Dalili za kukosa choo,chanzo chake na Tiba

Dalili za kukosa choo,chanzo chake na Tiba

Ikiwa mtu hajapata Choo kwa wiki nzima, lakini anahisi vizuri, anapaswa kutafuta ushauri wa matibabu hata kama anajiona yupo Sawa.

Na upande wa kupata Choo ni Mara ngapi kwa Siku ambapo ni Sawa kiafya tazama hapa.Muda Sahihi wa kupata Choo kwa Siku.

Kwa wengine, kukosa Choo mara kwa mara hutokana na mabadiliko machache ya mtindo wa maisha au mabadiliko ya lishe, au kwa kutumia baadhi ya dawa.Watu wenye tatizo la kukosa choo kupita kiasi wanaweza kuhitaji matibabu.

Dalili za kukosa choo

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za tatizo la Kukosa Choo unazoweza kuzipata;

1. Kupata choo chini ya mara tatu(3) kwa muda wa wiki nzima

2. Wakati ukijisaidia kinyesi kinakua kigumu na kimekauka

3. Unapata shida sana ya kujisaidia au unapata maumivu sehemu ya haja kubwa hata wakati choo kinatoka

4. Unapata maumivu ya tumbo au tumbo kukaza

5. Unahisi tumbo kujaa lakini ukijisaidia hamna kitu

6. Kuhisi hali ya kichefuchefu mara kwa mara

7. Baada ya Kujisaidia lakini bado unahisi kuna kitu kimebaki ndani(kama bado hujajisaidia ukamaliza) n.k

Ikiwa unakosa Choo lakini pia unapata dalili hizi hakikisha unawahi kwenye matibabu au kwa Ushauri Zaidi tuwasiliane ndani ya @afyaclass;

  • Unapata Maumivu makali sana ya Tumbo
  • Tumbo kuvimba
  • Unahisi kichefuchefu na kutapika
  • Unapata Homa
  • Unapata Maumivu makali ya Mgongo
  • Unajisaidia Damu n.k

Chanzo cha kukosa choo

Kuna Sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia tatizo la kukosa Choo ikiwemo;

– Kutokula vyakula vyenye nyuzi nyuzi(fibers) za kutosha

– Kutokunywa maji ya kutosha au kuwa na tatizo la Upungufu wa maji mwilini

– Kutokufanya Mazoezi ya mwili

– Kubadilisha mazingira na kwenda Sehemu ya Ugenini

– Kutumia kwa kiwango kikubwa sana Maziwa au bidhaa za maziwa

– Kuwa na Msongo wa Mawazo

– Matumizi ya baadhi ya dawa, Mfano wa dawa hizo ni kama vile;

  • Dawa jamii ya Strong pain medicines, kama zile zenye narcotics mfano;codeine, oxycodone (Oxycontin®) na hydromorphone (Dilaudid®).
  • Dawa jamii ya Nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs), kama vile ibuprofen (Advil®, Motrin®) na naproxen (Aleve®).
  • Dawa jamii ya Antidepressants, kama vile selective serotonin reuptake inhibitors (mfano fluoxetine [Prozac®]) au tricyclic antidepressants (mfano amitriptyline [Elavil®]).
  • Dawa jamii ya Antacids zenye calcium au aluminum, mfano Tums®.
  • Dawa jamii ya Iron pills.
  • Dawa za mzio(Allergy medications), kama antihistamines (mfano diphenhydramine [Benadryl®]).
  • Baadhi ya dawa za shinikizo la dami kama zile zenye calcium channel blockers (mfano verapamil [Calan SR®], diltiazem [Cardizem®] na nifedipine [Procardia®]) pamoja na beta-blockers (mfano atenolol [Tenormin®]).
  • Dawa jamii ya Psychiatric medications, mfano clozapine (Clozaril®) na olanzapine (Zyprexa®).
  • Dawa jamii ya Antiseizure medications, kama vile phenytoin na gabapentin.
  • Dawa jamii ya Antinausea medications, kama vile ondansetron (Zofran®).n.k

– Kuwa na baadhi ya Matatizo ya kiafya(Medical conditions) kama vile;

  • Matatizo ya tezi la thyroid kutokufanya kazi vizuri-underactive thyroid gland (hypothyroidism),
  • Ugonjwa wa Kisukari
  • Tatizo la uremia pamoja na hypercalcemia.
  • Kuwa na Saratani kama vile ya Utumbo mpana(Colorectal cancer).
  • Kuwa na tatizo la Irritable bowel syndrome (IBS)
  • Tatizo la Diverticulitis.
  • Obstructed defecation syndrome
  • Tatizo la Intestinal pseudo-obstruction.n.k

– Kuwa na matatizo kwenye mfumo wa Nerves(Neurologic disorders) ikiwemo;

  • Tatizo la kuumia uti wa mgongo(spinal cord injury)
  • Tatizo la multiple sclerosis,
  • Ugonjwa wa Parkinson’s disease
  • Pamoja na stroke.

Ikiwa una tatizo hili la kukosa Choo hakikisha unapata Msaada wa matibabu pamoja na Vitu vya Kufanya na kuzingatia.

NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!