Ticker

6/recent/ticker-posts

Wajawazito Kunufaika na Vifaa vya Kujifungulia



Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount leo Januari 18, 2023 wamegawa zawadi ya vifaa vya kujifungulia (Delivery Kit) kwa Wajawazito waliofika hospitalini hapo kupata huduma ya kujifungua ambazo inajumuisha vifaa muhimu vinavyohitajika pindi pale mama atakapokuwa anapata huduma ya kujifungua vilivyotolewa na wadau .

Mganga Mfawidhi wa Mount Meru, Dkt Alex Ernest ameeleza kuwa vifaa hivyo vimetolewa na wadau katika kuunga mkono juhudi za maboresho ya huduma za Afya yanayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Afya chini ya Waziri mwenye dhamana Mhe. Ummy Mwalimu katika kuhakikisha usimamizi wa utoaji huduma bora za Afya na kuhakikisha fedha za maboresho ya miundo mbinu, vifaa tiba na dawa zinafika kwa wakati ndani ya hospitali.

Aidha, ameongeza kuwa hospitali imekuwa na utaratibu wa kutoa zawadi hizo kwa wagonjwa wanaolazwa kwa lengo la kuwawezesha kuendelea na matibabu hasa pale wanapokuwa na uhitaji.

Nae, Muuguzi Mfawidhi wa Mount Meru Bi. Simphorosa Silalye amesema kwamba hospitali imeboresha huduma za matibabu ikiwemo huduma ya mama na mtoto kuanzia maeneo ya kujifungulia (labor ward) pamoja na wodi za kupumzikia kabla na baada ya kujifungua na ametoa rai kwa wadau na wananchi kwa ujumla kuendeleza desturi yakutoa misaada kwa wagonjwa waliopo hospitali kwani uhitaji ni mkubwa na ameeleza kuwa hili zoezi ni endelevu linalofanyika kwa mwaka mzima na misaada hiyo inawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa na wadau hao.



Post a Comment

0 Comments