kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba
kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida hii ikiwemo matatizo ya ngozi kama vile psoriasis, eczema, au tatizo la athlete’s foot. Na hata tiba sahihi ya shida hii ya kuwashwa nyayo za miguu hutegemea na chanzo chake.
Ingawa mara kwa mara unaweza kuwashwa nyayo za miguu hali ambayo haiwezi kuwa chochote cha kuwa na wasiwasi, Kuwashwa nyayo za miguu kupita kiasi au muwasho usiopata nafuu unaoendelea baada ya muda huenda ukahitaji matibabu.
kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini?
Hizi ni baadhi ya Sababu kubwa ambazo huweza kupelekea tatizo la kuwashwa nyayo za miguu;
1. Tatizo la kwenye nerves(Peripheral neuropathy)
Tatizo hili huhusisha uharibifu wa nerves kwenye maeneo kama vile miguuni n.k ambapo baadae husambaa kwenye sehemu zingine za mwili.
Kwa mujibu wa Taasisi moja inayojulikana kama “National Institute of Neurological Disorders and Stroke” inaelezea tatizo la peripheral neuropathy kama; uharibifu wa mfumo wa fahamu kwenye maeneo ya pembeni mwa mwili yaani “peripheral nervous system* ambapo huja kusambaa hadi kwenye mwili wote.
Uharibifu huu wa Nerves huweza kusababisha dalili mbali mbali ikiwemo;
- Kuwashwa kwenye maeneo mbali mbali ya mwili ikiwemo kwenye nyayo za miguu
- Miguu kufa ganzi
- Kuhisi maumivu kwenye maeneo mbali mbali ya mwili ikiwemo miguuni n.k
2. kuwa na tatizo la ngozi kavu(Dry skin)
Tatizo hili la ngozi kuwa kavu kuna wakati huweza kupelekea mtu kupata muwasho kwenye maeneo mbali mbali ya mwili ikiwemo kwenye nyayo za miguu,
Upakaji wa mafuta huweza kusaidia kupunguza tatizo la muwasho na ngozi kuwa kavu.
Tatizo la Ngozi kuwa kavu(dry skin) huweza kutokana na Sababu mbali mbali ikiwemo;
- Umri mkubwa
- Kukaa kwenye maeneo yenye ukame(dry climate)
- Kukaa kwenye mazingira ya maji mara kwa mara
- Kuogelea kwenye maji yenye chlorine(chlorinated water) n.k
Ikiwa mtu ana ngozi kavu kwenye miguu yake, anaweza kupata Muwasho. Kupaka krimu, losheni, au mafuta kunaweza kusaidia.
Ikiwa vilainishi vya kawaida havifanyi kazi, hakikisha unapata tiba kutoka kwa wataalam wa afya au kwa Ushauri Zaidi na Tiba tuwasiliane ndani ya @afyaclass
3. Tatizo la Psoriasis
Psoriasis ni hali ya ngozi ambayo husababisha vidonda, ngozi kuwa nyekundu na yenye magamba. Hali hii Inaweza kuathiri karibu sehemu yoyote ya mwili, ikiwa ni pamoja na miguu.
Tatizo la Psoriasis linaweza kusababisha muwasho sana kwenye ngozi na maumivu, na moja ya maeneo smbayo huweza kuathiriwa ni pamoja na kwenye nyayo za miguu.
Hali hii ya Psoriasis inatokea wakati mfumo wa kinga kwa mtu unapoanza kushambulia seli za ngozi zenye afya. Hii inaharakisha uzalishaji wa seli hizi, na kusababisha upele.
Matibabu kwa kawaida hujumuisha krimu na losheni ambazo zinaweza kuwa na laini,salicylic acid, corticosteroids, au mchanganyiko wa hivi vyote.
kwa Ushauri Zaidi na Tiba tuwasiliane ndani ya @afyaclass
4. Tatizo la Pumu ya ngozi(Eczema)
Eczema, pia hujulikana kama atopic dermatitis, na kwa lugha rahisi hujulikana kama Pumu ya ngozi;
Hali hii huambatana na ngozi kuwa kavu sana na kupata muwasho sana, na huweza kuathiri maeneo mbali mbali ya mwili ikiwemo miguuni.
Dyshidrotic eczema; ni aina ambayo mara nyingi inaonekana kwenye pande na nyayo za miguu. Husababisha malengelenge madogo, ya kina, yanayowasha sana. Wanawake wana uwezekano mara mbili wa kupata aina hii ya pumu ya ngozi(eczema).
Watu wanaweza kutibu muwasho unaotokana na ukurutu mdogo wa dyshidrotic kwa kuloweka miguu yao kwenye maji baridi au kutumia vitu vya baridi na unyevunyevu kwenye eneo hilo.
Ikiwa eczema ni kali zaidi, daktari anaweza kuagiza creams au kupendekeza ufumbuzi wa OTC. Au kwa Ushauri Zaidi na Tiba tuwasiliane ndani ya @afyaclass
5. Tatizo la Fangasi kwenye Ngozi(Athlete’s foot)
Fangasi wanaweza kukua ndani ya viatu vya wanamichezo na kusababisha tatizo ambalo hujulikana kama athlete’s foot.
Athlete’s foot; ni ugonjwa wa Fangasi kwenye ngozi ambao kwa kawaida hutokea katikati ya vidole vya miguu, ingawa unaweza pia kuathiri sehemu nyingine za miguu.
Matokeo yake husababisha muwasho pamoja na kuhisi hali ya kuungua kwenye eneo lililoathiriwa(itching and burning sensation). Hivo basi,kuwashwa nyayo za Miguu huweza kutokana na Mashambulizi ya Fangasi.
Fangasi hustawi kwenye hali ya joto, unyevunyevu na giza, kama vile ndani ya viatu vya michezo. Kuongezeka kwa fangasi hizi kunaweza kusababisha tatizo la athlete’s foot.
Dawa jamii ya antifungal, ambayo huja kama vidonge au lotions, kwa kawaida ni nzuri sana katika kutibu tatizo la athlete’s foot.
6. Tatizo la Mzio au Allergy(Allergic reactions)
Fahamu tatizo la Mzio au allergy ya ngozi huweza kupelekea mtu kupata tatizo la Muwasho kwenye maeneo mbali mbali ya ngozi ikiwemo kwenye nyayo za miguu.
Mzio wa ngozi unaweza kusababisha muwasho. Lakini pia huweza kutokana na hali fulani za ngozi, kama vile eczema au psoriasis au kutokana na kugusana na vitu kama vile mpira,chavua(pollen),vumbi,kemikali yoyote n.k.
Kutumia dawa jamii za antihistamines inaweza kusaidia kudhibiti dalili za Mzio au allergies. Dawa hizi huja kama vidonge au krimu za kupaka. kwa Ushauri Zaidi na Tiba tuwasiliane ndani ya @afyaclass
7. Maambukizi ya Minyoo(Hookworm infections)
Watu wengi hawafahamu kwamba minyoo huweza kusababisha madhara makubwa mwilini ikiwemo;
- Kikohozi ambacho hakiishi
- Kupungukiwa na Damu
- Muwasho kwenye ngozi n.k
Hookworm; ni aina ya vimelea vya minyoo(parasitic-worms) vinavyoishi kwenye utumbo wa binadamu. Watu wanaweza kupata minyoo kwa kutembea bila viatu katika maeneo ambayo mabuu wapo. Maambukizi ya minyoo ni nadra sana katika maeneo yenye usafi wa kutosha.
Kulingana na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), mtu anaweza kupata Muwasho mahali ambapo mabuu ya minyoo waliingia kwenye mwili wake.
Hivo endapo minyoo hawa wameingia mwilini kupitia kwenye nyayo za miguu hasa baada ya kutembea bila viatu huweza kupelekea tatizo la kuwashwa sana kwenye nyayo za miguu walipoingilia.
8. Tatizo la Scabies
Scabies huweza kutokea wakati mites wadogo sana wanapoingia kwenye ngozi ya mtu na kuweka mayai, kisha kusababisha upele unaowasha sana.
Hali hiyo inaambukiza na husafiri kwa mgusano wa ngozi hadi ngozi. Inaweza kutokea mahali popote kwenye mwili, ikiwa ni pamoja na miguuni.
Soma Zaidi hapa kuhusu tatizo hili la Scabies,chanzo,dalili na Matibabu
9. Ugonjwa wa kisukari(Diabetes)
Ugonjwa wa kisukari ni hali ya muda mrefu ambayo huathiri upinzani wa insulini na jinsi mwili hubadilisha chakula kuwa nishati. Inaweza kumaanisha kwamba viwango vya sukari kwenye damu ya mtu ni vikubwa sana, ambapo inaweza kuwa na madhara makubwa kiafya.
Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababisha tatizo la diabetic neuropathy, ambapo matokeo yake yanaweza kupelekea mtu kupata matatizo kama vile;
- kuwashwa kwenye ngozi maeneo mbali mbli ya mwili ikiwemo kwenye nyayo za miguuni,
- Kupata tatizo la kufa ganzi, haswa kwenye miguu.n.k
Mzunguko duni wa damu kwa sababu ya ugonjwa wa sukari pia unaweza kusababisha tatizo la kuwashwa. Pia, kuwa na kisukari kunaweza kuongeza hatari ya mtu kupata maambukizi ya bakteria na fangasi.
Soma Zaidi hapa: Ugonjwa wa Kisukari,chanzo,dalili na Madhara yake mwilini.
10. Kuungua(Burns)
Hata baada ya kupona, kuungua sana kunaweza kusababisha uharibifu wa kudumu na uwepo wa tatizo la kuwasha kwa ngozi.
Kulingana na utafiti wa 2013, zaidi ya asilimia 90% ya washiriki waliripoti kuwashwa kwenye ngozi baada ya kuchomwa au kuungua. Kwa zaidi ya asilimia 40% ya washiriki, kuwasha kuliendelea kwa muda mrefu.
Hivo ikiwa umeungua maeneo kama vile miguuni kwenye nyayo unaweza kukutana na tatizo lingine la muwasho kwenye nyayo hata baada ya kupona.
Kumbuka; Ikiwa una tatizo la Kuwashwa kwenye nyayo za Miguu hakikisha unapata matibabu sahihi kulingana na chanzo husika au;
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!