Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa UTI ni nini? na Dalili zake ni Zipi? Na je nani yupo kwenye hatari Zaidi kupata?



Ugonjwa wa UTI ni nini? na Dalili zake ni Zipi? Na je nani yupo kwenye hatari Zaidi kupata?

Ni kweli kwamba kuna Makala Nyingi sana Mtandaoni kuhusu Ugonjwa wa UTI, Lakini leo kupitia makala hii tutagusa vitu ambavyo pengine hujawahi kuvisikia popote.

Ugonjwa wa UTI

Ugonjwa wa UTI huhisisha maambukizi kwenye njia na mfumo mzima wa mkojo na kwa kitaalam hujulikana kama Urinary tract infections (UTIs),

Maambukizi haya hutokea pale ambapo viini vya magonjwa kama vile bacteria vinaposhambulia kwenye mfumo wa Mkojo.

Ugonjwa wa UTI ni ugonjwa sumbufu kwa watu wengi duniani sio Tanzania pekee, Mfano; kwa nchi ya Marekani pekee, Zaidi ya watu million 8.1 humuona daktari kila Mwaka kwa Sababu ya tatizo hili.

Ugonjwa huu huathiri maeneo mbali mbali kwenye mfumo wa Mkojo ikiwemo;

  • Figo
  • Njia ya mkojo,ureters,Urethra
  • Kibofu cha Mkojo n.k

Watu ambao wapo kwenye hatari ya Kupata UTI

Kutokana na utafiti wa Mwaka 2022 ulionyesha kwamba; Kundi hili la watu lipo kwenye hatari zaidi ya kupata Ugonjwa huu wa UTI;

  • Wanawake
  • Wajawazito
  • Wenye matatizo yanayosababisha upungufu wa kinga mwilini
  • Wazee
  • Wanaotumia Mpira wa mkojo maarufu kama Catheters
  • Waliopo kwenye Tiba ya mionzi(radiotherapy treatment)
  • Wenye matatizo ya Figo
  • Wenye Ugonjwa wa Kisukari
  • Wenye maambukizi ya UTI hapo awali
  • Wanaojisaidia kwenye mazingira machafu; mfano ya vyoo vichafu, maji machafu n.k

Kwa ujumla, wanawake wana uwezekano mkubwa wa kupata UTI kuliko wanaume, huku asilimia 40-60% ya wanawake wakipata maambukizi angalau mara moja katika maisha yao na asilimia 10% ya wanawake wanapata UTI mara moja kwa mwaka. Wanawake wako katika hatari zaidi kuliko wanaume kwa sababu mrija wao wa mkojo ni mfupi, ambayo inafanya iwe rahisi kwa bakteria kuingia kwenye kibofu.

Dalili za Ugonjwa wa UTI

Dalili za ugonjwa wa UTI tumezigawanya katika makundi mbali mbali ya watu mfano;

  • wazee,
  • watoto,
  • wanaume,
  • wanawake,
  • wajawajazito n.k

Kwa Ujumla,Nazo ni kama ifuatavyo;

– Kuhisi mkojo mara kwa mara na Kukojoa mara kwa mara

– Kupata maumivu,usumbufu wowote au kuhisi kuungua wakati wa kukojoa

– Kuhisi Mkojo kwa ghafla

– Mkojo kutoa harufu mbaya sana, na wakati mwingine kuwa kama na vidamu damu

– Kuhisi uchovu wa mwili kupita kiasi

– Kupata maumivu ya misuli,joints pamoja na mifupa

– Kuhisi maumivu ya kichwa

– Kuhisi homa

Ikiwa maambukizi yamepanda mpaka sehemu ya juu kwenye mfumo wa mkojo(upper urinary tract) inaweza kusababisha;

  • Homa: nyuzijoto 100.4 ºF (38 ºC)  au Zaidi
  • Hali kama ya kuchanganyikiwa
  • Kupata maumivu makali ya mgongo
  • Mwili kutetemeka sana
  • Kuhisi kichefuchefu na kutapika

Bacteria ambao husababisha Zaidi UTIs ni pamoja na;

– Escherichia coli

– Protus mirabilis

– Enterococcus faecalis

– Staphylococcus saprophyticus

– Klebsiella pneumoniae

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments