Dalili za mchafuko wa damu pamoja na Tiba yake

Mchafuko wa damu,chanzo,dalili na Tiba

Mchafuko wa damu; hiki ni kiswahili ambacho watu wamezoea kukitumia lakini maana yake ni “maambukizi kwenye damu-blood infection”

Endapo damu yako imepimwa na kuonekana ina viini vya magonjwa kama vile bacteria n.k utaambiwa damu yako ni Chafu au una tatizo la mchafuko wa damu.

Maambukizi kwenye damu kwa Lugha nyingine tunaita Blood Infection au kwa kitaalam Zaidi wanatumia neno “Sepsis”

Sepsis ni nini?

Sepsis ni pale ambapo mwili wako unakuwa na mwitikio mkali dhidi ya maambukizi kwenye damu. Wakati huo mfumo wako wa kinga, ambao kwa kawaida unakukinga dhidi ya vijidudu, huanza kushambulia tishu za mwili wako.

Hii husababisha uvimbe unaoweza kusababisha uharibifu wa viungo. Pia ni kawaida kwa mabonge ya damu kuundwa hali ambayo hupunguza mtiririko wa damu kwenye viungo vyako vya ndani, na kusababisha visipate virutubisho na oksijeni inayohitajika.

Mchafuko wa damu huhusisha kuwa na vimelea vya magonjwa kwenye damu, vimelea hivo ni pamoja na;

  • Bacteria(asilimia kubwa)
  • Fangasi
  • Virusi
  • Parasites

Chanzo cha Mchafuko wa damu

Kama tulivyosema, haya ni maambukizi ya viini vya magonjwa kwenye damu, viini hivi ni pamoja na bacteria, parasites, fangasi au viruses.

Unaweza kupata maambukizi kwenye damu kwa njia mbali mbali ikiwemo;

  • Kupitia IV lines kama upo hospitalini,
  • Kwenye vidonda
  • Kupitia mpira ya mkojo(urinary catheters)
  • vyakula unavyokula ikiwemo nyama n.k

Maambukizi haya huweza kupelekea tatizo la Sepsis;

– Pneumonia

– UTI-Urinary tract infections

– maambukizi kwenye kidole tumbo-appendix (appendicitis)

– Maambukizi tumboni(Abdominal infection)

– Maambukizi kwenye Ini au kifuko cha nyongo

– Maambukizi kwenye Ubongo au Uti wa mgongo

Aina ya Bacteria wanaosababisha mchafuko wa damu

Aina ya Bacteria wanaosababisha kwa kiasi kikubwa mchafuko wa Damu(Sepsis) ni pamoja na;

  • Staphylococcus aureus (S. aureus),
  • Streptococcus pyogenes (S. pyogenes),
  • Klebsiella spp.,
  • Escherichia coli (E. coli),
  • Pamoja na Pseudomonas aeruginosa (P. aeruginosa)

Watu ambapo wapo kwenye hatari ya kupata Mchafuko wa Damu

Watu ambapo wapo kwenye hatari ya kupata mchafuko wa damu ni pamoja na;

• Wenye kinga dhaifu ya Mwili

• Wenye magonjwa kama vile;

• Wajawazito

• Ambao wameshawahi kupata tatizo la mchafuko wa damu hapo kabla

• Wenye umri wa Zaidi ya miaka 65, hasa hasa ikiwa wana matatizo mengine ya kiafya

• Waliowahi kulazwa hospital kwa kuugua sana muda mrefu au kufanyiwa Upasuaji

• Wanaotumia mpira wa mkojo(Urinary cathers) au mipira ya kupumulia(breathing tubes)

• Wenye Vidonda vikubwa, kuungua au kupata majeraha mbali mbali kwenye ngozi

Dalili za Mchafuko wa damu

Hizi hapa ni baadhi ya dalili za mchafuko wa damu;

1. Kuwa na Homa

2. Mwili kutetemeka sana

3. kupata shida ya kukosa pumzi au kupumua kwa shida

4. Kuwa na dalili kama za kuchanganyikiwa

5. Joto la mwili kushuka sana

6. Kukojoa kidogo sana kuliko kawaida au kutokukojoa kabsa.

7. Mapigo ya Moyo kwenda mbio

8. Kuhisi kichefuchefu na kutapika

9. Kupata tatizo la Kuharisha

10. Mwili kuchoka sana, kuwa dhaifu au kukosa nguvu

11. Kutoa sana jasho

12. Kupata maumivu makali ikiwemo ya kichwa n.k

13. Kupata upele kwenye ngozi(Skin rashes)

14. Kuhisi kizunguzungu

15. Kuhisi usingizi sana

16. Ngozi kuwasha sana n.k

Ukiona dalili hizi hakikisha unapata Msaada Mapema au;

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!