Ticker

6/recent/ticker-posts

Maneno ya mwisho ya Rais wa Zamani wa Chile, Sebastián Piñera kwenye ajali ya helikopta iliyomuua



Maneno ya mwisho ya Rais wa Zamani wa Chile, Sebastián Piñera kwenye ajali ya helikopta iliyomuua.

Rais wa zamani wa Chile, Sebastián Piñera aliokoa maisha ya abiria watatu, akiwemo dada yake, kwa kuwaamuru waruke kutoka kwenye helikopta yake kabla ya kufa katika ajali ya kutisha.

Karla Rubilar, waziri wa zamani wa maendeleo ya jamii na familia, aliiambia Canal 24 ya Chile kwamba Piñera aliwaambia walionusurika, ‘Nyinyi ruka kwanza kwa sababu nikiruka nanyi, helikopta itawaangukia.’

Ndege hiyo, ikiwa na rais huyo wa zamani, kisha ikaanguka katika ziwa katika manispaa ya kusini ya Lago Ranco siku ya Jumanne wakati wa mvua kubwa.

Piñera, mwenye umri wa miaka 74, ambaye alihudumu kuanzia 2010-2014 na 2018-2022, alikuwa likizoni na familia yake na alikuwa akisafiri na dadake Magdalena Piñera na marafiki wawili, Ignacio Guerrero na mwanawe Bautista Guerrero.

Awali watatu hao walikuwa na chakula cha mchana nyumbani kwa mwanafunzi mwenzake wa chuo kikuu, José Cox.

Mpiga mbizi wa idara ya zima moto aliupata mwili wa Rais Piñera ukiwa ndani ya helikopta, ambayo ilikuwa futi 91 chini ya uso wa maji.

Iliwachukua wapiga mbizi kama dakika 10 kuuchukua mwili huo na kuuweka kwenye mashua.

“Utaftaji haukua mgumu sana, kwa kuwa hali ya hewa, joto, maji, upepo, kina na uchunguzi, vilikwenda vyema kusaidia kupiga mbizi” mwendesha mashtaka wa eneo la Los Ríos Ricardo González alisema, kulingana na gazeti la La Tercera.

“Alikuwa mtu mashuhuri, mtu mkarimu sana na jasiri sana,” Magdalena Piñera aliuambia mtandao wa habari wa Chile Meganoticias Jumanne usiku.

Rubilar, ambaye aliwahi kuwa msemaji katika muhula wa pili wa rais huyo wa zamani, alisema maneno yake ya mwisho yalikuwa mfano wa kiongozi anayewatanguliza wengine mbele yake.

Alisema Rais Piñera alitaka kusaidia utawala wa Rais Gabriel Boric katika juhudi za uokoaji kufuatia moto wa nyika ulioua watu 131 na kuchoma nyumba 3,000 wiki iliyopita katika mkoa wa Valparaiso.



Post a Comment

0 Comments