Hatari ya Upungufu wa damu kwa mama Mjamzito
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, hivi sasa takriban asilimia 30% ya watu duniani wanatatizo la upungufu wa damu(anemia), hasa anemia inayotokana na upungufu wa madini ya chuma yaani Iron deficiency anemia. Wanawake na watoto ndio wagonjwa wenye shida hii zaidi ya anemia.
Upungufu wa damu kwa wanawake wajawazito ni tatizo linalogusa afya ya umma katika nchi nyingi. Utafiti wa Taasisi ya Kitaifa ya Lishe ulionyesha kuwa asilimia 36.8% ya wanawake wajawazito nchini Vietnam wana upungufu wa damu wakati wa ujauzito.
Anemia kwa wanawake wajawazito mara nyingi hujidhihirisha kwa dalili kama vile;
- uchovu na udhaifu wa mwili,
- upotezaji wa nywele,
- kucha kubadilika rangi
- Rangi kubadilika kwenye utando wa mucous mdomoni,
- Lips za midomo kuwa nyeupe zaidi,macho, viganja vya mikono n.k
- Mapigo ya moyo kwenda mbio, Shida ya kupumua, n.k
#SOMA Zaidi kuhusu dalili za Upungufu wa damu mwilini
Wanawake wajawazito huchukuliwa kuwa na tatizo la upungufu wa damu au anemia wakati wa ujauzito ikiwa wana kiwango cha hemoglobin (Hb) chini ya 11g/dl.
Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha upungufu wa damu mwilini lakini kinachojulikana zaidi kwa wajawazito ni upungufu wa madini ya Chuma.
>>Soma hapa kufahamu Damu imetengezwa na nini?
Hatari ya Upungufu wa damu kwa mama Mjamzito
“Athari za upungufu wa damu kutokana na madini chuma Katika kipindi chote cha ujauzito, Hali hii huathiri vibaya ustawi wa mama na kiumbe tumboni, na inahusishwa na kuongezeka kwa magonjwa na kifo cha mtoto aliyetumboni.
Akina mama walioathiriwa mara kwa mara na shida hii ya Upungufu wa damu hupata matatizo ya kupumua, kuzirai, uchovu, mapigo ya moyo kwenda mbio, na matatizo ya usingizi.
Pia wana hatari kubwa ya kupata maambukizi ya kabla ya kuzaa, tatizo la kifafa cha mimba pre-eclampsia, na kutokwa na damu.
Athari Zaidi za Upungufu wa damu kwa Mjamzito ni pamoja na;
Matokeo mabaya ya uzazi yanayojumuisha kuchelewa kwa ukuaji wa mtoto aliyetumboni, Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati, Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo, Na vyote hivi vina hatari kubwa ya kusababisha vifo kwa Watoto, hasa katika ulimwengu unaoendelea.
(1) Madhara yanayoweza kujitokeza kwa Mama mjamzito
- Kuharibika kwa mimba kwa urahisi,
- Kupata tatizo la placenta previa,
- kupata tatizo la placenta abruption
- shinikizo la damu wakati wa ujauzito,
- preeclampsia,
- kupasuka mapema kwa chupa ya Uzazi,
- kutokwa na damu nyingi baada ya kuzaa,
- maambukizi ya baada ya kujifungua.
(2) Madhara yanayoweza kujitokeza kwa Mtoto
– Mtoto kuzaliwa na Uzito mdogo sana
– kuzaliwa kabla ya wakati,
– Watoto wanaozaliwa na mama walio na upungufu wa damu wakati wa ujauzito pia huwa na upungufu wa damu, uzito mdogo, kuzaliwa kabla ya wakati,hatari ya kuongezeka kwa magonjwa ya watoto wachanga kuliko kawaida.
Anemia ya upungufu wa madini ya chuma kwa watoto wachanga inaweza kuwa na athari za muda mrefu katika ukuaji wa ubongo na matokeo yake yanaweza kudhoofisha uwezo wa mtoto kujifunza kutokana na kasoro za malezi ya myelin kutokana na upungufu huo.
Watoto wa akina mama walio na anemia ya ujauzito katika ujauzito wa mapema wana hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu kuliko watoto wengine hadi utu uzima.
Kwa hiyo, madaktari wamezingatia upungufu wa Damu kutokana na madini chuma(Iron deficiency anemia) wakati wa ujauzito kama tishio la uzazi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Rejea Link;
• Mayoclinic
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!