Connect with us

News

Dola bilioni 1 kuwezesha uzalishaji wa chanjo Afrika

Avatar photo

Published

on

Viongozi wa dunia pamoja na wawakilishi wa mashirika ya afya na makampuni ya dawa wamejumuika pamoja siku ya Alhamisi mjini Paris, Ufaransa katika mkutano wa kilele unaojadili masuala ya chanjo.

 Katika mkutano huo, kumetangaza ufadhili wa dola bilioni 1.2 zitakazowezesha kuzalisha chanjo huko Afrika, bara ambalo linakabiliwa na matatizo mengi ya kiafya ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.

Mbali na viongozi wa Magharibi, mkutano huo umehudhuriwa pia na viongozi kutoka nchi kadhaa za Kiafrika kama Botswana, Rwanda, Senegal, Ghana, Mataifa mengine yamewakilishwa na mawaziri.

Katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kitendo cha kupiga jeki utengenezaji wa chanjo barani humo, itakuwa hatua muhimu kuelekea kuanzishwa kwa soko la kweli la chanjo Afrika.

Macron ameendelea kusema kuwa robo tatu ya fedha hizo zitafadhiliwa na mataifa ya Ulaya. Ujerumani itachangia dola bilioni 318 kama alivyoeleza Kansela Olaf Scholz katika ujumbe wa video. Ufaransa itatoa dola milioni 100, Uingereza dola milioni 60, huku wafadhili wengine wakiwa ni pamoja na Marekani, Canada, Norway, Japan na Wakfu wa Bill na Melinda Gates.

Kauli za viongozi mbalimbali wakiwemo wa Afrika

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat aliuambia mkutano huo kwamba mpango huo unaweza kuwa kichocheo cha kukuza sekta ya dawa barani Afrika na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi wanachama. Mahamat amesema Afrika huagiza nje ya bara hilo asilimia 99 ya chanjo zake na kwa gharama kubwa.

Kenya- Mama akiwa na mwanae aliyekamlisha dozi ya chanjo ya Malaria
Mama akiwa na mwanae aliyekamlisha dozi ya chanjo ya Malaria huko KenyaPicha: Yasuyoshi Chiba/AFP/Getty Images

Janga la UVIKO-19 liliweka bayana hali ya kutokuwepo usawa katika usambazaji wa chanjo ulimwenguni, kwani nchi tajiri zenye makampuni mengi makubwa ya dawa zilijipatia dozi nyingi za chanjo na kuiacha Afrika ikiwa nyuma. Mpango huo mpya unalenga kuanzisha uzalishaji wa chanjo barani Afrika ili kuliwezesha bara hilo kuwa na uhuru zaidi na kuepusha kujirudia kwa hali iliyoshuhudiwa wakati wa janga la corona.

Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza David Cameron, aliuambia mkutano huo kwamba wakati kutakapotokea janga jingine, na hata kama viongozi katika nchi tajiri za Magharibi watakuwa na nia njema kama malaika, bado kutakuwepo shinikizo la kujihifadhia chanjo kwa ajili ya watu wetu, na kwamba hilo halitazuilika kila wakati.

Kuibuka tena kwa ugonjwa la kipindupindu hivi karibuni katika maeneo mengi ya Afrika, kumeonyesha hitaji la kuwepo wazalishaji zaidi wa chanjo ndani ya Afrika. Kwa sasa, ni kampuni moja tu duniani ya EuBiologics ya Korea Kusini ndio hutengeneza dozi za chanjo kwa bei nafuu ili kukabiliana ugonjwa huo hatari.

Macron amesema mlipuko wa kipindupindu kwa sasa unaathiri karibu nusu ya Afrika huku akitoa wito kwa kuufanya ugonjwa huo kutokomezwa kabisa. Alitangaza pia msururu wa uzalishaji wa chanjo za kipindupindu utakaozinduliwa barani Afrika na kampuni ya biopharmaceutical ya Afrika Kusini ya Biovac.

Kituo cha kwanza cha BioNTech cha kutengeneza chanjo ya mRNA Rwanda
Bango la uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha kwanza cha BioNTech cha kutengeneza chanjo ya mRNA barani Afrika mnamo tarehe 23.06.2022 huko Kigali, Rwanda.Picha: Luke Dray/Getty Images

Muungano wa Gavi unaoyajumuisha mashirika mbalimbali yenye jukumu la kusaidia  kusambaza chanjo za zaidi ya magonjwa 20 kwa nchi maskini , ulikuwa mmoja wa waandaaji wa Jukwaa hilo la Kimataifa kuhusu uhuru na ubunifu wa Chanjo. Katika kongamano hilo, muungano wa Gavi ulitangaza kuwa unalenga kukusanya dola bilioni 9 ili kufadhili programu zake za chanjo kuanzia mwaka 2026 hadi 2030.

Mwenyekiti wa Gavi Jose Manuel Barroso amesema kitendo cha kuwapa chanjo watoto milioni moja tangu mwaka 2000 ni mafanikio ya ajabu, na kwamba mtoto anayezaliwa zama hizi, anaweza kufikisha kwa urahisi miaka mitano kuliko hapo awali katika historia.

Hata hivyo, Barroso ameongeza kusema kuwa bado kuna mamilioni ya watoto ambao hawajapata chanjo dhidi ya ugonjwa wowote huku mamia ya mamilioni ya wengine wakihitaji kupatiwa chanjo zaidi.

Hadi sasa, asilimia mbili tu ya chanjo zinazotolewa barani Afrika ndizo hutengenezwa katika bara hilo. Umoja wa Afrika unalenga kuongeza idadi hiyo hadi kufikia asilimia 60 ifikapo mwaka 2040.

(Chanzo: AFP)

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa2 months ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa3 months ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa3 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa3 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa4 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake5 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa7 hours ago

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri Yapo magonjwa mbali mbali ya ngozi ambayo huweza kuathiri Sehemu za Siri za Mwanaume...

Magonjwa4 days ago

Dalili za acid reflux,Soma hapa Kufahamu

Dalili za acid reflux: Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD), ni tatizo ambalo huwapata Watu wengi,Tatizo hili hujulikana kwa jina...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe au ni ugonjwa ambao huhusisha ngozi kupoteza rangi...

Magonjwa3 weeks ago

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu Baada ya Ugonjwa huu wa macho kusumbua watu wengi kwa kipindi cha Hivi Karibuni,...

Magonjwa3 weeks ago

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu Utangulizi: Scabies huhusisha mtu kuwa na vipele na muwasho kwenye ngozi yake ambapo...

Magonjwa4 weeks ago

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume Gono ni neno maarufu ambalo kirefu chake ni Gonorrhea na kiswahili chake ni...

Magonjwa4 weeks ago

Dalili Mpya za ukimwi kwenye ngozi

Zipi ni Dalili za ukimwi kwenye ngozi Zipi ni dalili za Ukimwi kwenye ngozi ya mtu? Fahamu hapa kupitia makala...

Magonjwa1 month ago

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu Huu ni ugonjwa wa kuambukiza uliosababishwa na kirusi cha corona, ambao...

Magonjwa1 month ago

Ishara za Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI) kwa Wanaume na Wanawake

Ishara za Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI) kwa Wanaume na Wanawake Karibu! Hapa kwa makala yenye taarifa muhimu kuhusu...

Magonjwa1 month ago

Vyanzo Vya Kifo cha Ghafla: Sababu Zinazotisha na Jinsi ya Kujikinga

“Vyanzo Vya Kifo cha Ghafla: Sababu Zinazotisha na Jinsi ya Kujikinga” Kifo cha ghafla ni janga lisilotarajiwa ambalo linaweza kumpata...

Trending