jinsi Ozempic, dawa maarufu ya kupunguza uzito inavyosababisha tatizo la wasiwasi, mfadhaiko na vitendo vya kujiua

Wataalamu wanaeleza jinsi matumizi ya Ozempic yanavyoonekana kubadilisha haiba ya watu na kupunguza tamaa yao ya dawa za kulevya, pombe na hamu ya tendo.

Wanasayansi wamejitokeza kueleza jinsi Ozempic, dawa maarufu ya kupunguza uzito sasa inavyoathiri haiba ya watu kwa kuwafanya wawe na wasiwasi, mfadhaiko na kukabiliwa na vitendo vya kujiua.

Idadi inaongezeka ya wagonjwa wanaodai kuwa dawa ya GLP-1 na zingine kama hiyo zimesababisha wasiwasi, unyogovu,mfadhaiko na mawazo ya kujiua, hata kama wanapunguza uzito.

Ozempic, na matibabu mengine maarufu kama Wegovy, yana athari kwa viwango vya dopamini, ambavyo vinawajibika kwa anuwai ya utendaji.

Pamoja na kuathiri msukumo wetu wa kihisia na kimwili kwa ajili ya chakula, kemikali ya ubongo huathiri hisia za, furaha, motisha na harakati.

Wanasayansi sasa wanaamini kuwa viwango hivi vinavyobadilika katika dopamini vinaweza kueleza kwa nini baadhi ya watumiaji wamedai kuwa dawa hizo pia zimepunguza hamu yao ya dawa za kulevya, pombe na kufanya ngono.

Dk Kent Berridge, profesa wa saikolojia na sayansi ya neva katika Chuo Kikuu cha Michigan, anasema vitu vyote vya kulevya na chakula huwezesha ishara sawa za dopamini na maeneo ya kujifunza katika ubongo.

“Tamaa ya dawa za kulevya pia inaongezeka pamoja na njaa.” Aliambia Daily Mail.

“Watafiti wanapojaribu kuwafanya wanyama wajifunze kutumia kokeini, mara nyingi watawafanya kuwa wawe na njaa kwa muda kidogo, kwani hii huwasaidia kujifunza,” Dk. Berridge alieleza.

“Njaa inamaanisha unahitaji chakula lakini inaweza kuwa zaidi ya hiyo, njaa inaamsha hamu ya vitu vingi. Ikiwa una njaa, Unakuwa na motisha ya vitu vingi, hata vile ambavyo sio chakula,hamu inaonekana kuongezeka.

Kwa sababu dawa hizi huwasaidia wagonjwa kuhisi kushiba kwa muda mrefu, wataalam wanaamini kwamba pia hupunguza tamaa ya vitu vingine mbali na chakula pia, kama vile dawa za kulevya, ngono na pombe.

“Kushiba kunaweza kuwa sio tu kupunguza hamu ya chakula lakini uwezekano wa mambo mengine,” Dk Berridge alisema.

Dawa za GLP-1 zinaonekana kubadilisha mifumo ya motisha ya dopamini, kudhoofisha lakini sio kuondoa matamanio. Kwa mfano, wagonjwa wamegundua kuwa hawapotezi hamu ya kula lakini hula kidogo wakati wanatumia dawa hizi ambazo wataalam wanaamini kuwa zinaweza kuleta madhara mengine.

Pia Utafiti unaonyesha kwamba unaweza kupata matokeo ya kupungua kwa hamu ya tendo wakati wa kutumia dawa za GLP-1 “inawezekana.”

Dk Berridge alieleza kuwa kwa sababu ngono ni tamaa ya asili ya kufurahisha, kukandamiza njia hizi kunaweza kusababisha kupungua kwa hamu ya kufanya ngono.

“Ikiwa unakandamiza [uwezeshaji wa dopamine] Pia matokeo yake ni kupungua kwa hamu ya kufanya ngono” mtaalam wa matibabu alisema.

Mfumo wa kuripoti matukio mabaya yanayohusu Chakula na Dawa wa Marekani ulipokea ripoti 606 za matatizo ya akili yaliyounganishwa na matumizi ya Ozempic, pamoja na ripoti 324 zilizounganishwa na Saxenda na 190 kwa Wegovy mwaka wa 2023.

FDA inahitaji dawa za kudhibiti uzito zinazofanya kazi kwenye mfumo mkuu wa neva, ikiwa ni pamoja na Saxenda na Wegovy, ziwe na onyo kali.

Mwandishi mkuu wa utafiti Dk. Alexis Conason, mwanasaikolojia aliyeidhinishwa katika NYC, alisema;

“Watu huweka hisia nyingi na matumaini katika kupunguza uzito, na wanaamini ikiwa tu watapunguza uzito kila kitu kitakuwa sawa na mambo yote mazuri wanayotaka maishani yatakuja watakapopunguza uzito,” Conason aliiambia The Post hapo awali.

NB; Ni vizuri sana kiafya kupunguza Uzito, lakini Zingatia njia Salama za kupunguza Uzito

#SOMA Hapa Jinsi ya Kupunguza Uzito

•Rejea Link;Uzito journal of tips, FDA

BonusTips; MADHARA ya Kuwa na Uzito Mkubwa kiafya

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!