Ticker

6/recent/ticker-posts

Madaktari wapandikiza Figo ya Nguruwe kwa binadamu



Madaktari wapandikiza Figo ya Nguruwe kwa binadamu.

“Hii sio tu njia ya kunisaidia, lakini njia ya kutoa matumaini kwa maelfu ya watu wanaohitaji upandikizaji ili kuishi.”

Richard Slayman wa miaka 62 amefanikiwa kupata figo mpya kutoka kwa nguruwe ambayo ilibadilishwa vinasaba ili kupunguza hatari ya kiungo hicho kukataa kufanya kazi.

Madaktari wa upasuaji wa Marekani wanasema Rick Slayman ni “shujaa halisi” kwa kujaribu upasuaji huo.

Upasuaji huo wa saa nne, uliofanyika Machi 16 , “unaashiria hatua kubwa katika jitihada za kutoa viungo vinavyopatikana kwa urahisi zaidi kwa wagonjwa”, Hospitali ya Massachusetts ilisema katika taarifa.



Post a Comment

0 Comments