Ticker

6/recent/ticker-posts

Watu milioni 41 hufariki kwa mwaka kutokana na magonjwa yasiyoambukiza



Watu milioni 41 hufariki kwa mwaka kutokana na magonjwa yasiyoambukiza.

Kila Mwaka watu Milioni 41 duniani hufariki kutokana na magonjwa yasiyoambukiza na vifo milioni 17 kati ya hivyo huwapata watu walio na umri wa chini ya miaka 70 huku sababu kubwa ya vifo hivyo ikiwa ni magonjwa ya moyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi wakati akiwasilisha mada katika Mkutano wa Mafunzo wa 108 wa watayayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma kupitia TBC, ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)

“Vifo milioni 17 huwapata watu waliochini ya miaka 70, kitaalamu tunaita pre-mature death (vifo vya kabla ya wakati) na idadi kubwa ya vifo hivi vinatokea katika nchi za uchumi wa chini na wa kati” amesema Prof. Janabi

Prof. Janabi ametoa rai kwa washiriki kuzingatia mtindo bora wa Maisha ikiwemo kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na sukari ili kujiepusha na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu na sukari.

Aidha ametoa wito kwa watu ambao tayari wameshajikuta wanachangamoto za shinikizo la juu la damu kuendelea kutumia dawa kama ambavyo wanashauriwa na wataalamu ili kujikinga ya magonjwa ya moyo pamoja na Figo.

@tbc_online @tbctaifa



Post a Comment

0 Comments