Nini kinasababisha hedhi kuchelewa
Endapo una aina ya mzunguko wa hedhi ambao haubadiliki badiliki yaani regular menstrual cycles, kuna wakati unaweza kukutana na vipindi vya hedhi kuchelewa kuliko kawaida,
Hii huweza kukupa wasi wasi nini kinaendelea mwilini, Moja ya Sababu ya haraka haraka ambayo unaweza kufikiria ni kuhusu kubeba Mimba.
Katika Makala ya Leo,tumechambua Sababu kuu zinazoweza kukusababishia Hedhi yako ichelewe.
Nini kinasababisha hedhi kuchelewa
Zipo Sababu nyingi ambazo huweza kuchangia tatizo hili, na Baadhi ya Sababu hizo ni pamoja na;
1. Kufanya Mazoezi kupita kiasi, Exercising Rigorously
Kila kitu kinataka kiasi, hata Mazoezi tunasema yana Faida nyingi mwilini lakini pia yanataka Kiasi,
Unaweza kuona shida ya kuchelewa kwa hedhi kutokana na kufanya mazoezi mazito. Mazoezi ya nguvu ya mara kwa mara yanaweza kusababisha vipindi visivyo kawaida vya hedhi ikiwemo kukosa hedhi. Unaweza pia kupata hedhi isiyo ya kawaida ikiwa utaanza kufanya mazoezi tena baada ya kutofanya kwa muda.
Mazoezi kupita kiasi husababisha physical stress mwilini mwako, Hali ambayo huuambia Ubongo Kuacha kuzalisha vichocheo yaani reproductive hormones.
Moja ya vichocheo hivo ni Pamoja na gonadotropin-releasing hormone (GnRH). Hormone hii ndyo inayohusika na Muda wa Hedhi yako kutoka,Ikiwa Ubongo haujaitoa au unaitoa Taratibu sana hedhi inaweza kuacha Kutoka.
2. Mabadiliko kwenye Uzito wa Mwili
Kichocheo cha Estrogen kwa asilimia kubwa huzalishwa kutoka kwenye tishu zinazotengeneza mafuta baada ya kipindi cha Ukomo wa Hedhi(menopause),tishu hizi hufahamika kama adipose tissue,
Ingawa,Mwanamke mwenye mafuta yaliyozidi,mwili wake huweza kuzalisha estrogen nyingi kipindi chochote cha Maisha yake sio tena baada ya kufikia ukomo wa hedhi. Hii ina maana kadri kiwango cha Mafuta kinapozidi mwilini ndivo kiwango cha estrogen huongezeka pia.
Matokeo yake,Estrogen ikizidi huathiri mzunguko wa hedhi na kuleta madhara kama vile;
- Kuvuja damu nyingi ya Hedhi
- Kukosa Hedhi
- Hedhi kuchelewa kutoka
- Au Hedhi kutokutoka kwa mpangilio
Hivo ukiwa na Uzito Mkubwa upo kwenye hatari hii,
FAHAMU,Kama Uzito wako wa mwili unapungua kupita kiasi kwa kasi sana upo kwenye hatari ya Kupata mabadiliko ya Hedhi Pia.
Estrojeni ni muhimu kwa ajili ya kujenga ukuta wa uterasi kwa mimba inayoweza kutokea wakati wa mzunguko wa hedhi. Unapopoteza uzito mwingi, mwili wako hautoi estrojeni ya kutosha.
3. Kuwa na Msongo wa Mawazo au Stress
Hali ya Stress inaweza kusababisha mabadiliko ya Hedhi ikiwemo hedhi kuchelewa kutoka,
Utafiti umeonyesha kuwa watu walio na viwango vya juu vya mfadhaiko,Msongo wa mawazo au Stress pia walikuwa wakipata vipindi visivyo kawaida vya HEDHI.
Wakati STRESS inaathiri muda wa hedhi, inaweza kuathiri uzazi Pia. Wale ambao wana Stress kwa kiwango kikubwa wanaweza kuwa na wakati mgumu zaidi wa kupata mimba au kuwa na ujauzito usio na matatizo.
4. Mabadiliko ya vichocheo au Hormones mwilini
Mfano kwenye tezi la thyroid—Homoni za tezi la Thyroid huwajibika kwa udhibiti wa nishati ya mwili wako na huathiri viungo vingi. Viwango vya homoni za tezi hili vinapokuwa juu au chini, utendaji wa mwili wako unaweza kubadilika—pamoja na utendajikazi wako wa mzunguko wa hedhi.
Kwa wale wanaozalisha kiwango kikubwa cha thyroid hormone— huweza kupata Hedhi karibu karibu , Na wale ambao hawazalishi thyroid hormone ya kutosha huweza kupata hedhi kwa kuchelewa au mara chache Zaidi
5. Kuwa kwenye Mazingira yenye Dawa za kuua wadudu,Exposure to Pesticides
Pesticides zinaweza kuwa na uhusiano wa karibu na mabadiliko ya Hedhi yaani irregular periods.
Washiriki wa utafiti mmoja walikuwa wamekabiliwa na dawa za kuulia wadudu kutokana na kufanya kazi kwenye mashamba, kuishi ndani yake, au vyote viwili.
Wengi walikabiliwa na viuatilifu vya kemikali vinavyovuruga mfumo wa endocrine, dawa ya kuua wadudu inayojulikana kusababisha mabadiliko ya hedhi. Washiriki waliripoti hitilafu katika urefu wa mzunguko wao na kutokuwepo kwa kipindi chao cha Hedhi kwa zaidi ya siku 90.
6. Unyonyeshaji
Ukichagua kunyonyesha mara kwa mara, kipindi chako cha Hedhi hakirudi mara moja. Hii inajulikana kama Lactational amenorrhea, Na hutokea baada ya mtu kujifungua na huongeza muda wa mtu kupata mimba tena. Kwa sababu hiyo, baadhi ya watu huitumia kama njia ya uzazi wa Mpango.
7. Umri
Kipindi chako cha Hedhi kinaweza kisiwe cha kueleweka hadi miaka yako inapofikia 20. Hata hivyo, unapokaribia kukoma hedhi, hedhi inaweza kuwa isiyo ya kawaida tena.
Ingawa labda unatarajia kupata Hedhi kidogo unapokaribia kukoma kwa hedhi, inaweza kutofautiana kulingana na wakati wake. Kwa mfano, hedhi yako inaweza kusimama kwa miezi michache kisha kurudi bila kutarajia.
Hizo ndyo baadhi ya Sababu za Kuchelewa kwa Hedhi…!!!!
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILINE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!