Ticker

6/recent/ticker-posts

Shule za Cross River zafungwa kufuatia mlipuko wa surua



Shule za Cross River zafungwa kufuatia mlipuko wa surua.

Shule mbili zinazopatikana katika eneo la serikali ya mtaa wa Akpabuyo katika jimbo la Cross River nchini Nigeria zimefungwa kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa surua.

Kamishna wa Afya katika Jimbo hilo, Dk. Henry Ayuk alisema shule hizo mbili ni Shule ya Sekondari ya Navy na Shule ya Msingi ya Penniel, zote ziko katika eneo moja.

Ayuk alisema Timu ya wataalam kutoka Wizara ya Afya tayari imeshapelekwa katika eneo lililoathiriwa.

Alisema;

“Utoaji wa Chanjo kwa watoto unaendelea katika maeneo yaliyoathirika na katika maeneo mengine ya serikali za mitaa ambapo hakuna kesi zilizoripotiwa.”

Kamishna huyo ambaye alibainisha kuwa Wakala wa Maendeleo ya Afya ya Msingi wa Jimbo anaongeza chanjo ya kawaida ili kujenga kinga zaidi(herd immunity),

alionya kuwa ugonjwa wa surua ni ugonjwa wa kuambukiza, haswa kwa watoto ambao hawajapata chanjo, wazazi na walezi wanahimizwa kuitikia vyema kampeni za kawaida za chanjo kwa watoto wao.”



Post a Comment

0 Comments