Ticker

6/recent/ticker-posts

Madhara ya Vidonge vya Uzazi wa Mpango kwa Mjamzito: Je, Ni Kiasi Gani cha Hatari?



Madhara ya Vidonge vya Uzazi wa Mpango kwa Mjamzito: Je, Ni Kiasi Gani cha Hatari?

Baadhi ya Wanawake hawajui kwamba ni wajawazito,hivo wanaendelea kutumia vidonge vya kuzuia mimba kumbe tayari wanayo,

kwa Wanawake ambao wapo kwenye hali hii, Walitumia vidonge vya kuzuia mimba huku tayari wana mimba, Je, Wanaweza kupata madhara yoyote?

Zipo tafiti mbali mbali kuhusu matumizi ya vidonge vya Uzazi wa mpango na madhara kwa Ujauzito, na katika tafiti hizo baadhi zimeonyesha hakuna madhara yoyote na zingine zimeonyesha kuna madhara.

Mfano: Utafiti wa mwaka 2016 kuhusu matumizi ya Vidonge vya Uzazi na madhara kwenye Ujauzito ulionyesha;

Watoto ambao huzaliwa na wakina mama ambao wanatumia vidonge vya uzazi huwa kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo kwenye mfumo wa upumuaji au matatizo kama vile wheezing and rhinitis (a stuffy and runny nose).

A 2016 studyTrusted Source suggests that babies born to mothers using the pill have an increased risk of wheezing and rhinitis (a stuffy and runny nose).

Vidonge vya uzazi wa mpango ni njia maarufu ya kuzuia mimba, lakini mara nyingine wanawake huendelea kuchukua vidonge hivi bila kujua madhara yanayoweza kutokea wanapokuwa wajawazito.

Inawezekana kabisa kwa mwanamke kuwa na mimba ingawa anatumia vidonge hivi, na hali hii inaweza kuathiri afya ya mtoto na mama.

Madhara ya Vidonge vya Uzazi wa Mpango kwa Mjamzito:

Hapa tunachunguza madhara ya vidonge vya uzazi wa mpango kwa mjamzito, Na Madhara hayo ni kama ifuatavyo;

1. Hatari ya Kutopata Mimba Kwa Wakati:

Matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango wakati wa mimba yanaweza kuongeza hatari ya kuchelewa kugundua ujauzito.

Hii ni kwa sababu vidonge hivyo vinaweza kuficha dalili za ujauzito kama kutotulia kwa hedhi n.k.

2. Ongezeko la Hatari ya Mimba Iliyoharibika:

Kuna ushahidi unaonyesha kuwa wanawake wanaochukua vidonge vya uzazi wa mpango wanapokuwa wajawazito wanaweza kuwa na hatari kubwa ya kupata mimba iliyoharibika au mimba kutotungwa vizuri kwenye eneo husika.

3. Mabadiliko ya Hormoni:

Vidonge vya uzazi wa mpango vina vichocheo au homoni zinazoweza kubadilisha mfumo wa homoni mwilini. Hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanamke na kusababisha matatizo wakati wa mimba.

4. Upungufu wa Madini ya Folate:

Vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza kusababisha upungufu wa madini ya folate mwilini.

Hii ni hatari kwa ukuaji wa afya kwa mtoto na inaweza kuchangia matatizo ya kuzaliwa kwa watoto.

5. Kuongezeka kwa Hatari ya Blood Clots:

Baadhi ya vidonge vya uzazi wa mpango vyenye homoni vinaweza kuongeza hatari ya blood clots. Hii inaweza kuwa hatari zaidi wakati wa ujauzito.

6.Mambo Mengine ya Kuzingatia:

Vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza pia kuathiri virutubisho mwilini kama vile vitamini na madini mengine muhimu kwa ukuaji wa mtoto.

Ni muhimu kuzingatia kuwa madhara haya hayatokei kwa kila mwanamke, na kila mwili unaweza kupata hali tofauti kwa vidonge vya uzazi wa mpango.

Kabla ya kuanza au kuacha matumizi ya vidonge hivi wakati wa ujauzito, ni vyema kushauriana na daktari ili kupata ushauri sahihi na kuelewa athari zinazoweza kutokea kwa hali yako maalum. Kumbuka, afya ya mama na mtoto ni kipaumbele cha juu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584. karibu….!!!!!



Post a Comment

0 Comments