Connect with us

Magonjwa

Mzunguko wa hedhi,mzunguko wa hedhi siku 28

Avatar photo

Published

on

Mzunguko wa hedhi,mzunguko wa hedhi siku 28

Mzunguko wa hedhi(menstrual cycle) huanza unapopata hedhi au kwa lugha nyingine mzunguko wa hedhi huanza pale Mwanamke anapovunja ungo,

Huu ndio wakati unapotoa utando wa uterasi yako. Mzunguko huu ni sehemu ya mfumo wako wa uzazi na hutayarisha mwili wako kwa ajili ya kupata mimba. Mzunguko wa kawaida asilimia kubwa kwa wanawake wengi huchukua siku 28.

Period au Hedhi ni nini?

Period au Hedhi ni ile damu inayotoka kila Mwezi baada ya kuta za Uzazi kubomoka(monthly shedding of the lining of your uterus).

Damu hii huchanganyika na tissu kutoka ndani ya kizazi, vyote kwa pamoja hutoka kama uchafu kupitia kwenye mlango wa kizazi(Cervix) kisha kutolewa nje ya mwili kupitia Ukeni.

Yapo majina mengi ambayo huweza kutumika hapa ikiwemo;

  • Hedhi
  • Period
  • Menstruation
  • menses,
  • menstrual period, n.k

Tukio hili au Mchakato huu mzima kwa Ujumla wake huendeshwa na vichocheo vya Mwili au hormones,

Hormones hufanya kazi kama chemical messengers ndani ya mwili wako. Tezi kwenye Ubongo aina ya pituitary gland na vifuko vya mayai au ovaries (kama sehemu ya mfumo wa Uzazi) hutengeneza na kutoa vichocheo ndani ya muda flani kwenye mzunguko wako wa hedhi, kwa ajili ya kuratibu mzunguko wako mzima(menstrual cycle).

Vichocheo hivi husababisha kuta za kizazi kuwa pana zaidi, na kujiandaa kushika kiumbe endapo ujauzito utatokea,

Mbali na hivo, vichocheo hivi husaidia vifuko vya mayai au Ovaries kutoa yai,mchakato ambao hujulikana kama ovulation. Yai husogea chini ya mirija yako ya uzazi(fallopian tubes), ambapo hungoja manii. Ikiwa manii au mbegu za kiume hazijalirutubisha yai hilo, mimba haitokei. Hivo basi,Utando wa uterasi uliotengenezwa kwa ajili ya mtoto kujishikiza huvunjika na kutoka, Na Hiki ndyo tunaita kipindi cha Hedhi.

Mzunguko wa hedhi

Mzunguko wa hedhi au menstrual cycle huelezea kile kipindi chote ambacho hujumuisha mfululizo wa matukio mbali mbali wakati mwili wako unajiandaa kubeba ujauzito,

Mzunguko wa Hedhi(menstrual cycle) huanza Siku yako ya kwanza kupata Hedhi(menstrual period) mpaka utakapokuja kuona hedhi kwa mara nyingine.

Kumbuka; Mzunguko wa kila mtu ni tofauti kidogo, lakini mchakato wake ni sawa.(Every person’s cycle is slightly different, but the process is the same).

Je, Mzunguko wa kawaida wa Hedhi huchukua Muda gani?

Fahamu, Wastani wa Mzunguko wa Hedhi ambao ni kawaida asilimia kubwa ni Siku 28. Ingawa, Mzunguko wa hedhi Unaoanzia Siku 21 mpaka 35 bado ni wa Kawaida.

Je, period au Hedhi inatakiwa kuchukua siku ngapi kutoka kwa kawaida?

Kwa Asilimia kubwa Wanawake wengi huchukua Siku 3 mpaka 7 za kupata Hedhi,

Ukiona unapata Siku zako za Hedhi kwa Zaidi ya Siku 7, ni tatizo, hakikisha unapata Msaada kutoka kwa Wataalam wa afya.

VIPINDI VINNE KWENYE MZUNGUKO WA HEDHI(Four phases of the menstrual cycle)

fahamu kwenye Mzunguko wako mzima wa hedhi, huchukua Vipindi vinne muhimu ambavyo ni;

(1) The menses phase:

Awamu hii huanza siku ya kwanza ya kupata hedhi. Ni wakati utando wa uterasi unapovunjika na kutolewa nje kupitia ukeni ikiwa ujauzito haujatokea. Watu wengi hutokwa na damu kwa siku tatu hadi tano, lakini muda wa siku tatu hadi siku saba kwa kawaida sio tatizo.

(2) The follicular phase:

Awamu hii huanza siku unapopata hedhi na kuishia kwenye ovulation (huingiliana na awamu ya hedhi/menses phase na kuishia wakati wa ovulation).

Wakati huu, kiwango cha homoni ya estrojeni huongezeka, ambapo husababisha safu ya uterasi (endometrium) kukua na kuwa nene.

Zaidi ya hayo, homoni nyingine inayojulikana kama —  follicle stimulating hormone (FSH) husababisha follicles katika ovari zako kukua. Wakati wa siku 10 hadi 14, moja ya follicles inayoendelea itaunda yai lililokomaa kabisa ambapo ndyo hujulikana kama (ovum).

(3) Ovulation:

Baada ya yai kukomaa tunaingia kwenye hatua hii. Awamu hii hutokea takribani siku ya 14 katika mzunguko wa hedhi wa siku 28,

Kuongezeka kwa ghafla kwa homoni nyingine — homoni ya luteinizing (LH) — husababisha ovari yako kutoa yai lake. Tukio hili hujulikana kama ovulation.

(4) The luteal phase:

Awamu hii hudumu kutoka siku ya 15 hadi siku ya 28. Yai lako hutoka kwenye ovari na kuanza kusafiri kupitia mirija yako ya fallopian hadi kwenye uterasi.

Kiwango cha homoni ya progesterone huongezeka ili kusaidia kuandaa safu yako ya uterasi kwa ajili ya ujauzito. Ikiwa yai litarutubishwa na manii hujishikamanisha na ukuta wako wa uterasi (implantation), na hapo ndipo Ujauzito huendelea kukua siku hadi siku.

Ikiwa mimba haijatokea, viwango vya estrojeni na progesterone hupungua na utando mwingi wa uterasi yako hubomoka wakati wa kipindi chako cha hedhi.

Je, Hedhi inaanza kutoka ukiwa na Umri gani?

Wanawake wengi huanza kupata hedhi wakiwa na umri wa wastani wa miaka 12. Hata hivyo, unaweza kuanza kupata hedhi mapema ukiwa na umri wa miaka 8 au baada ya kufikia umri wa miaka 16. Kwa ujumla, watu wengi hupata hedhi ndani ya miaka michache baada ya kukua kwa matiti na nywele za sehemu za siri.

Watu huacha kupata hedhi wakati wa kukoma hedhi, ambayo hutokea karibu na umri wa miaka 51. Wakati wa kumaliza, Hedhi(Menopause) unaacha kuzalisha mayai.

Dalili za kuanza kupata Hedhi ni Zipi?

Watu wengine hupata dalili za hedhi na wengine hawapati. Ukali wa dalili hizi pia unaweza kutofautiana. Dalili ya kawaida ni tumbo kuuma. Mkazo unaohisi kwenye eneo la pelvic ni dalili za uterasi yako kujigandamiza(contract) na kutoa utando wake.

Dalili zingine zinazoashiria kupata Hedhi ni pamoja na;

  • Kubadilika kwa mood,(Mood changes), Hapa utaona baadhi ya wanawake wanakuwa na vihasira hasira vya karibu, kununa n.k
  • Kupata shida ya Usingizi
  • Kupata Maumivu makali ya Kichwa
  • Kuanza kutamani baadhi ya vyakula na vingine kuvichukia
  • Chuchu kuuma,kuwasha,kuvimba au kuongezeka ukubwa
  • Kupata Chunusi Zaidi kwenye Ngozi n.k

Jinsi Mzunguko wako wa Hedhi unaweza kubadilika baada ya Muda?

Mzunguko wako wa hedhi unaweza kubadilika kutoka miaka ya ujana hadi miaka 40 au 50. Unapopata hedhi kwa mara ya kwanza, ni kawaida kuwa na mizunguko mirefu au mtiririko mzito wa hedhi. Inaweza kuchukua hadi miaka mitatu kwa vijana kuwa na mizunguko ya kawaida baada ya kuanza kupata hedhi. Mzunguko wa kawaida wa hedhi ni mzunguko ambao:

  1. Hutokea takriban kila siku 21 hadi 35.
  2. Husababisha damu kutoka kati ya siku tatu hadi saba.

Mara tu unapofikisha miaka 20, mizunguko yako inakuwa thabiti na ya kawaida. Mara tu mwili wako unapoanza kubadilika hadi kukoma hedhi, hedhi yako itabadilika tena na kuwa isiyo ya kawaida zaidi.

Pia ni kawaida kwa kipindi chako cha Hedhi kubadilika wakati wa matukio mengine ya maisha yanayoathiri homoni zako, kama vile baada ya kuzaa au unaponyonyesha n.k.

Ni kipindi gani Cha Hedhi kinachukuliwa kuwa kisicho cha kawaida?

Hedhi isiyo ya kawaida hufafanua jambo lolote ambalo si la kawaida Mwilini. Baadhi ya mifano ya kipindi cha Hedhi kisicho cha kawaida ni:

  1. Vipindi vinavyotokea chini ya siku 21 au zaidi ya siku 35 tofauti.
  2. Kutokuwa na hedhi kwa miezi mitatu (au siku 90).
  3. Mtiririko wa hedhi ambao ni mzito sana au mwepesi kuliko kawaida.
  4. Kutokwa na damu kwa muda ambao hudumu zaidi ya siku saba.
  5. Vipindi ambavyo vinaambatana na maumivu makali, kichefuchefu au kutapika sana.
  6. Kutokwa na damu au madoa ambayo hufanyika kati ya hedhi.
  7. Kutokwa na hedhi Zaidi ya Mara mbili ndani ya Mwezi mmoja n.k.

Je, ni kiasi gani Cha Damu natakiwa kutoa katika Kipindi cha HEDHI?

Unatakiwa kupoteza damu kati ya vijiko viwili hadi vitatu vya chakula (tbsp.) wakati wa kipindi chako cha Hedhi.

Baadhi ya ishara za kutokwa damu kwa hedhi isiyo ya kawaida ni pamoja na;

• Kutokwa na damu kwenye kisodo au pedi kila saa moja hadi mbili.

Kutoa mabonge ya damu makubwa zaidi.

• Kutokwa na damu kwa muda mrefu zaidi ya siku saba kila unapopata hedhi.

Ni kawaida kupata mabadiliko fulani katika kiwango cha kutokwa na damu kila mzunguko. Ni muhimu pia kukumbuka kuwa kawaida yako inaweza kuwa tofauti na ya mtu mwingine. Jaribu kutolinganisha. Ongea na mtoa huduma ya afya ikiwa una wasiwasi kuhusu kutokwa na damu isiyo ya kawaida au kiwango kikubwa cha damu wakati wa kipindi chako cha Hedhi.

Jinsi ya Kufuatilia Mzunguko wako wa Hedhi?

Ni vyema kufahamu vizuri kuhusu Mzunguko chako wa hedhi. Kutopata hedhi kunaweza kusionekane kuwa jambo kubwa, lakini hedhi isiyo ya kawaida inaweza kuwa ishara ya tatizo. Mtoa huduma wako wa afya atakuuliza kuhusu kipindi chako cha hivi karibuni na mizunguko ya hedhi. Kujua ni nini kawaida kwako kunaweza kusaidia sana kwa mtoaji wako wa huduma.

Kufuatilia vizuri Mzunguko wako wa hedhi pia kunaweza kusaidia katika kujua wakati wa ovulation, wakati ambao una uwezekano mkubwa wa kupata Ujauzito. Inaweza pia kukusaidia kupanga mapema au kujiandaa kutokwa na damu wakati wa hafla maalum au likizo.n.k

Moja ya Njia Za kukusaidia Kufuatilia Mzunguko wako wa Hedhi ni Pamoja na kutumia;

  • Kalenda
  • Na wengine hutumia baadhi ya application kwenye Simu.

Ukiona hali hii kwenye Mzunguko wako wa Hedhi hakikisha unapata Msaada Mapema?

1. Hujapata hedhi hadi kufikia umri wa miaka 16.

2. Hupati Hedhi yako kwa miezi mitatu au zaidi.

3. Unatokwa na damu ghafla kwa siku zaidi kuliko kawaida.

4. Unavuja damu nyepesi au nzito kuliko kawaida.

5. Una maumivu makali wakati wa hedhi.

6. Unatokwa na damu katikati ya hedhi(au unatokwa na damu mara mbili au Zaidi ndani ya mwezi mmoja)

7. Unahisi mgonjwa baada ya kutumia tampons.

8. Unafikiri unaweza kuwa mjamzito – kwa mfano, umefanya ngono na hedhi yako imechelewa kwa angalau siku tano.

9. Kipindi chako cha Hedhi hakijarudi ndani ya miezi mitatu baada ya kuacha dawa za kupanga uzazi na unajua kuwa wewe si mjamzito.

10. Una maswali yoyote au wasiwasi kuhusu kipindi chako cha Hedhi au uwezekano wa ujauzito.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In https://afyaclass.com Also Follow us on Instagram @afyaclass

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa2 months ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa3 months ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa3 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa3 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa5 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake5 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa4 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa1 day ago

Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu

Dalili za infection kwenye damu Mchafuko wa damu,chanzo,dalili na Tiba Mchafuko wa damu; hiki ni kiswahili ambacho watu wamezoea kukitumia...

Magonjwa4 days ago

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri Yapo magonjwa mbali mbali ya ngozi ambayo huweza kuathiri Sehemu za Siri za Mwanaume...

Magonjwa1 week ago

Dalili za acid reflux,Soma hapa Kufahamu

Dalili za acid reflux: Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD), ni tatizo ambalo huwapata Watu wengi,Tatizo hili hujulikana kwa jina...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe au ni ugonjwa ambao huhusisha ngozi kupoteza rangi...

Magonjwa4 weeks ago

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu Baada ya Ugonjwa huu wa macho kusumbua watu wengi kwa kipindi cha Hivi Karibuni,...

Magonjwa4 weeks ago

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu Utangulizi: Scabies huhusisha mtu kuwa na vipele na muwasho kwenye ngozi yake ambapo...

Magonjwa1 month ago

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume Gono ni neno maarufu ambalo kirefu chake ni Gonorrhea na kiswahili chake ni...

Magonjwa1 month ago

Dalili Mpya za ukimwi kwenye ngozi

Zipi ni Dalili za ukimwi kwenye ngozi Zipi ni dalili za Ukimwi kwenye ngozi ya mtu? Fahamu hapa kupitia makala...

Magonjwa1 month ago

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu Huu ni ugonjwa wa kuambukiza uliosababishwa na kirusi cha corona, ambao...

Magonjwa1 month ago

Ishara za Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI) kwa Wanaume na Wanawake

Ishara za Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI) kwa Wanaume na Wanawake Karibu! Hapa kwa makala yenye taarifa muhimu kuhusu...

Trending