TEMEKE: ruhusa ya Mume kuweza kumuona Mkewe wakati akijifungua

TEMEKE: ruhusa ya Mume kuweza kumuona Mkewe wakati akijifungua

Hospitali ya Rufaa Mkoa Temeke(TRRH) imeanza rasmi kutoa huduma ya kujifungua ukiwa na Msaidizi yaani Mama, Mwenza au Dada na kuruhusu Mama anayejifungua kuchagua Muuguzi anayemtaka kama muongozo mpya wa ‘chati uchungu’ unavyosema ambapo sasa Mume anaweza kuruhusiwa kumuona Mkewe wakati akijifungua.

Hassan Mwauta, ambaye ni Mume wa mmoja wa wajawazito waliotumia huduma hiyo katika Hospitali hiyo, amesema “Nimemleta Mke wangu kuja kujifungua na nilisikia kuna huduma ya Mzazi kujifungua akiwa na Mwenza wake nilipofika hapa nimejionea mwenyewe nimeshangaa kwakweli mazingira mazuri na huduma nzuri, unaweza kuingia na mjamzito wako ukakaa nae muda wowote unaotaka”

Kwa upande wake, Afisa Mkunga, Shukrani William kutoka hospitali hiyo ameeleza namna wodi ya kujifungulia kina mama ilivyoboreshwa na kusema kuwa maboresho hayo yamefanywa ili kumuwezesha mjamzito kupata huduma bora zaidi na kuwa karibu na Msaidizi wake pamoja na kuzingatia utu na heshima kwa mama mjamzito.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imesema inaendelea kufanya maboresho ya kimiundombinu ili kuweza kutoa huduma bora zaidi kwa Watanzania.

Via:MillardAyoUPDATES

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!