Ticker

6/recent/ticker-posts

Wahudumu wa afya ngazi ya jamii lazima watoke kwenye Jamii Zao



Wahudumu wa afya ngazi ya jamii lazima watoke kwenye Jamii Zao.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam tarehe 31 Januari 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea tuzo maalum ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Sekta ya Afya wakati wa uzinduzi wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es salaam tarehe 31 Januari 2024.

“Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ndio askari wa mbele katika Sekta ya Afya kwa kuwa ndio wanaibua magonjwa na wanaweza wakazuia na kutoa taarifa zozote kuhusu masuala ya magonjwa, lakini pia ni nguzo muhimu katika kuimarisha mifumo ya Afya ili kufikia lengo la huduma za Afya kwa wote.” Amesema Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu leo Januari 31, 2024 wakati wa Uzinduzi wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

“Uzinduzi wa mpango huu jumuishi ni hatua nzuri kufikia malengo ambayo tumejiwekea kama nchi na kama Dunia, sisi kama Bunge tunakwenda na kauli mbiu isemayo Afya ya jamii Nyumba kwa Nyumba Hatuachi Mtu.” Amesema Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi Mhe. Faustine Ndugulile leo Januari 31, 2024 wakati wa Uzinduzi wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya jamii.

“pango huu jumuishi ndio daraja kati ya huduma za Afya na jamii kwamalengo ya 95 95 95  yatahitaji kwenda na jamii. “Naipongeza Serikali kwa kuja na mpango jumuishi ambaoo amesema anaimani kabisa askari wa Afya ya Jamii na hawa wanajeshi (wahudumu wa Afya ngazi ya jamii) ndio watakao tufikisha katika malengo hayo.” Ameongeza

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akimpokea na kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kwenye Uzinduzi wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii utakaofanyika kwenye kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere leo Januari 31, 2024 Jijini Dar Es Salaam.

Dkt. Mpango amepokelewa  na Waziri @ummymwalimu akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam Bw. Albert Chalamila, Naibu Waziri anayeshulikia masuala ya Afya OR- Tamisemi Mhe. Festo Dugange, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Afya na maswala ya UKIMWI Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe.

Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii tunataka watoke kwenye jamii zao sio mtu unatoka Tanga unaenda kufanya kazi Buhigwe kama mhudumu wa afya ngazi ya jami,

wakati Buhigwe wana mila zao wana taratibu zao na desturi zao za kuhudumia mgonjwa na kusaidia jamii,

kwahiyo watachaguliwa na mikutano mikuu ya vijiji au watapeleka maombi kwenye vijiji au mitaa ndio vitawapitisha,

tunaamini hakutakuwa na vitendo vya rushwa wala upendeleo na tumewawekea malengo, watapitia angalau kaya 23 kwa wiki sawa na kaya 100 kwa mwezi pamoja na maeneo mengine yenye mkusanyiko kama masoko stendi za mabasi, nyumba za ibada na mikutano.

Wahudumu hawa watawajibika katika kituo cha kutoa huduma kilichopo katika eneo lake. Waziri @ummymwalimu

“Serikali ya Awamu ya Sita imetenga jumla ya shilingi bilioni 899.4  kwa ajili ya kutekeleza mpango wa  kuajiri na kuwajengea uwezo jumla ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wapatao 137,294 katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara , Utekelezaji wa Mpango huo utafanyika katika kipindi cha miaka mitano kwa awamu ambapo mwaka wa kwanza (2023/24) zaidi ya Wahudumu 28,000 watafikiwa na baadaye wastani wa Wahudumu 27,324 kila mwaka kwa kipindi cha miaka minne mfululizo kuanzia mwaka 2024/25 hadi 2027/28.”  Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango

WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII NI TEGEMEO KATIKA SEKTA YA AFYA

Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ndio Mstari wa mbele katika Sekta ya Afya wanaoweza kuibua wagonjwa na kutoa taarifa zote kuhusu masuala ya Magonjwa ikiwemo yasiyoambukiza na yakuambukiza kama ya milipuko.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Januari 31, 2024 wakati wa Uzinduzi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii iliyozinduliwa leo na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdori Mpango katika kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam.

”Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ndio askari wa mbele katika Sekta ya Afya na ndio wanaibua wagonjwa na wanaweza wakazuia na kutoa taarifa zote kuhusu masuala ya magonjwa na ni nguzo muhimu katika kuimarisha mifumo ya Afya ngazi ya jamii ili kufikia lengo la huduma za Afya kwa wote.” Amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri @ummymwalimu amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wanaenda kuwapunguzia mzigo watumishi walio katika ngazi za Hospitali kwa kuwa kuna baadhi ya vijiji havina vituo vya Afya au vinapatikana mbali na makazi ya watu.

“Ndio maana tumeona ni muhimu sasa turasimishe mpango huu ili kutomuacha mtu yoyote, Mfano kwa upande wa ugonjwa wa Kifua Kikuu tulipoamua kutumia wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wameibua wagonjwa wapya asilimia 50 kwa kila wagonjwa wapya 100 wanaogunduliwa na ugonjwa huo.”  Amesema Waziri Ummy



Post a Comment

0 Comments