Connect with us

Magonjwa

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Avatar photo

Published

on

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo cha tatizo la maumivu makali ya njia ya haja kubwa ni Bawasiri,ila sio kila mtu mwenye maumivu makali sehemu ya njia ya haja kubwa basi ana Bawasiri.

Baada ya kuliona hilo na kukutana na maswali mengi juu ya tatizo hili la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la bawasiri,nmeona nitoe maelekezo kwa kina kuhusu baadhi ya sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kupatwa na tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa ambayo huweza kutokea wakati anajisaidia au hata akiwa amekaa tu.

Sababu au Chanzo cha Maumivu makali sehemu ya Haja Kubwa

BAADHI YA SABABU ZA TATIZO LA MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA NI PAMOJA NA;

1. Tatizo la Bawasiri,kutoka kinyama sehemu ya haja kubwa,kuvimba kwa mishipa ya vein kwenye njia ya haja kubwa, hapa kuna bawasiri ya ndani pamoja na bawasiri ya nje,zote hizi huweza kusababisha maumivu makali ya sehemu ya haja kubwa

2. Mtu Kuwa na tatizo la jipu au majipu ambayo yametokea kwenye njia ya haja kubwa

3. Uwepo wa tatizo la Saratani au Kansa ya sehemu ya haja kubwa kama vile;Anal cancer,Rectum cancer n.k

4. Mtu kupatwa na tatizo la Fistula ambalo hujulikana kama Anal fistula

5. Mtu kupatwa na majeraha yoyote au michubuko kwenye sehemu ya haja kubwa,kutokana na sababu mbali mbali kama vile; kufanya mapenzi kinyume na maumbile yaani Anal sex, kuumia kwenye ajali n.k

6. Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Bacteria,Fangasi, Virusi,Minyoo n.k

7. Maambukizi ya baadhi ya magonjwa ya zinaa yaani sexual transmitted infections(STD’s)

8. Magonjwa kama Crohn’s, ambapo huu ni ugonjwa ambao huhusisha mtu kuvimba utumbo au kuwa na vidonda ambavyo huweza kuwepo kwenye utumbo lakini pia kwenye Rectum hata kupelekea mtu kuharisha au kujisaidia kinyesi kilichochanganyika na Damu

9. Tatizo la Levator Ani syndrome, ambapo misuli ya sehemu ya haja kubwa huwa dhaifu,kukakamaa,ukavu kupita kawaida,hali ambayo huleta maumivu ya njia ya haja kubwa hasa wakati wa kujisaidia

10. Tatizo la Pelvic Floor Dysfunction,ambapo misuli kwenye eneo lote la nyonga ikiwa ni pamoja na sehemu ya haja kubwa kushindwa kutanuka vizuri

11. Magonjwa mbali mbali ya ngozi kama vile; Psoriasis, maambukizi ya fangasi kwenye njia ya haja kubwa n.k

12. Tatizo la mtu kujisaidia kinyesi kigumu au kwa kitaalam hujulikana kama Constipation

13. Lakini pia kwa wakati mwingine ugonjwa wa Masundosundo au kwa kitaalam Genital warts huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili

VIPIMO VYA TATIZO HILI

Mgonjwa huweza kuchukuliwa history ya tatizo lake lilivyoanza, Kufanyiwa ukaguzi kwa njia mbali mbali kama vile; kuingiza kidole sehemu ya haja kubwa, kutumia kipimo cha Endoscopy n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI LA MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Tiba ya tatizo hili huanza kulingana na sababu za tatizo lenyewe,hivo kama tulivyochambua sababu mbali mbali hapo juu,ndivo na tiba zake huwa mbali mbali, ila kwa ujumla mgonjwa huweza kupata tiba kama vile;

• Matumizi ya baadhi ya dawa za kuondoa kabsa maumivu

• Matumizi ya dawa za kulainisha choo yaani stool softers pamoja na dawa za kulainisha misuli ya sehemu ya haja kubwa

• Kula vyakula na matunda yenye nyuzi nyuzi yaani Fibers kama maembe,machungwa,mapapai,

maparachichi n.k

• Huduma ya upasuaji kwa mgonjwa N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Jinsi ya Kupunguza Au Kuzuia kabsa Maumivu sehemu ya Haja Kubwa

Kuna vitu vya kufanya na Kuzingatia(Do) na kuna vitu vingine hushauriwi kuvifanya kabsa(Don’t)

Zingatia mambo Haya(Do);

âś“ Hakikisha unakunywa maji mengi kila siku

âś“ Kula vyakula vyenye fibre au nyuzi nyuzi za kutosha, ikiwemo mboga za majani na matunda
NB: Maji pamoja na vyakula vya aina hii husaidia kulainisha choo chako na kuzuia tatizo la kupata choo kigumu(Constipation)

âś“ Fanya Mazoezi ya mwili mara kwa mara(exercise regularly)

âś“ Baada ya Kujisaidia haja kubwa,jisafishe na maji safi, au kama unatumia toilet paper, hakikisha inakuwa laini sio ngumu

âś“ Tumia dawa za kutuliza Maumivu ikiwemo paracetamol

âś“ Oga na maji ya moto ili kupunguza kuwasha na maumivu n.k

Usifanye kabsa Vitu hivi kama una tatizo hili(Don’t)

Ă— usijikune karibu na sehemu ya haja kubwa

Ă— Ukihisi haja kubwa jisaidie, epuka tabia ya kujibana kwa muda mrefu

Ă— Usitumie nguvu sana wakati wa kujisaidia haja kubwa

Ă— Usitumie sabuni zenye kemikali kali karibu na sehemu ya haja kubwa

Ă— Epuka kula vyakula vyenye viungo vingi au kutumia pombe pamoja na vinywaji vingine vyenye kiwango kikubwa cha caffeine

Ă— Usibebe au kunyanyua vitu vizito sana

Ă— Usitumie dawa jamii ya ibuprofen kama unavuja damu sehemu ya haja kubwa(anus).

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ushauri|Tiba|CheckIn 🩺🌡️ContactUs; +255758286584 or INBOX📩. For More Healthtips everyday Link In https://afyaclass.com Also Follow us on Instagram @afyaclass

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa3 weeks ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa4 weeks ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa1 month ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa2 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa3 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake4 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa4 days ago

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani Mkojo kuuma au kupata maumivu wakati wa kukojoa ni hali ambayo kwa kitaalam...

Magonjwa5 days ago

Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono dalili Zake

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa2 weeks ago

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu Haya ni maneno ambayo umekuwa ukiyasikia sana linapokuja swala la vipimo cha UKIMWI, je...

Magonjwa2 weeks ago

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia. Kutana na Ilene Raymond Rush ambaye aligunduliwa Kisukari aina ya Pili(Type 2...

Magonjwa2 weeks ago

Ugonjwa unaosababishwa na konokono

Ugonjwa unaosababishwa na konokono Ugonjwa unaosababishwa na konokono unaitwa schistosomiasis, au bilharzia. Ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na minyoo wanaoitwa...

Magonjwa2 weeks ago

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake. Wengi tumesikia kuhusu Red Eyes(Macho mekundu) Lakini je umewahi kusikia kuhusu Pink Eyes,?...

Magonjwa3 weeks ago

Omeprazole inatibu ugonjwa gani,Fahamu hapa

Omeprazole inatibu ugonjwa gani Omeprazole inatibu ni nini?, Hili ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara kwa mara na wafwatiliaji wengi...

Magonjwa3 weeks ago

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani Mate kujaa Mdomoni,ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watu, na zipo...

Magonjwa3 weeks ago

Glaucoma: Ugonjwa hatari unaopoteza nuru ya macho

Glaucoma: Ugonjwa hatari unaopoteza nuru ya macho Kuna magonjwa mengi yanayohusiana na macho, mengi yanatibika lakini kuna baadhi ya magonjwa...

Magonjwa4 weeks ago

Kunguni husababisha ugonjwa gani

Kunguni husababisha ugonjwa gani Kunguni ni wadudu wadogo ambao chakula chao kikubwa ni damu, wadudu hawa huweza kunyonya damu kutoka...