Dalili za Gono kwa Mwanamke

Dalili za Gono kwa Mwanamke

Gono ni kifupi tu ambacho kimekua maarufu sana, lakini kifupi hiki kinatokana na neno “Gonorrhea”

Na Tafsiri Yake ni Ugonjwa wa Zinaa ambao unaitwa Kisonono

#Soma Zaidi hapa Dalili za Ugonjwa wa Gono kwa Wanaume

Mara nyingi unasikia Dalili za Ugonjwa wa Gono/Gonorrhea au Kisonono kwa mwanaume, Je wanawake hawapati Gono?

Ugonjwa wa Kisonono au Gono huwapata watu wa jinsia Zote, Ingawa asilimia kubwa Watu huzungumzia dalili kwa upande wa Wanaume,kwa kuliona hilo leo ndani ya afyaclass, Tunachambua dalili za Ugonjwa wa Gono kwa Mwanamke.

Dalili za Gono kwa Mwanamke

Dalili za Gono au kisonono kwa kawaida hutokea ndani ya wiki 2 baada ya kuambukizwa, ingawa wakati mwingine hazionekani hadi miezi mingi baadaye.

Takriban Mwanaume 1 kati ya wanaume 10 walioambukizwa na wanawake 5 kati ya 10 walioambukizwa hawatapata dalili zozote zinazoonekana, kumaanisha kuwa ugonjwa unaweza kwenda bila kutibiwa kwa muda.

Dalili za Ugonjwa wa Gono kwa Mwanamke ni Pamoja na;

1. Mwanamke kutokwa na Uchafu usio wakawaida Ukeni,

Uchafu huu huwa mwepesi au kama maji,na warangi ya kijani au njano

2. Mwanamke Kupata Maumivu au kuhisi kuungua wakati Unakojoa

3. Mwanamke kupata maumivu makali sehemu ya chini ya Tumbo,Ingawa hii sio sana

4. Mwanamke kuvuja damu katikati ya Hedhi, kupata damu nzito sana ya hedhi

5. Au Kuvuja damu baada ya Tendo la Ndoa, Japo dalili hizi sio Sana kutokea.

Ukiona dalili Zozote ambazo huzielewi,hakikisha unaongea na Wataalam wa afya.

#SOMA Zaidi hapa kuhusu dalili za Ugonjwa wa Gono

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!