Connect with us

Magonjwa

Ugonjwa wa eczema,Ukurutu au Pumu ya Ngozi,chanzo chake,Dalili na Tiba

Avatar photo

Published

on

Ugonjwa wa eczema,Ukurutu au Pumu ya Ngozi,chanzo chake,Dalili na Tiba

Eczema ni ugonjwa wa ngozi ambao huhusisha hali ya mabaka mabaka ya ngozi,ngozi kuwaka moto, kuwasha, kupasuka n.k. Aina zingine za Eczema zinaweza pia kusababisha malengelenge.

Tatizo hili la Eczema hujulikana kama Ugonjwa wa Ukurutu au Pumu ya Ngozi,

Watu wengi hutumia neno ukurutu(eczema) wanapohusisha Atopic dermatitis ambayo ndiyo aina inayojulikana zaidi. Aina hii ya atopic dermatitis huhusisha zaidi mfumo wa kinga ya mwili, ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa ngozi au kuvimba kwa ngozi, pumu na Homa za mara kwa mara.

Vyakula vingine, kama vile karanga na maziwa, vinaweza kusababisha dalili zaidi za eczema pamoja na Vichochezi vya mazingira kama moshi, baadhi ya sabuni, baadhi ya mafuta ya kupaka na kupikia,manukato n.k

DALILI ZA UGONJWA HUU WA ECZEMA(UKURUTU AU PUMU YA NGOZI)

Dalili za ugonjwa Huu zinaweza kutofautiana kulingana na umri wa mtu, ukali wa hali hiyo na zinaweza kutofautiana kwa mtu na mtu.

(1). Dalili za jumla za eczema ni pamoja na:

– Ngozi kuwa kavu sana na magamba

– Mtu kupata shida ya ngozi kuwasha

– Kuhisi hali ya kuungua sana kwenye ngozi

– Ngozi kuwa nyekundu kwenye baadhi ya maeneo

– Ngozi kubadilika na kuwa na mabaka mabaka yanayowasha, na wakati mwingine kuwa na upele,malenge lenge au vidonda. N.K

(2). Dalili za Eczema kwa watoto wachanga

Dalili zifuatazo za ugonjwa huu wa ngozi ni kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 2:

– vipele juu ya kichwa na mashavu

– vipele vinavyotoka kabla ya kuvuja maji

– upele ambao unaweza kusababisha Muwasho sana, na kusababisha mtoto kushindwa kulala

(3). Dalili za eczema kwa watoto wa Miaka 2 na Zaidi.

Dalili zifuatazo za ugonjwa huu wa ngozi ni kwa watoto wenye umri wa miaka 2 na zaidi:

– upele unaoonekana nyuma ya mikunjo ya viwiko au magoti

– vipele vinavyoonekana kwenye shingo, viganja vya mkono, vifundoni na mpasuko kati ya matako na miguu.

– vipele vya matuta

– vipele vinavyoweza kuwa vidogo vidogo sana na vyeusi zaidi

– Ngozi kuvimba au kuwa nene zaidi kwa kitaalam hujulikana kama lichenification, na kuwa na muwasho wa kudumu,

Watoto wengi walio na hali hii huipata kabla ya umri wa miaka 5.

(4). Dalili za Eczema kwa watu wazima

Dalili zifuatazo za ugonjwa huu wa ngozi hutokea kwa watu wazima:

– vipele ambavyo vina magamba zaidi kuliko vinavyotokea kwa watoto

– vipele ambavyo kwa kawaida huonekana kwenye mikunjo ya viwiko au magoti au sehemu ya shingo.

– vipele vinavyofunika sehemu kubwa ya mwili

– ngozi kuwa kavu sana kwenye maeneo yaliyoathirika

– vipele ambavyo huwashwa sana n.k

CHANZO CHA UGONJWA HUU WA NGOZI NI NINI?

Ugonjwa huu wa eczema(Ukurutu au Pumu ya ngozi) huweza kuhusishwa na sababu mbali mbali ikiwemo;

• Sababu za Kigenetics, ambapo vinasaba vya tatizo hili huweza kutokea kwenye familia,

Watu ambao wana ndugu wenye shida hii ya Eczema, wenye Asthma au seasonal allergies wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu wa ngozi.

• Tatizo la kiutendaji kwenye mfumo wako wa kinga ya Mwili

• Pia baadhi ya tafiti zinaonyesha tatizo hili huweza kutokea kwa wakina mama ambao wanapata watoto kwenye umri mkubwa sana kuliko wale ambao wanajifungua mapema

• Sababu za kimazingira,ikiwemo uchafuzi wa mazingira,kukaa sehemu zenye kemikali za sumu zaidi,n.k

• Matatizo mengine ya ngozi ambayo huweza kuhusisha ngozi kuwa na jeraha,na kuruhusu maji maji kutoka nje pamoja na vimelea vya magonjwa kupenya ndani

• Matatizo kama Endocrine disorders ikiwemo thyroid disease n.k

MATIBABU YA UGONJWA HUU WA NGOZI

Kwa sasa hakuna tiba ya eczema,Matibabu huhusisha zaidi kudhibiti dalili za ugonjwa huu ikiwemo ngozi iliyoathirika.

(1)Mambo ambayo unaweza kufanya ukiwa nyumbani;

Kuna mambo kadhaa ambayo watu wenye eczema wanaweza kufanya ili kusaidia afya ya ngozi na kupunguza dalili.

Mambo hayo ni kama vile;

– kuoga kwa maji ya uvuguvugu

– kupaka moisturizer ndani ya dakika 3 baada ya kuoga

– Kuhakikisha ngozi haiwi kavu kila siku kwa kupaka mafuta n.k

– Kuvaa nguo za pamba pamoja na vitambaa laini, na kuepuka nguo za kubana sana na zenye nyuzi mbaya ambayo huweza kuleta mikwaruzo.

– Kuepuka matumizi ya sabuni zenye kemikali zaidi,mafuta ya kupaka au manukato ya aina yoyote.

– kuweka kucha fupi ili kuzuia mikwaruzo kwenye ngozi.

Watu wanaweza pia kujaribu tiba mbalimbali za asili za ukurutu, ikiwa ni pamoja na aloe vera, mafuta ya nazi n.k

DAWA;

Zipo dawa kadhaa ambazo huweza kutumika kudhibiti dalili za eczema kama vile:

âś“ Dawa za kupaka(Topical corticosteroid creams and ointments):

✓ Dawa za vidonge vya kunywa(Oral medications): Jamii ya corticosteroids au immunosuppresants.

✓ Dawa jamii ya Antibiotics,Antihistamines: n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ushauri|Tiba|CheckIn 🩺🌡️ContactUs; +255758286584 or INBOX📩. For More Healthtips everyday Link In https://afyaclass.com Also Follow us on Instagram @afyaclass

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa4 weeks ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa1 month ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa2 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa2 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa3 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake4 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa1 day ago

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa2 days ago

Ugonjwa unaosababishwa na kula nyama mbichi

Ugonjwa unaosababishwa na kula nyama mbichi Madhara ya kula nyama ya ng’ombe mbichi Ni desturi ya baadhi ya watu kula...

Magonjwa1 week ago

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani Mkojo kuuma au kupata maumivu wakati wa kukojoa ni hali ambayo kwa kitaalam...

Magonjwa1 week ago

Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono dalili Zake

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa2 weeks ago

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu Haya ni maneno ambayo umekuwa ukiyasikia sana linapokuja swala la vipimo cha UKIMWI, je...

Magonjwa3 weeks ago

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia. Kutana na Ilene Raymond Rush ambaye aligunduliwa Kisukari aina ya Pili(Type 2...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa unaosababishwa na konokono

Ugonjwa unaosababishwa na konokono Ugonjwa unaosababishwa na konokono unaitwa schistosomiasis, au bilharzia. Ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na minyoo wanaoitwa...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake. Wengi tumesikia kuhusu Red Eyes(Macho mekundu) Lakini je umewahi kusikia kuhusu Pink Eyes,?...

Magonjwa3 weeks ago

Omeprazole inatibu ugonjwa gani,Fahamu hapa

Omeprazole inatibu ugonjwa gani Omeprazole inatibu ni nini?, Hili ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara kwa mara na wafwatiliaji wengi...

Magonjwa4 weeks ago

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani Mate kujaa Mdomoni,ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watu, na zipo...