Kutoka damu wakati wa mimba changa
Ujauzito ukiwa mchanga,kutoa vidamu ambavyo tunasema “spotting” ni kawaida, na hali hii hutokea wakati kiumbe kinachokua tumboni(developing embryo) kinajishikiza kwenye kuta za tumbo la uzazi. Na mara nyingi hii hutokea kile kipindi ambacho ungetakiwa upate hedhi yako ya kawaida.
Implantation Bleeding: Hii ni damu inayotoka wakati yai lililorutubishwa linajipandikiza kwenye ukuta wa uterasi. Hii kawaida hutokea wiki ya 1-2 baada ya kutunga mimba na mara nyingi siyo tatizo.
Katika Makala hii tunazungumzia tatizo la kutoa damu wakati wa mimba changa kama dalili ya hatari kipindi cha ujauzito na sio hizo spotts ambazo ni kawaida sio tatizo.
Kutoka damu wakati wa mimba changa;
Kutoka damu wakati wa ujauzito, hasa katika trimester ya kwanza (mimba changa), inaweza kuwa na sababu mbalimbali na mara nyingi inahitaji uangalizi wa karibu wa kitaalam.
Chanzo cha Kutoka damu wakati wa mimba changa
Hapa kuna baadhi ya sababu zinazochangia kutokwa na damu katika trimester ya kwanza:
1. Tatizo la Miscarriage (Kuharibika kwa Mimba):
Kutoka damu kunaweza kuwa ishara ya kuharibika kwa mimba, hasa ikiambatana na maumivu ya tumbo. Hii ndiyo sababu kuu ya kutokwa na damu katika trimester ya kwanza.
2. Tatizo la Ectopic Pregnancy (Mimba kutunga nje ya kizazi):
Hii ni hali hatari ambapo mimba inakua nje ya uterasi, Na mara nyingi hutokea katika moja ya mirija ya fallopian. Hii Inahitaji matibabu ya haraka.
3. Molar Pregnancy (Mimba ya Mole):
Hii ni tatizo adimu ambapo ujauzito haufanyiki kwa njia ya kawaida, na badala yake, tishu isiyo ya kawaida inakua ndani ya uterasi. Hii pia inaweza kusababisha kutoka damu.
4. Sababu Zingine: Kutokwa na damu wakati mwingine kunaweza kusababishwa na maambukizi katika uke au mlango wa kizazi(cervix), au hali zingine kama polyps za cervix.n.k
– Mabadiliko kwenye mlango wa kizazi(Cervical changes)
Ujauzito unaweza kusababisha mabadiliko kwenye mlango wa kizazi(Cervix) na hii wakati mwingine huweza kusababisha kuvuja damu hasa baada ya tendo.
– Maambukizi ukeni(Vaginal infections)
Ukiwa mjamzito halafu ukapata maambukizi mengine ya magonjwa Ukeni,hii inaweza kuchangia pia tatizo la kutokwa na damu wakati wa ujauzito.
Sababu zingine za damu kutoka ukiwa mjamzito hasa baada ya mimba kukua
Sababu zingine za damu kutoka ukiwa mjamzito hasa baada ya mimba kukua ni pamoja na;
1. Kuwa na tatizo la Placental abruption
Hali hii ni ya hatari na huhusisha kondo la nyuma(placenta) kuachia lilipojishikiza kwenye kuta za mji wa mimba,
Na huweza kuambatana na maumivu ya tumbo pamoja na damu.
2. Tatizo la Low-lying placenta (placenta praevia)
Hali hii hutokea pale ambapo kondo la nyuma(placenta) limejishikiza ila ni kwenye sehemu ya chini ya tumbo la uzazi karibu kabsa na mlango au shingo ya kizazi.
Mwanamke mwenye tatizo hili huweza kuvuja damu nyingi wakati wa ujauzito.
3. Tatizo lingine ni tatizo la Vasa praevia
Hii ni hali ya nadra sana kutokea,ambapo mishipa ya damu ya mtoto hupita kwenye utando unaofunika seviksi.
Chupa ya uzazi inapopasuka, Mishipa hii inaweza kupasuka na kusababisha kutokwa na damu ukeni. Mtoto anaweza kupoteza kiasi cha damu kinachohatarisha maisha.
Ni muhimu sana kwa mwanamke yeyote mjamzito anayepitia tatizo la kutokwa na damu—hata kama ni kidogo—kupata ushauri wa kitaalam mara moja. Daktari anaweza kufanya uchunguzi, kama vile ultrasound, ili kutambua chanzo cha tatizo na kutoa maelekezo yanayofaa kwa matibabu au ufuatiliaji zaidi.
Kumbuka, ingawa kutokwa na damu wakati wa mimba changa inaweza kuwa ya kutisha, si kila wakati inaashiria tatizo kubwa. Hata hivyo, bora kuchukua tahadhari na kuwasiliana na mtaalamu wa afya kwa ushauri na uchunguzi zaidi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!