Kuvunjika Moyo ni Ugonjwa? fahamu hapa Ugonjwa wa Moyo kuvunjika
Takotsubo cardiomyopathy au “Broken Heart Syndrome” ni tatizo ambalo hutokea kwenye moyo ambapo asilimia kubwa huhusiana na Hisia, tatizo hili limepewa jina la “Ugonjwa wa kuvunjika moyo au Broken Heart Syndrome”.
Tatizo hili hutokea pale misuli ya moyo inapopigwa na butwaa au kudhoofika ghafla. Mara nyingi hutokea kufuatia mkazo mkali wa kihisia au kimwili. Hali hiyo ni ya muda na watu wengi hupona ndani ya miezi miwili.
Ugonjwa wa moyo uliovunjika(Broken heart syndrome); ni hali ya moyo ambayo mara nyingi huletwa na hali zenye mkazo na hisia kali. Hali hiyo pia inaweza kusababishwa na ugonjwa mbaya wa mwili au upasuaji. Ugonjwa wa moyo uliovunjika kawaida ni wa muda mfupi. Lakini watu wengine wanaweza kuendelea kujisikia vibaya baada ya moyo kuponywa.
Unapofikiria juu ya moyo uliovunjika, labda unafikiria zaidi juu ya ustawi wa kimhemko au hisia kuliko afya ya moyo wako wa mwili. Lakini fahamu kuwa kuna mwingiliano kwa kiasi kikubwa.
Hiyo ni kwa sababu hali yetu ya kihisia ina athari halisi kwa hali yetu ya kimwili (na kinyume chake). Unapopatwa na matukio ya kihisia au ya kiwewe,kushtua n.k, mfumo wako wa neva huchochea homoni za mafadhaiko, kama vile adrenaline na epinephrine.
Hiyo ni kawaida. Lakini mara chache, na kwa sababu ambazo hazieleweki vizuri, mtu aliye na shida ya kihisia anaweza kupata tukio la mashambulizi ya moyo,linaloitwa ugonjwa wa moyo uliovunjika au broken heart syndrome.
Hali hii inaweza kuiga mshtuko wa moyo ambao tunaujua kama heart attack lakini mashambulizi ya moyo haya(heart attack) kwa kiasi kikubwa husababishwa na kuganda kwa damu kwenye mishipa ya arteries.
Fahamu,Kufuatia hali ya kushtushwa na hisia, unapata ongezeko kubwa la vichocheo au hormones aina ya adrenaline – zaidi ya kawaida kama matokeo au majibu dhidi ya hisia.
Kuongezeka kwa kasi kwa homoni hizi kunaweza kusababisha misuli ya moyo wako kushindwa kusinyaa kama kawaida(contracts), na hivyo kusababisha tatizo la Moyo kushindwa kufanya kazi kwa muda mfupi.
Dalili za ugonjwa wa moyo kuvunjika(Broken heart syndrome)
Dalili za ugonjwa wa moyo uliovunjika zinaweza kufanana kama za mshtuko wa moyo au shambulio la moyo(Heart attack) dalili hizo ni pamoja na:
?kupata Maumivu ya ghafla na makali ya kifua.
?Kukosa pumzi.
?Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.
?Kupata Shinikizo la chini la damu.
?Kuzimia.n.k
Chanzo cha ugonjwa wa moyo kuvunjika(Broken heart syndrome)
Mpaka sasa,Sababu halisi ya ugonjwa wa moyo uliovunjika haijulikani. Inafikiriwa kuwa kuongezeka kwa homoni za mafadhaiko, kama vile adrenaline, kunaweza kuharibu mioyo ya watu wengine kwa muda mfupi.
Lakini haifahamiki Jinsi homoni hizi zinavyoweza kuumiza moyo au ikiwa ni kitu kingine ndicho chanzo, hyo haifahamiki kabisa.
kumbuka; Ukiwa unapata dalili zozote kati ya hizi, hakikisha unapata Msaada wa kitaalam au;
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!