Connect with us

afya news

kuleta mabadiliko vita dhidi ya Malaria Kusini mwa Jangwa la Sahara

Avatar photo

Published

on

kuleta mabadiliko vita dhidi ya Malaria Kusini mwa Jangwa la Sahara

Rais Mstaafu, Dk Jakaya Kikwete akizungumza katika mkutano wa tatu wa Baraza la Kumaliza Malaria. Dk Kikwete alikuwa Mjumbe wa Baraza la Kimataifa la Kutokomeza Malaria jijini Dar es Salaam mara mbili.

Tunapoadhimisha Siku ya Malaria Duniani, sekta ya afya duniani inashuhudia maendeleo makubwa katika vita dhidi ya ugonjwa huo, hasa katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara eneo ambalo linabeba mzigo mkubwa zaidi wa ugonjwa huu hatari.

Kiini cha maendeleo haya ni kugunduliwa kwa chanjo ya R21/Matrix-M™, iliyotengenezwa kwa juhudi za ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Oxford na Taasisi ya Serum ya India, ikiwa ni uboreshaji kutoka kampuni ya Novavax’s Matrix-M™.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Afya Ifakara, Dk Honorati Masanja.

Chanjo hii ni zana yenye nguvu, inayoongeza kwa kiasi kikubwa mwitikio wa kinga mwilini na kuonyesha ufanisi mkubwa, katika maeneo yanayokabiliwa na maambukizi makali ya malaria.

Ubunifu kupitia ushirikiano

Uundaji wa chanjo ya R21/Matrix-M™ unawakilisha kilele cha ushirikiano wa kimataifa na mafanikio ya kisayansi. Ushirikiano huo ulichanganya utaalamu wa kina wa Chuo Kikuu cha Oxford katika utafiti wa chanjo na Taasisi ya Serum, inayoongoza kwa uzalishaji wa chanjo India. Novavax ilichangia teknolojia yake ya ubunifu ya adjuvant ambayo ni muhimu katika kuimarisha mwitikio wa kinga.

Dk Ally Olotu, Mtafiti wa Chanjo ya Malaria na kiongozi wa watafiti wa Taasisi ya Afya Ifakara (IHI), akifafanua jambo huku Profesa Adrian Hill wa Oxfords (kushoto) akisikiliza kwa makini.

Muungano huu umetoa chanjo ambayo sio tu kwamba inakidhi viwango vya ufanisi na usalama, lakini pia inatoa ahadi ya kupatikana kwa bei nafuu katika maeneo yenye uhitaji mkubwa.

Ufanisi na matokeo

Dk Ally Olotu, Mchunguzi Mkuu na Mkurugenzi wa Sayansi kati­ka Taasisi ya Afya Ifakara (IHI), akizungumzia matokeo ya chanjo hiyo amesema;

“Kufikia kiwango cha ufanisi cha asilimia 77 katika majaribio ya awamu ya pili, chanjo ya R21/Matrix-M™ imeonyesha uboresh­aji mkubwa katika chanjo ya awali ya RTS,S/AS01 ambayo ilionyesha ufanisi wa takriban asilimia 56 hapo awali, hii inatoa matumaini mapya na ulinzi kwa makundi yaliyo hatarini zaidi katika nchi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.”

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeidhinisha chanjo ya R21/Matrix-M™ kwa ajili ya kuzuia Malaria kwa watoto wanaoishi katika maeneo yenye maambukizi makubwa.

Chanjo ya Malaria ikiwa tayari kwa matumizi

Uamuzi huu ulifuatia matokeo ya majaribio yaliyoonye­sha ufanisi wa asilimia 75 kati­ka maeneo yenye maambukizi makubwa na asilimia 68 katika mikoa yenye uwepo wa malaria kwa muda mrefu. Wasifu wa usala­ma wa chanjo wenye athari ndogo, unasisitiza uwezekano wake wa kutumika kwa kiwango kikubwa.

Maoni ya wataalamu wa afya

Huku dunia ikisherehekea maendeleo ya karibuni katika vita dhidi ya Malaria, sauti za watu muhimu katika mapambano dhi­di ya ugonjwa huu hatari, zina­toa matumaini juu ya matokeo ya ugunduzi huu. Dk Matshidiso Moe­ti, Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, alielezea faida kubwa za chanjo ya R21/Matrix-M™, akise­ma, “Kuidhinishwa kwa chanjo ya R21/Matrix-M™ kunaweza kupun­guza kwa kiasi kikubwa pengo kati ya mahitaji na usambazaji, kui­marisha mikakati yetu ya kuzuia malaria na uwezekano wa kuokoa mamia na maelfu ya maisha ya vijana barani Afrika.”

Akitoa maoni yake wakati wa mahojiano maalumu, Dk Olotu alieleza juu ya uidhinishaji wa chanjo uliofanywa na WHO. “Uid­hinishaji wa WHO ni hatua muhimu katika afya ya umma. Uwezo wa chanjo hii kupunguza kasi ya viwango vya Malaria unaweza kubadilisha hali ya kuzuia malaria, sio tu Tanzania, bali kimataifa.” Mapendekezo haya yanasisitiza uwezo wa chanjo ya R21 kubadili­sha mbinu ya kuzuia malaria na kutoa mwanga wa matumaini kwa maeneo yaliyoathirika zaidi na ugonjwa huo.

Aidha, Machi 26, 2024, Taasisi ya Afya Ifakara ilishiriki katika kikao cha tatu cha Baraza la End Malaria jijini Dar es Salaam, amba­po Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alitoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kukabiliana na Malaria nchini. Kikwete alisifu nafasi ya Taasisi ya Ifakara katika uten­genezaji wa chanjo na kusisitiza umuhimu mkubwa wa chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano ambao wako katika hatari zaidi.

Chanjo ya R21, imeonyesha ufanisi wa kutegemewa katika majaribio ya kliniki, ikiimarisha zaidi mapambano dhidi ya Malaria kwa kuongeza zana zaidi katika orodha ya afua zilipo ikiwemo vyandarua.

Kuongeza kiwango cha usamba­zaji ulimwenguni

Taasisi ya Serum ya India ime­jitolea kuzalisha hadi dozi milioni 200 kila mwaka, kuhakikisha upa­tikanaji wa chanjo hiyo ili kuki­dhi mahitaji ya kimataifa. Kiwango hiki cha uzalishaji ni muhimu kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya dharura ya maeneo yenye malaria. GAVI, ina jukumu muhimu katika juhudi hii kwa kuwezesha ufad­hili na usambazaji wa chanjo katika nchi za kipato cha chini na kuhakikisha upatikanaji sawa. Dk Olotu anasisitiza uharaka wa utoaji wa chanjo hiyo kwa kusema kuwa “Tuna matumaini kwamba mchakato huu utahitimishwa haraka ili kutoa ufikiaji wa chanjo hii ya kuokoa maisha kwa watoto ambao wako katika hatari zaidi.”

Taasisi ya Afya Ifakara iko mstari wa mbele

Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) ime­kuwa sehemu muhimu katika tath­mini ya kitabibu ya chanjo ya R21/Matrix-M™. Ushiriki wa taasisi hiyo ni muhimu katika utekelez­aji na uendeshaji wa majaribio, ambayo yanazingatia viwango vya kitabibu vya kimataifa huku yakiz­ingatia maudhui ya ndani.

Dk Olotu aliongoza timu ya wata­alamu kupitia majaribio ya awamu ya tatu ya chanjo hiyo, akishiriki­ana na taasisi kama vile Imperial College London na washirika wen­gine katika mabara kadhaa. Ush­irikiano huu umekuwa muhimu katika kutathmini utendaji kazi wa chanjo katika mazingira tofauti ya magonjwa na kutoa maarifa muhimu ambayo yanagusa mika­kati ya afya ya kimataifa.

Majaribio ya kitabibu na matokeo yake kwa jamii ya Kitanzania

Majaribio ya kitabibu yaliyo­fanywa katika vijiji vya Kiwangwa na Miono katika Mkoa wa Pwani na Taasisi ya Afya Ifakara, yame­kuwa muhimu. Maeneo haya yali­yochaguliwa kwa viwango vyao vya maambukizi ya Malaria, yame­toa taswira ya ufanisi wa chanjo katika mazingira tofauti. Zaidi ya watoto 600 wenye umri wa miezi 6-36 walishiriki, ikionyesha idadi ya watu walio katika hatari zaidi.

Dk Honorati Masanja, Mkuru­genzi Mkuu wa IHI anabainisha kuwa, “Hili ni tukio la kihistoria kwa Ifakara, Tanzania na jamii ya kimataifa. Jukumu la taasisi yetu katika majaribio haya linasisitiza dhamira yetu ya kupambana na malaria kupitia utafiti na uvum­buzi wa msingi.”

Safari ya kutokomeza Malaria

Kutolewa kwa mafanikio kwa chanjo ya R21 kunaashiria waka­ti wa mabadiliko katika afya ya umma Tanzania na nchi kama Gha­na ambapo Malaria inasalia kuwa changamoto kubwa ya kiafya. Muingiliano wa chanjo hii katika programu zilizopo za kudhibiti Malaria kunaweza kongeza juhu­di za kuboresha afya ya umma, uwezekano wa kuzuia mamilioni ya visa vya Malaria na kupunguza mzigo mkubwa ambao ugonjwa huu unaweka kwa jamii.

Msimamo wa Ghana wa kuwa nchi ya kwanza kuidhinisha chanjo ya R21 unatoa funzo kwa mataifa mengine. Maendeleo haya muhimu yanaangazia umuhimu wa mamlaka za afya za kitaifa katika kupitisha suluhu bunifu za kupambana na kutokomeza ugon­jwa huu hatari.

Njia ya kusonga mbele inahusi­sha sio tu kuendelea kwa usam­bazaji wa chanjo lakini pia uju­muishaji wa zana hizi mpya katika mikakati mipana ya kudhibiti Malaria. Kwa kushughulikia chan­gamoto za kiufundi, kuimarisha imani ya jamii na kuhakikisha uta­fiti na ufuatiliaji endelevu, jamii ya afya duniani inaweza kupiga hat­ua kubwa kuelekea kutokomeza mojawapo ya magonjwa hatari zaidi duniani.

Kuhusu Taasisi ya Afya Ifakara (IHI)

Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) au kwa kifupi Ifakara, ni shirika linaloongoza la utafiti wa afya barani Afrika lenye rekodi nzuri ya kuendeleza, kupima na kuthibi­tisha ubunifu wa afya.

Taasisi hii inaendeshwa na maeneo ya kimkakati ya utafiti, mafunzo na hudu­ma. Ifakara inajumuisha taaluma mbalimbali za kisayansi, kuanzia sayansi ya msingi ya matibabu na ikolojia hadi majaribio ya kima­tibabu, utafiti wa mifumo ya afya, tafsiri ya sera na utekelezaji wa programu za afya.

Mwelekeo wa kimkakati wa Ifak­ara

Ifakara inatazamia kuwa na watu wenye afya njema na walio­wezeshwa kupata huduma za afya na masuluhisho yanayothibitika. Taasisi hii inajidhatiti kufikia dira ya kuwa kituo cha umahiri katika utoaji wa huduma bora za afya kwa ushirikiano kupitia utafiti, uvumbuzi, uimarishaji wa uwezo na utekelezaji wa programu.

Kazi za Ifakara katika mkakati wake wa miaka mitano (2023-2028) zinalenga katika kutoa masuluhisho ya msingi kwa ajili ya kushughulikia mahitaji na chan­gamoto za jamii, tafsiri ya sera na maarifa ili kuziba pengo kati ya utafiti na sera, uwezeshaji wa jamii ili kuwezesha ushirikiano, kufanya maamuzi ya pamoja na kuwekeza kwa kiasi kikubwa kati­ka maendeleo ya taasisi ili kuinua ubora katika utafiti na utekelezaji wa programu kwa madhumuni ya kubadilisha maisha ya watu.

Zaidi ya miaka 60 ya kuboresha afya ya jamii

Ziara ya Ifakara ya mtaalamu wa wanyama wa Uswizi Prof. Rudolf Geigy mwaka wa 1949 iliashiria mwanzo wa historia ya zaidi ya miaka 60 ya Ifakara. Geigy [1920-1995] alitafuta eneo kwa ajili ya kutafiti magonjwa ya kitropiki. Miaka minane baadaye, alifungua Maabara ya Taasisi ya Tropiki ya Uswizi (STIFL).

Jina “Ifakara” linamaanisha “mahali unapoenda kufa”, kiele­lezo cha mzigo mkubwa wa kihis­toria wa magonjwa katika eneo hilo kabla ya juhudi kubwa za kudhibiti kuanza. Katika miaka ya baada ya uhuru, STIFL ilitekeleza jukumu la kutoa mafunzo kwa maafisa wa matibabu ambao wangeweza kutumikia nchi baada ya Uhuru. Serikali ya Tanzania iliiagiza STI­FL kutekeleza jukumu hilo.

Mwaka 1996, Ifakara ilibadilish­wa jina na kuitwa ‘Ifakara Health Research and Development Center (IHRDC). Jina hili lilidumu hadi mwaka 2008 ambapo lilibadilish­wa tena na kuwa Taasisi ya Afya ya Ifakara. Uongozi imara wa waku­rugenzi wa sayansi wa Tanzania tangu 1993, kama vile Dk. Andrew Kitua na warithi wake, uliifanya IHI kusifiwa kimataifa.

Upanuzi uliendelea kwa kufun­guliwa kwa tawi jipya la Bagam­oyo mwaka 2005 na maendeleo makubwa ya miundombinu yaliyo­fanyika mwaka 2012 kwa kuanzish­wa kwa Kituo cha Mafunzo na Kituo cha Majaribio ya Kliniki. Dk. Honorati Masanja, Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa sasa, aliteuliwa mwaka 2016.

Karibu AfyaUpdates Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In https://afyaclass.com  Also Follow us on Instagram @afyaclass

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa4 weeks ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa1 month ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa2 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa2 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa3 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake4 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa1 day ago

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 days ago

Ugonjwa unaosababishwa na kula nyama mbichi

Ugonjwa unaosababishwa na kula nyama mbichi Madhara ya kula nyama ya ng’ombe mbichi Ni desturi ya baadhi ya watu kula...

Magonjwa1 week ago

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani Mkojo kuuma au kupata maumivu wakati wa kukojoa ni hali ambayo kwa kitaalam...

Magonjwa1 week ago

Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono dalili Zake

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa2 weeks ago

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu Haya ni maneno ambayo umekuwa ukiyasikia sana linapokuja swala la vipimo cha UKIMWI, je...

Magonjwa3 weeks ago

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia. Kutana na Ilene Raymond Rush ambaye aligunduliwa Kisukari aina ya Pili(Type 2...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa unaosababishwa na konokono

Ugonjwa unaosababishwa na konokono Ugonjwa unaosababishwa na konokono unaitwa schistosomiasis, au bilharzia. Ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na minyoo wanaoitwa...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake. Wengi tumesikia kuhusu Red Eyes(Macho mekundu) Lakini je umewahi kusikia kuhusu Pink Eyes,?...

Magonjwa3 weeks ago

Omeprazole inatibu ugonjwa gani,Fahamu hapa

Omeprazole inatibu ugonjwa gani Omeprazole inatibu ni nini?, Hili ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara kwa mara na wafwatiliaji wengi...

Magonjwa4 weeks ago

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani Mate kujaa Mdomoni,ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watu, na zipo...