SAYANA PRESS ni nini? Je,ni Njia mpya ya Uzazi wa mpango?

SAYANA PRESS ni nini? Je,ni Njia mpya ya Uzazi wa mpango?

SAYANA PRESS ni nini?

Hii ni njia mpya ya Uzazi wa mpango, njia hii huzuia kupata ujauzito kwa muda mrefu,

na kwa mujibu wa campuni ya utengenezaji Pfizer” wanasema;

Njia hii ya muda mrefu itatumika endapo wewe pamoja na Wataalam wa afya wameona inafaa zaidi kwako kutumia, hivo ni muhimu kupata Ushauri wa kutosha na Elimu kabla ya matumizi yake.

Na ikiwa una upango wa Kutumia SAYANA PRESS kwa muda wa Zaidi ya Miaka 2 wewe pamoja na Wataalam wa afya lazima mjadili Faida na Hasara zake kwa kina kabla ya kutumia.

SAYANA PRESS imetengenezwa na nini?

Ingredient kubwa ndani ya SAYANA PRESS ni Medroxyprogesterone acetate(MPA) ambapo inafanana na hormone asilia mwilini ya Progesterone ila sio sawa.

SAYANA PRESS inafanyaje Kazi?

SAYANA PRESS inafanya kazi kwa kuzuia mayai yasikomae na kutolewa kwenye Ovaries wakati wa Mzunguko wako wa Hedhi,

Hivo kama mayai hayatatolewa au hakuna Ovulation, basi ni dhahiri kwamba hakuna Ujauzito Pia, maana mbegu za kiume haziwezi kukutana na mayai.

Kwa mujibu wa nhs.uk wanasema;

SAYANA PRESS ni mfumo mpya wa Depo-Provera(njia ya Sindano), na inafanana kabsa na Depo-provera jinsi inafanya kazi pamoja na matokeo yake mwilini.

Haya ni maneno yao;

“Sayana Press is a new form of Depo-Provera and is available in some clinics.

It’s very similar to Depo-Provera in the way it works and the effects it can have on your body”.

Je,Kwa hapa Tanzania SAYANA PRESS imefika?

Haya ni maelezo ya Dkt.Mollel Bungeni;

Swali&Majibu; Sayana Press ni njia ya kuzuia kupata ujauzito kwa muda mrefu, hivyo matumizi ya kuzuia mimba kwa Sayana Press na P2 ni tofauti.

Dkt. Mollel amesema Sayana Press imesajiliwa na TMDA na inapatikana kwenye vituo binafsi vya kutolea huduma za afya kwa Wateja wanaohitaji.

Watu ambao hawaruhusiwi kutumia SAYANA PRESS

Huruhusiwi kabsa Kutumia SAYANA PRESS Kama;

  • Una Mzio au ALLERGY na Ingredient za Medroxyprogesterone acetate(MPA) au Ingredients nyingine zilizotajwa ndani ya SAYANA PRESS
  • Ikiwa unafikiri wewe ni Mjamzito
  • Kama una tatizo la Kuvuja damu Ukeni ambapo hujui chanzo chake ni nini
  • Kama una magonjwa ya Ini(LIVER DISEASES)
  • Ikiwa una Saratani ya matiti au Viungo vingine vya Uzazi(Sex organs)
  • Una tatizo la Blood clots ambapo ni matokeo ya tatizo la deep vein thrombosis n.k
  • Au kuwa na tatizo lolote linalohusu mzunguko wa damu
  • Kama una matatizo ya mifupa kama vile mifupa kudhoofika,kukosa nguvu,kuwa mywembamba n.k
  • Kama una ugonjwa wowote unaoathiri mishipa ya damu ndani ya Ubongo

Tahadhari dhidi ya Matumizi ya SAYANA PRESS

– Hakikisha umefanyiwa uchunguzi wa kutosha kabla ya kuanza kutumia SAYANA PRESS

-ZUNGUZA NA DAKTARI WAKO AU WATAALAM WA AFYA Ikiwa una hali kama hizi;

• Una tatizo la maumivu makali ya kichwa au kipandauso(migraine headache)

• Una ugonjwa wa kisukari au historia ya ugonjwa huu kwenye Familia yako

• Maumivu makali ya miguu, miguu kuvimba n.k

• Matatizo ya Mifupa

• Matatizo kwenye damu,ikiwemo damu kugandana, blood clots n.k

• Kuwa na magonjwa ya Moyo

• Kuwa na magonjwa ya Ini

• Una matatizo mbali mbali ya hedhi

• Una tatizo la kiharusi(stroke)

• Una ugonjwa wa Presha, pamoja na matatizo mbali mbali kwenye mzunguko wa damu

• Una ugonjwa wa Pumu,Asthma

• Una Saratani ya Matiti au Saratani Zingine

• Una ugonjwa wa Kifafa n.k

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!