Ticker

6/recent/ticker-posts

Msongo wa mawazo chanzo cha magonjwa mengi



Msongo wa mawazo chanzo cha magonjwa mengi

Usichokijua ni kwamba; Msongo wa mawazo,mfadhaiko(Stress,depression) ni sababu kuu ya ulemavu duniani kote na ni mchangiaji mkuu wa ongezeko kubwa la magonjwa hasa yasioyakuambukiza.

Hali hizi huweza kutokea kwa mtu yeyote na zinaweza kudhibitiwa. Zipo njia za kukusaidia kama unapitia hali kama hizi;

Kwenye Ukurasa wa Shirika la Afya Duniani(WHO) wanasema;

“Depression is a leading cause of disability worldwide and is a major contributor to the overall global burden of disease.

Here’s what you should know about #depression:

✔️It can happen to anyone.
✔️It is an illness, not a sign of weakness.
✔️It can be treated”

Msongo wa mawazo, au stress, ni hali ya kihisia inayoweza kuathiri afya ya mtu kiafya na kiakili. Dalili za msongo wa mawazo zinaweza kutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine na zinaweza kujumuisha:

(1) Dalili za Kihisia na Kiakili:

 Hisia za kufadhaika au kukata tamaa – Kuhisi kuzidiwa na mambo yanayoendelea kwenye maisha yako.

Kukosa motisha au kufurahia mambo – Kupoteza hamu ya kufanya shughuli zilizokuwa zinakupa raha awali.

Hisia za wasiwasi au hofu – Kuwa na wasiwasi wa kupita kiasi kuhusu mambo ambayo yanaweza au hayawezi kutokea.

Shida za kumbukumbu au umakini – Kupata shida ya kukumbuka mambo, kuzingatia, au kufanya maamuzi.

Mood swings – Kubadilika kwa ghafla kwa hisia zako.

Kujitenga – Kujitenga na marafiki, familia, na shughuli za kijamii.

(2) Dalili za Kimwili:

Mabadiliko katika hamu ya kula – Kula kupita kiasi au kushindwa kula.

Shida za usingizi – Kupata shida kulala au kulala kupita kiasi.

Maumivu ya kichwa au mgongo – Kupata maumivu ya mara kwa mara yasiyo na sababu ya wazi.

Uchovu wa mara kwa mara – Kuhisi uchovu hata baada ya kupumzika au kulala.

Mabadiliko ya kimaumbile – Mabadiliko katika mzunguko wa hedhi au matatizo ya nguvu za kiume.

Matatizo ya tumbo – Kama vile kuhisi tumbo limejaa, kuharisha, au constipation.

(3) Dalili za Kijamii:

Kupunguza ufanisi kazini – Kupata shida kufanya kazi kwa ufanisi au kumaliza kazi.

Kukwepa majukumu – Kukwepa majukumu ya kikazi au kijamii.

Kutumia vibaya vileo na dawa – Kutumia pombe, dawa za kulevya, au dawa nyingine kama njia ya kukabiliana na stress.

Ni muhimu kutafuta usaidizi iwapo unahisi msongo wa mawazo unakuzuia kuishi maisha ya kawaida. Hii inaweza kujumuisha kuzungumza na mtaalamu wa afya ya akili, kama vile mshauri nasaha au mwanasaikolojia, au kuzungumza na daktari kuhusu chaguzi za matibabu.

Fahamu Msongo wa mawazo huweza kuleta madhara makubwa ikiwemo;

Njia za kupunguza msongo wa mawazo na kuboresha afya yako ya akili na mwili

Maisha ni safari ndefu yenye changamoto nyingi ambazo zinaweza kusababisha msongo wa mawazo, Msongo wa mawazo ni tatizo kubwa la kiafya ambalo linaweza kuathiri afya yako ya akili na mwili.

Njia za kupunguza msongo wa mawazo ni muhimu sana ili kuweza kuishi maisha yenye afya na furaha,Katika makala hii, tutajifunza njia za kupunguza msongo wa mawazo na kuboresha afya ya akili na mwili.

Stress huweza kuathiri vyote viwili,akili pamoja na mwili, Ingawa kuwa na kiwango kidogo sana cha Stress huweza pia kusaidia mtu kutimiza majukumu yake ya kila siku vizuri, ila ikiwa ni kwa kiwango kikubwa ni tatizo kubwa ambalo huweza kusababisha madhara makubwa kimwili na kiakili(Physical and mental health problems).

Njia za kupunguza msongo wa mawazo

Hapa chini ni baadhi ya njia za kupunguza msongo wa mawazo:

1. Fanya mazoezi mara kwa mara

Mazoezi ni muhimu sana katika kupunguza msongo wa mawazo, Unaweza kufanya mazoezi kama vile;

kutembea,

kukimbia,

kuogelea

kucheza mpira

kuruka kamba

au kucheza michezo ya viungo.

Mazoezi husaidia kuongeza kiwango cha endorphins, ambayo ni kemikali inayosababisha hisia za furaha na kupunguza msongo wa mawazo.

2. Pata usingizi wa kutosha

Kupata usingizi wa kutosha ni muhimu sana katika kupunguza msongo wa mawazo.

Jitahidi kupata masaa 7-8 ya kulala usingizi kila siku, Kama una tatizo la kukosa usingizi, jaribu kutumia mbinu kama vile kutengeneza mazingira ya utulivu kabla ya kulala au kufanya mazoezi ya kupumzisha mwili na akili kabla ya kulala.

3. Fanya mazoezi ya kupumzisha akili

Mazoezi ya kupumzisha akili kama vile;yoga pamoja na meditation ni njia nzuri ya kupunguza msongo wa mawazo. Mazoezi haya husaidia kuongeza utulivu wa akili na kusaidia kujenga nguvu ya kiroho.

4. Kula vizuri

Chakula ni muhimu sana katika kudumisha afya ya mwili na akili. Kula lishe yenye virutubisho vyote muhimu kama vile;

protini,

wanga,

mafuta n.k

bila kusahau Kula mboga mboga za majani pamoja na matunda,

Unaweza pia kula matunda yenye vitamini na madini muhimu kama vile vitamin C, E na magnesium ambavyo husaidia kupunguza msongo wa mawazo.

5. Jifunze kusimamia muda wako

Kusimamia muda wako ni muhimu sana katika kupunguza msongo wa mawazo. Hivo Jitahidi kusimamia vizuri muda wako na kufanya mambo yako ndani ya muda unaostahili,

Usifanye vitu nje ya muda au kwa kuchelewa,hii itaongeza zaidi tatizo la Msongo wa mawazo.

6. Punguza matumizi ya kafeini na pombe

Kafeini pamoja na pombe zinaweza kuongeza msongo wa mawazo na kusababisha matatizo ya kukosa usingizi au kutokulala.

Kama unatumia kafeini au pombe, jaribu kupunguza matumizi yako au kuepuka kabisa.

7. Panga mipango ya maisha yako

Kupanga mipango ya maisha yako kunaweza kukusaidia kupunguza msongo wa mawazo. Jitahidi kujua malengo yako na uweke mikakati ya kufikia malengo hayo. Hii itakusaidia kuwa na utulivu wa akili na kuepuka msongo wa mawazo.

8. Usipende kukaa Peke yako muda mwingi,badala yake Tumia muda wako pamoja na familia na marafiki

kutenge Muda wa kukaa na familia pamoja na marafiki ni muhimu sana katika kupunguza msongo wa mawazo,

Kupata muda wa kuongea na kushirikiana na watu wako wa karibu kunaweza kukusaidia kupata faraja na kujenga uhusiano mzuri na watu wengine.

9. Fanya vitu unavyovipenda zaidi

Kufanya Vitu unavyovipenda zaidi ni njia bora ya kukusaidia kupunguza Msongo wa mawazo,

Pata Muda wa kufanya vitu unavyovipenda zaidi.

Fanya vitu unavyovipenda zaidi ikiwemo vitu vya kupumzisha na kuburudisha akili kama vile;

Kuangalia Movie/filamu

Kusikiliza Muziki

Kupika

Kusoma vitabu vya hadithi n.k

10. Tafuta msaada wa kitaalamu

Kama msongo wako wa mawazo unazidi kuwa mkubwa na unakwamisha maisha yako, tafuta msaada wa kitaalamu. Kuna wataalamu wa afya ya akili ambao wanaweza kukusaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuboresha afya yako ya akili.

Hitimisho(Conclusion):

Msongo wa mawazo ni tatizo kubwa la kiafya ambalo linaweza kusababisha matatizo ya akili na mwili. Njia za kupunguza msongo wa mawazo ni muhimu sana ili kuishi maisha yenye afya na furaha,

Kwa kufuata njia hizi, utaweza kupunguza msongo wa mawazo na kuwa na afya bora ya akili na mwili.

Kumbuka, kupunguza msongo wa mawazo si jambo rahisi lakini inawezekana kabisa. Ni muhimu kuanza na hatua ndogo kwa kuzingatia mambo machache kila siku ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Epuka kusubiri mpaka hali yako iwe mbaya sana, badala yake anza mapema na Pia tafuta msaada wa kitaalamu kama utahitaji. Kwa kufanya hivyo, utaweza kuishi maisha yenye afya bora ya akili na mwili.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments