Tatizo la Uzito kuongezeka kipindi cha Likizo au mapumziko na madhara yake
Tatizo la Uzito kuongezeka kipindi cha Likizo au mapumziko na madhara yake
Uzito mkubwa ni tatizo linalozidi kuenea na kuwa sugu, kwa sasa ni sababu ya tano ya vifo ulimwenguni kote,
Inahusishwa sana na kisukari cha aina ya 2(type2 diabetes), ugonjwa wa moyo, na aina fulani za saratani.
Utafiti wa mwaka 2000 ulionyesha kuwa msimu wa likizo ya majira ya baridi kali au kuanzia wiki ya mwisho ya Novemba hadi wiki ya kwanza au ya pili ya Januari, unaweza kuwa wakati wa ongezeko kubwa la uzito kwa Watu,
Wataalamu wa matibabu katika Chuo Kikuu cha Tiba na Famasia Grigore T. Popa huko Iasi, Romania walichunguza mifumo ya lishe kwenye sikukuu za majira ya baridi,
Msimu huu wa kitamaduni unajulikana kwa matumizi kupita kiasi, kalori nyingi, vyakula vyenye sukari nyingi, vinywaji na pombe, pamoja na kupungua kwa shughuli za kimwili.
Wataalam hao walizingatia mambo ya kisaikolojia yanayoathiri ongezeko la uzito wakati wa likizo za majira ya baridi na uundaji wa lishe za vyakula maarufu vya sherehe.
Waligundua kuwa watu wengi katika tafiti walizochanganua waliongezeka uzito zaidi hali waliopata wakati wa likizo, haswa wale walio na unene uliopitiliza.
Watafiti wanaamini kuwa ukaguzi huu wa kimfumo ulikuwa wa kwanza kuchunguza umuhimu wa mifumo ya lishe wakati wa likizo za majira ya baridi.
Wanatumai kuwa matokeo yao, yaliyochapishwa katika jarida la Nutrients, yanaweza kusaidia kuhimiza mienendo inayohusishwa na mafanikio ya muda mrefu katika kudhibiti uzito.
Soma Madhara ya Uzito Mkubwa hapa;
Pata ebook ya kukusaidia Kupunguza Uzito kwa haraka Zaidi;
https://afyaclass.com/2022/06/jinsi-ya-kupunguza-uzito-ndani-ya-wiki-moja.html
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!