Connect with us

Uzazi/Ujauzito

Dalili za uchungu wiki ya 37,Soma hapa kufahamu

Avatar photo

Published

on

Dalili za uchungu wiki ya 37,Soma hapa kufahamu

Wiki ya 37 ya ujauzito uumbaji wa mtoto unakuwa umekamili na huweza kuishi bila uangalizi maalumu akizaliwa. Uzito wake inakadiliwa kuwa kati ya kilo 3 hadi 4 na urefu wa nchi 19.1. Dalili za uchungu zinaweza kuanza wakati wowote ndani ya wiki 2 hadi 3 kuanzia sasa.

Matumbo ya mtoto wakati huu huwa yametengeneza kinyesi kinachonata na rangi ya kijani iliyokolea kiasi cha kuonekana kama cheusi ambapo atajisaidia wakati wa kuzaliwa.

Vinyweleo vichache vya awali pia vinakuwa vinefunika mwili wake vikifahamika kwa jina la lanugo.

Je mtoto anakuwa amekamilika?

Mifumo yote ya mtoto inakuwa imekamilika na ukuaji wa hatua hatua ya mwisho wa mapafu, mfumo wa fahamu na ubongo hutokea.

Je, ni salama kujifungua wiki ya 37?

Katika kipindi hiki, unakuwa umebakisha wiki 2 hadi 3 kabla ya kujifungua. Ingawa mtoto anakuwa amekamilika, inashauriwa kusubiri mpaka uchungu asili uanze kwa kuwa ni salama na umepangiliwa kutokea kwa wakati sahihi na huwa salama ukilinganisha na uchungu wa kuanzishwa.

Endapo uchungu utaanza wenyewe katika wiki hii ni salama na mtoto atazaliwa na ataweza kuishi bila kuhitaji uangalizi maalumu. Usiharakishe kujianzishia uchungu mwenyewe au na mtaalamu wa afya isipokuwa endapo kuna sababu ya msingi. Wakati huu ni vema kuepuka pia vyakula, dawa au kitu chochote lkinachoweza kuamsha uchungu.

Dalili za uchungu wiki ya 37

Si kawaida kupata uchungu katika wiki ya 37, endapo itatokea mtoto akizaliwa anaweza kuwa na afya njema hata hivyo atakuwa kwenye uangalizi maalumu kwa siku za awali. Dalili zifuatazo zinaweza kutokea;

Kujongea kwa misuli ya tumbo la chini

Kwenye wiki hii ya 37 unaweza kuhisi dalili hii kama ishara ya awali za uchungu, dalili hii humaanisha uchungu wa uongo kwa mijongeo ya misuli huwa haina mpangilio maalumu na haitokei mara kwa mara kama uchungu wa kweli.

Kuzibuka kwa kifuniko cha shingo ya kizazi

Kutokwa na makamasi mengi ukeni yanayoweza kuwa ya rangi ya maji, pinki, au kuwa na michirizi yad amu. Dalili hii ni kiashiria cha kutoka kwa kifuniko cha shingo ya kizazi ambacho huzuia vimelea kutoka ukeni kuingia kwenye kizazi.

Makamasi yanaweza kutoka kwa dakika chache, masaa au siku kadhaa kabla ya uchungu kuanza. Dalili hii huwa haigunduliwi na wanawake wengi.

Maumivu ya mgongo

Maumivu mara nyingi huwa ya mgongo wa chini yaani katika maeneo ya kiuno, ambayo huwa endelevu na huwa makali ya kutovumilika kwenye hatua za mwisho za uchungu. Maumivu haya yanahusishwa kusababishwa na mgandamizo kwenye via na mishipa ya fahamu ya mfuko wa matumbo(peritoniamu) kutokana na unaoletwa na kukua kwa kizazi.

Hisia za kujisaidia

Ni ishara ya mgandamizo kwenye matumbo na kibofu cha mkojo hivyo kupelekea hisia za kutaka kujisaidia. Hi pia humaanisha mtoto anajongea uelekeo wa kutoka nje ya kizazi kwa jina jingine mtoto kushuka. Mara nyingi hizia hizi huletwa na mgandamizo wa kichwa cha mtoto kwenye maeneo tajwa.

Kupasuka kwa chupa ya uzazi

Kati ya wanawake 10, mjamzito mmoja hupata dalili hii ambayo hutokea sana nyumbani wakati umelala. Baadhi ya nyakati chupa ya uzazi hupasuka kwenye uchungu na wakati mwingine hupasuliwa kwneye hatua ya pili ya uchungu.

Baadhi ya nyakahu huwa ni vigumu kutofautisha kati ya mkojo na maji ya chupa ya uzazi. Hata hivyo kupasuka kwa chupa ya uzazi huambatana na maji mengi yanayochuruzika kwenye mapaja kama mtu amesimama na huwa meupe, hayana harufu na hutoka mengi kwa ghafla au kuendelea kumwagika taratibu.

Kama ukipata dalili hii hakikisha kuwa si mkojo kwa kunusa, na kama ikionekana si mkojo unapaswa kuzingatia utoshiriki ngono au kutumia pedi ya kuchomeka ukeni au kufanya chochote kinachoweza kuingiza bakteria ukeni. Wakati huu onana na mtoa huduma ya afya.

Maji yakiwa na rangi tofauti na maji au harufu huweza kuashiria, maambukizi, au kuchanganyika  na choo cha mtoto.

Mabadiliko ya urefu na upana wa shingo ya kizazi

Shingo ya kizazi huwa fupi na nyembamba. Hii ni ishara kwamba sehemu ya chini ya kizazi inajiandaa kwa ajili ya kutoa mtoto kwa kuwa shingo kuwa nyembamba hufanya iweze kutanuka kirahisi Zaidi. Dalili hii hupimwa na mtaalamu wa afya kwa kutia vidole viwili ukeni ili kuifikia shingo ya kizazi.

Ongezeko kipenyo cha shingo ya kizazi

Kuongezeka kwa kipenyo cha shingo ya kizazi ni dalili inayoashiria kufunguka kwa njia ya uzazi ili kichwa cha mtoto. Kizio cha kipimo hiki ni sentimita na kipenyo cha mwisho cha kutanuka ni sentimita 10. Dalili hii huwezi kuifahamu mwenyewe, mtaalamu wa afya hupima shingo ya kizazi kupitia uke kutumia vidole viwili kila baada ya masaa 2 hadi 4 ikitegemea hatua ya uchungu uliyonayo. Hatua za awali za uchungu huweza kuchukua muda kabla ya kwenda kuwa uchungu wa kujifungua

Je, ni salama kujifungua wiki ya 37

Katika kipindi hiki, unakuwa umebakisha wiki 1 hadi 3 kabla ya kujifungua. Ingawa mtoto anakuwa amekamilika uumbaji wa viungo na mifumo mingi, wakati huu mtoto huhitaji kuongezeka uzito zaidi na kuimarika kwa mfumo wa upumuaji na fahamu.

Endapo uchungu utataka kutokea, daktari anaweza kuuruhusu uendelee. Baada ya kujifungua unaweza kuwekwa chini ya uangalizi maalumu kwa masaa kadhaa kabla ya kuruhusiwa kwenye nyumbani na mwanao.

Wakati huu kama uchungu haujaanza ni vema kuepuka pia vyakula, dawa au kitu chochote kinachoweza kuamsha uchungu

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD, Dkt. Salome A, M.D

Rejea za dawa:

– Pregnancy week by week. Week 37 https://www.thebump.com/pregnancy-week-by-week/37-weeks-pregnant. Imechukuliwa 20.07.2023

– Hutchison J, et al. Stages of Labor. 2023 Jan 30. In: StatPearls [Internet]. Treasure Island (FL): StatPearls Publishing; 2023 Jan–. PMID: 31335010.

– Melzack R, et al. Low-back pain during labor. Am J Obstet Gynecol. 1987 Apr;156(4):901-5. doi: 10.1016/0002-9378(87)90349-8. PMID: 2953242.

– Signs and Symptoms of Labor. https://americanpregnancy.org/healthy-pregnancy/labor-and-birth/signs-of-labor/. Imechukuliwa 18.07.2023

– William’s Obstetrics Twenty-Second Ed. Cunningham, F. Gary, et al, Ch. 17.

– NHS. Pregnancy signs. https://www.nhs.uk/pregnancy/labour-and-birth/signs-of-labour/signs-that-labour-has-begun/. Imechukuliwa 18.07.2023

– Cleveland clinic. 8 Signs That Labor Is 24 to 48 Hours Away. https://www.google.com/search?q=labor+symptoms&client. Imechukuliwa 18.07.2023

– NCBI. Stages of labor. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK544290/#:. Imechukuliwa 18.07.2023

MASWALI&MAJIBU kuhusu afya| Link...👇

https://afyaclass.com/afyaforums

Karibu AfyaUpdates Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In https://afyaclass.com  Also Follow us on Instagram @afyaclass

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa2 weeks ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa3 weeks ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa1 month ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa1 month ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa3 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake3 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa6 days ago

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu Haya ni maneno ambayo umekuwa ukiyasikia sana linapokuja swala la vipimo cha UKIMWI, je...

Magonjwa6 days ago

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia. Kutana na Ilene Raymond Rush ambaye aligunduliwa Kisukari aina ya Pili(Type 2...

Magonjwa1 week ago

Ugonjwa unaosababishwa na konokono

Ugonjwa unaosababishwa na konokono Ugonjwa unaosababishwa na konokono unaitwa schistosomiasis, au bilharzia. Ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na minyoo wanaoitwa...

Magonjwa1 week ago

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake. Wengi tumesikia kuhusu Red Eyes(Macho mekundu) Lakini je umewahi kusikia kuhusu Pink Eyes,?...

Magonjwa2 weeks ago

Omeprazole inatibu ugonjwa gani,Fahamu hapa

Omeprazole inatibu ugonjwa gani Omeprazole inatibu ni nini?, Hili ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara kwa mara na wafwatiliaji wengi...

Magonjwa2 weeks ago

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani Mate kujaa Mdomoni,ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watu, na zipo...

Magonjwa2 weeks ago

Glaucoma: Ugonjwa hatari unaopoteza nuru ya macho

Glaucoma: Ugonjwa hatari unaopoteza nuru ya macho Kuna magonjwa mengi yanayohusiana na macho, mengi yanatibika lakini kuna baadhi ya magonjwa...

Magonjwa3 weeks ago

Kunguni husababisha ugonjwa gani

Kunguni husababisha ugonjwa gani Kunguni ni wadudu wadogo ambao chakula chao kikubwa ni damu, wadudu hawa huweza kunyonya damu kutoka...

Magonjwa4 weeks ago

je ugonjwa wa pumu unaambukiza

je ugonjwa wa pumu unaambukiza? Hili ni Swali ambalo watu wengi huuliza,hata kwenye page za afyaclass, kwa kuliona hilo, tumeona...

Magonjwa1 month ago

Dalili za mwanzo za ugonjwa wa ini

Dalili za mwanzo za ugonjwa wa ini Ugonjwa wa ini (hepatic disease) mara nyingi huanza taratibu na dalili zisizo wazi,...