Ticker

6/recent/ticker-posts

Chanzo cha Homa ya manjano kwa watoto wachanga



Chanzo cha Homa ya manjano kwa watoto wachanga

Homa ya manjano kwa watoto wachanga ni tatizo ambalo husababisha ngozi ya mtoto kubadilika rangi na kuwa manjano, tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama Jaundice.

Tatizo hili la homa ya manjano kwa watoto wachanga(Jaundice) husababishwa na kukusanyika kwa bilirubin kwenye damu ya Mtoto.

Hii Inatokea kwa sababu ini la mtoto bado halijakomaa vya kutosha ili kuondoa bilirubini. Homa ya manjano ni ya kawaida sana kwa watoto,na kwa kawaida huisha yenyewe, Ila Wakati mwingine watoto wanahitaji matibabu ya Mwanga(phototherapy) ili kukabiliana na tatizo hili.

Bilirubin ni dutu za njano mwili mwako ambazo huundwa wakati seli nyekundu za damu zinapovunjwa. Unapokuwa mjamzito, ini lako huondoa bilirubini kwa mtoto wako. Lakini baada ya kuzaliwa, ini la mtoto wako lazima lianze kuondoa bilirubini,

Ikiwa ini la mtoto wako halijakomaa vya kutosha, huenda lisiweze kuondoa bilirubini. bilirubini inapoanza kujikusanya, ngozi ya mtoto wako yaweza kubadilika na kuonekana ya manjano.

Jaundice hatari zaidi huweza kutokea ikiwa mtoto ana;

> Maambukizi kwenye damu-blood infection (sepsis).

> Alipata shida sana ikiwemo kuchubuka wakati wa kuzaliwa

> Ana kiwango kikubwa sana cha seli nyekundu za damu(Too many red blood cells).

> Ana kiwango kidogo cha Oxygen(hypoxia).

> Ana matatizo kwenye Ini kama vile tatizo la biliary atresia nk.

Aina za Manjano kwa Mtoto

Kuna aina mbali mbali za manjano kwa mtoto ikiwemo;

  • Physiological jaundice, Hii ndyo aina ambayo huwapata watoto wengi zaidi, na mara nyingi hutokea siku mbili au tatu baada ya mtoto kuzaliwa. Aina hii sio hatari na huisha yenyewe ndani ya wiki mbili.
  • Breastfeeding jaundice, Hii ni aina ya manjano ambayo hutokana na unyonyeshaji, aina hii hutokea kwenye wiki ya kwanza baada ya mtoto kuzaliwa, na chanzo chake kikubwa ni pale ambapo mtoto hapati maziwa ya kutosha.
  • Breast milk jaundice, Aina hii hutokana na baadhi ya vitu vilivyomo kwenye maziwa yako ambapo huathiri uwezo wa ini la mtoto kuvunja bilirubin. bilirubin ikikusanyika ndipo tatizo la manjano hutokea. Aina hii hutokea baada ya wiki ya kwanza toka mtoto kuzaliwa na huweza kuchukua mwezi au zaidi kuisha.
  • Aina zingine  hutokana na mtoto mwenyewe kuwa na matatizo ya kiafya

Dalili za Homa ya manjano kwa watoto wachanga

Dalili kubwa za tatizo hili la manjano kwa watoto ni pamoja na;

– Ngozi ya mtoto kubadilika rangi na kuwa manjano, unaweza kuona vizuri hali hii mtoto akiwa kwenye mwanga mfano mbele ya dirisha,

Mara nyingi Hali hii ya manjano huanza kuonekana usoni kwa mtoto kwanza.

– pia kwenye macho ya mtoto na chini ya ulimi huweza kuonekana manjano,

ndipo bilirubin ikiongezeka zaidi,manjano husambaa kwenye maeneo mengine kama  vile;

  • Kifuani
  • Tumboni
  • Miguuni
  • Kwenye mikono n.k

Pia inaweza kuwa vigumu kugundua haraka tatizo la manjano kwa mtoto ikiwa ana ngozi nyeusi, hali hii utaigundua haraka kwa mtoto mweusi kwenye macho na chini ya Ulimi.

Vipimo vya Manjano kwa Mtoto

– Kitu cha kwanza,kugundua tatizo la homa ya manjano kwa mtoto ni kupitia dalili atakazozionyesha; ikiwemo dalili kubwa ya kubadilika rangi ya ngozi na kuwa manjano.

– Njia nyingine ni kuchunguza kiwango cha bilirubin kwa mtoto, ambapo mojawapo ya Vipimo ni kutumia kipimo cha damu(Blood test) ili kugundua total serum bilirubin (TSB) level.

Kwa mujibu wa “The American Academy of Pediatrics” wameelezea tatizo la manjano kwa Watoto, na kuonyesha baadhi ya viwango vya bilirubin ikiwa vimezidi kulingana na umri wa mtoto kama ifuatavyo,

“Total serum bilirubin (TSB) level” ikiwa hivi mtoto huwa na manjano;

  • Kubwa kuliko millligrams 10 kwa mtoto mwenye umri wa chini ya saa 24
  • Ikiwa kubwa kuliko milligrams 15 kwa mtoto mwenye umri wa saa 24 mpaka 48
  • Kubwa kuliko milligrams 18 kwa mtoto mwenye umri wa saa 49 mpaka 72
  • Kubwa kuliko milligrams 20 kwa mtoto mwenye umri wa zaidi ya Saa 72

Matibabu ya Homa ya Manjano kwa Watoto wachanga

✓ Tatizo la homa ya Manjano likiwa kwa kiwango kidogo sana(Mild levels of jaundice)huweza kupotea lenyewe pasipo hata tiba,

Na hii huweza kuchukua wiki moja mpaka mbili, hapa mama atashauriwa tu kumnyonyesha mtoto vizuri mara 10 mpaka 12 kwa siku, Hii itasaidia mtoto kujisaidia sana na kuondoa kiwango cha bilirubin kilichozidi mwilini kupitia kinyesi.

✓ Tiba ya mwanga(phototherapy), Mtoto ataanza kupata tiba hii ikiwa kiwango cha bilirubin ni kikubwa au kinaendelea kupanda.

✓ Na kwa kesi chache sana za watoto ambazo Tiba ya mwanga(phototherapy) haikusaidia, wataalam wa afya watashauri Tiba inayojulikana kama exchange transfusion.

ambapo kiwango flani cha damu ya mtoto hubadilishwa na kuwekewa damu nyingine ya mtu ambayo haina shida.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments