Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume
Gono ni neno maarufu ambalo kirefu chake ni Gonorrhea na kiswahili chake ni Kisonono.
Huu nu ugonjwa wa Zinaa(sexually transmitted infection (STI) ambao husababishwa na bacteria wanaojulikana kama Neisseria gonorrhoeae.
Ugonjwa wa Kisonono au gonorrhea huweza kuwapata Watu wa jinsia Zote,ila katika Makala hii tunazungumzia Zaidi kwa Wanaume.
Maeneo ambayo Kisonono Huweza Kuathiri
Mbali na Ugonjwa wa Kisonono au Gonorrhea kuathiri sehemu za Siri yaani kwenye Uume na Ukeni, yapo maeneo mengine ambayo huweza kuathiriwa na Ugonjwa huu,
Kisonono katika maeneo mengine ya mwili;
Ugonjwa wa Kisonono au Gonorrhea huweza kuathiri Sehemu hizi za mwili;
• Njia ya haja kubwa au eneo la Rectum.
Dalili ni pamoja na kuwashwa kwa njia ya haja kubwa, kutokwa na usaha kutoka kwenye puru, madoa ya damu nyekundu kwenye tishu za choo n.k
• Macho
Kisonono kinachoathiri macho kinaweza kusababisha maumivu ya macho, kutokwa na usaha kwenye jicho moja au yote mawili.n.k
• Kooni
Dalili za maambukizi ya koo zinaweza kujumuisha vidonda kooni, lymph nodi Kuvimba kwenye shingo.n.k
• Kwenye Joints
Ikiwa joint moja au zaidi Zimeambukizwa, dalili mojawapo kwa joints Zilizoathiriwa Zinaweza kuwa joto, kubadilika rangi na kuwa nyekundu, kuvimba na kusababisha maumivu sana, hasa wakati wa kutembe. Hali hii inaitwa septic arthritis.
DALILI ZA UGONJWA WA GONO KWA MWANAUME NI PAMOJA NA;
– Kutokwa na usaha sehemu za Siri au Uchafu wa Rangi nyeupe,njano,au kijani kwenye Uume
– Kuumia wakati wa kukojoa,kitaalam (dysuria).
– Kupata maumivu ya Korodani, Korodani kuvimba n.k
– Kuwashwa kwenye kitundu ambacho mkojo hupita
– Kupatwa na hali ya kuchomwa wakati wa kukojoa ambayo tunasema kwa kitaalam burning sensation
– Mwanaume kupatwa na tatizo la kushindwa kukojoa kabsa au mkojo kugoma kutoka, kitu ambacho huweza kumsababishia maumivu makali pamoja na mahangaiko
– Kukojoa mkojo ambao umechanganyika na Damu
– Joto la mwili kupanda au kuwa na homa n.k
Hizo ndyo Baadhi ya Dalili za Ugonjwa Huu. Ikiwa una Dalili hizi hakikisha Unapata Msaada wa Tiba.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!