Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani

Mkojo kuuma au kupata maumivu wakati wa kukojoa ni hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Dysuria (Painful Urination)

Dysuria inamaanisha unahisi maumivu au hisia ya kuungua wakati unapokojoa (kukojoa). Wanaume na wanawake wa umri wowote wanaweza kupata dysuria, lakini ni kawaida zaidi kwa wanawake.

Maambukizi ya mfumo wa mkojo(UTI) mara nyingi huhusishwa na dysuria, Matibabu ya hali hii ya kuumia wakati wa kukojoa hutegemea na sababu au chanzo chake.

Mkojo kuuma au Dysuria sio ugonjwa bali ni dalili ya tatizo au ugonjwa flani, na mara nyingi hali hii huambatana na hali ya kukojoa mara kwa mara.

Nani anaweza kupata shida hii ya Mkojo kuuma au Dysuria

Wanaume na wanawake wa umri wowote wanaweza kupata shida hii ya mkojo kuuma, Ingawa hali hii Ni kawaida zaidi kwa wanawake. Maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTIs) mara nyingi huhusishwa na dysuria. UTI hutokea kwa wanawake zaidi kuliko kwa wanaume.

Watu wengine walio katika hatari kubwa ya kupata shida ya Mkojo kuuma au dysuria ni pamoja na:

  • Wanawake wajawazito.
  • Wanaume na wanawake wenye ugonjwa wa kisukari.
  • Wanaume na wanawake wenye aina yoyote ya ugonjwa wa kibofu.

Chanzo cha Mkojo kuuma ni nini?

Sababu Zinazowezekana tumezigawanya kulingana na jinsia ya mtu, kama ifuatavyo;

WANAWAKE: Kukojoa kwa uchungu kwa wanawake kunaweza kuwa matokeo ya:

– Maambukizi ya kibofu (cystitis).

– Maambukizi ya uke

– Maambukizi ya njia ya mkojo au UTI

– Tatizo la Endometritis na sababu nyingine nje ya maambukizi kwenye njia ya mkojo, ikiwa ni pamoja na tatizo la diverticulosis na diverticulitis.

– Kuvimba kwa kibofu cha mkojo au urethra (urethritis) (Urethra ni mrija unaoanzia sehemu ya chini ya kibofu chako na kutoka nje ya mwili wako),

Kuvimba kwa kawaida husababishwa na maambukizi.
Kuvimba kunaweza pia kusababishwa na kujamiiana, matumizi ya douchi, baadhi ya sabuni,Toilet paper, sponji za kuzuia mimba au dawa za kuua manii.n.k.

WANAUME: Kukojoa kwa uchungu kwa wanaume kunaweza kuwa ni matokeo ya:

+ Maambukizi ya mfumo wa mkojo(UTI) na maambukizi mengine nje ya njia ya mkojo, ikiwa ni pamoja na diverticulosis na diverticulitis.

– Ugonjwa wa Saratani ya Tezi dume(Prostate cancer)

NB; Pia Mkojo kuuma kwa wanaume na wanawake kunaweza kuwa ni matokeo ya magonjwa ya zinaa (STIs) au athari ya dawa. Dawa za saratani au chemotherapy au matibabu ya mionzi kwenye eneo la fupanyonga huweza kusababisha kuvimba kwa kibofu cha mkojo na kusababisha kukojoa kwa maumivu.

Vipimo vya Kufanya ili kugundua Ugonjwa

  1. Kuchukua historia ya mgonjwa,ikiwemo kujua kama una historia ya magonjwa kama kisukari, upungufu wowote wa Kinga mwili n.k
  2. Kipimo cha Mkojo
  3. Kipimo cha magonjwa ya Zinaa n.k

Matibabu ya Mkojo Kuuma

Matibabu ya dysuria yanategemea sababu ya maumivu yako / hisia ya kuungua wakati wa kukojoa. Hatua ya kwanza katika matibabu yako ni kubaini kama kukojoa kwako kwa uchungu kunasababishwa na maambukizi, kuvimba, vipengele vya lishe, au tatizo la kibofu chako cha Mkojo.

Maambukizi ya mfumo wa mkojo(UTI) mara nyingi hutibiwa na dawa jamii ya antibiotics

Pia Zingatia baadhi ya Mambo muhimu kama vile;

  • Hakikisha unakunywa maji ya kutosha
  • Hakikisha usafi wako binafsi,ikiwemo nguo za ndani,vyoo n.k
  • Jikinge na magonjwa ya Zinaa(STDs) n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!