Ticker

6/recent/ticker-posts

Sherehe:bibi harusi wa Gambia afaulu mtihani wake wa kupimwa ubikira, na kupokea zawadi ya pesa taslimu kutoka kwa mumewe



Sherehe:bibi harusi wa Gambia afaulu mtihani wake wa kupimwa ubikira, na kupokea zawadi ya pesa taslimu kutoka kwa mumewe.

Mwanamke wa Gambia, Meta Mbye, amepokea zawadi ya pesa taslimu D28,000 kutoka kwa mumewe baada ya kufaulu mtihani wake wa kupimwa ubikira,

Sherehe baada ya Mwanamke huyo kupimwa na kukutwa bado ni bikra.

Video iliyosambaa kwenye mtandao wa TikTok inaonyesha wanafamilia wakisherehekea baada ya jaribio hilo.

Mmoja wa jamaa, ambaye alikaa nje akisubiri Meta alipokuwa akipimwa ubikira, alithibitisha kuwa mume wa Meta alimpa zaidi ya D28,000.

“Mume alifurahi sana ndiyo maana alimpa D28,000, ambayo iliwekwa chini ya mto wake,” alisema.

Baadhi ya wazee waliokuwepo baada ya mtihani huo walimpongeza mama Meta kwa kumlea mwanamke safi.

Video hiyo imezua hisia tofauti huku wengi wakimpongeza Meta kwa kubaki bikira hadi siku ya harusi yake huku wengine wakitetea kuwa mtihani wa ubikira unapaswa kupigwa marufuku kwa sababu unafedhehesha.



Post a Comment

0 Comments