Magonjwa
Dalili za Ugonjwa wa Surua,chanzo na Tiba yake
Dalili za Ugonjwa wa Surua,chanzo na Tiba yake
UGONJWA WA SURUA(MEASLES),CHANZO,DALILI NA MATIBABU YAKE
Ugonjwa huu huhusisha Mfumo wa hewa na husababishwa na virusi aina ya Paramyxovirus na pia uenezwaji wa virusi hawa ni kwa njia ya mtu kupumua, kupiga chafya, kukohoa au wakati mwingine mtu akiongea.
Licha ya chanjo ambazo watoto hupewa kliniki lakini bado Ugonjwa huu wa Surua huendelea kusababisha Vifo kwa watoto wengi wenye umri wa chini ya Miaka 5.
DALILI ZA UGONJWA WA SURUA NI PAMOJA NA;
– Kuwa na mapele katika sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo Usoni
– Mgojwa kupatwa na hali ya kukohoa
– Mgonjwa Kupatwa na mafua mepesi
– Joto la mwili la Mgonjwa kupanda
– Mgonjwa kubadilika rangi ya macho na kuwa mekundu
MADHARA YA UGONJWA WA SURUA NI PAMOJA NA;
- Mgonjwa kupatwa na tatizo la masikio
- Kuathiriwa utoaji wa sauti kwa Mgonjwa kwani ugonjwa huu huhusisha mfumo mzima wa hewa
- Athari katika ubongo wa binadamu
- Kuchangia tatizo la Pneumonia au Homa ya mapafu
- Kuchangia kuwepo kwa matatizo ya moyo
- Huathiri utengenezaji wa seli za Damu
MATIBABU YA UGONJWA WA SURUA
Hakuna tiba au dawa ya moja kwa moja mpaka sasa kwa ajili ya kutibu surua, Japo mgonjwa atashauriwa kupata mda wa kutosha kupumzika,kupata hewa ya kutosha na kunywa maji kwa kiasi kikubwa.
Hivo basi matibabu ya surua yataangalia sana dalili za Mgonjwa na singinevyo.
-
Uzazi/Ujauzito5 days ago
Dalili za hatari baada ya kujifungua kwa upasuaji
-
Magonjwa4 days ago
Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu
-
Uzazi/Ujauzito3 days ago
Dalili za mimba hutokea baada ya siku ngapi
-
Magonjwa7 days ago
Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri
-
Magonjwa2 days ago
kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani
-
Events6 days ago
Chad yafanikiwa kuondoa Ugonjwa wa trypanosomiasis,WHO yatangaza
-
News4 days ago
TANZIA:Yusuf Manji afariki dunia akipatiwa Matibabu Marekani
-
Utafiti22 hours ago
Zaidi ya vifo milioni 3 kila mwaka hutokana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya-WHO