti

Kuongezeka kwa matiti ni mchakato unaoanzia kipindi cha Ukuaji au balehe(puberty),

Kiwango na ukubwa wa matiti hutegemea na Sababu za ndani kwa mhusika, ikiwemo;

  • Vichocheo(hormnes)
  • Uzito
  • Umri n.k

Vichocheo(Hormones): hormones za kike kama vile estrogen huhamasisha ukuaji wa matiti katika kipindi chote cha Maisha,

Hivo basi, kitu chochote kinachoathiri(fluctuations) kiwango cha hormones za estrogen na progesterone kinaweza kubadilisha umbo au shape na Ukubwa wa matiti,

mfano; Hedhi(menstruation), Ujauzito, au Mwanamke kufikia ukomo wa hedhi(menopause), vyote hivi vinaweza kubadilisha umbo na ukubwa wa matiti.

Uzito wa Mwili(Body weight): Watu wengi hawafahamu;  Uzito unaweza kuongezeka(overweight) au kushuka(underweight) kiasi kwamba huweza kubadilisha umbo pamoja na Ukubwa wa matiti yako.

Umri(Kuzeeka): Kadri Umri unavyokuwa mkubwa Zaidi ngozi hubadilika na kupungua uwezo wake wa asili wa kuvutika na kuwa Imara( elastic and firm),

Hali hii huweza kusababisha kubadilika kwa umbo na Ukubwa wa Matiti yako.

Madhara ya kuongeza matiti

Urembo unazidi kuwa ghali mno huku kila mwanadada akifanya lolote kupendeza, walio na matiti madogo huyanenepesha kwa wale wenye makubwa pia huyapunguza na kuwa saizi wanayotaka.

Wanadada wengi wamepoteza maisha kwa kutumia baadhi ya vipodozi katika kujirembesha.

Upasuaji salama wa matiti hugharimu mamilioni ya fedha ambayo wengi wa wanadada hawawezi kugharamu hivyo hulazimika kutumia mbinu zenye bei chee ikiwemo upasuaji ambao hatima yake huwa na athari kubwa maishani mwao.

Jarida la TUKO.co. ke limefanya utafiti na kugundua madhara yanayotokana na upasuaji wa matiti,

Na haya hapa ni baadhi ya Madhara yaliyoorodheshwa;

1. Matititi huishia kuwa kombo kwa kukosa umbo mzuri.

2. Ngozi huathirika kwa kujikunjakunja.

3. Kovu kuchukua muda mrefu kabla kupona kabisa na kukupa maumivu si haba.

4. Mwili kupasuka na kifaa cha kunenepesha matiti kuonekana nje ya mwili.

5. Kuambukizwa magonjwa mengine ikiwemo kupooza

6. Upasuaji huweza kusababisha kufura kwa ncha ya matiti

7. Huweza kuathiri kwa kupunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa

8. Matiti kuanguka – Kwa wengine, badala ya matiti yao kuwa tisti baada ya upasuaji, yanaregarega kama ya ajuza.

9. Rangi ya matiti huweza kubadilika kutokana na kufuja kwa damu wakati wa upasuaji

10. Wengine huathirika kwa kushikwa na upele matitini

11. Matiti huweza kufura na kuwa makubwa kupita kiasi.

Kumbuka: Usifanye vitu hivi kwa Ushawishi wa watu wengine pasipo kupata maelekezo ya kina kutoka kwa Wataalam wa Afya.



Post a Comment

0 Comments