Ticker

6/recent/ticker-posts

Madhara ya kupiga X ray,Soma hapa kufahamu



Madhara ya kupiga X ray

X-rays ni aina ya mionzi ambayo ina uwezo wa kutengeneza Picha za Tishu pamoja na miundo mbali mbali ndani ya mwili.

Ingawa ni zana muhimu ya kupiga picha na kusaidia kwenye Matibabu kwa kiasi kikubwa sana, X-rays huleta hatari na inaweza kusababisha mabadiliko katika DNA.

Wakati Mionzi ya X-ray inapofyonzwa ndani ya miili yetu, inaweza kuharibu miundo ya molekuli na kusababisha madhara.

Kiwango cha juu sana cha mionzi ya X-rays husababisha uharibifu kwa seli za binadamu, kama inavyothibitishwa na;

  • Tatizo la kuungua au kuchomwa kwa ngozi,
  • kupoteza nywele,
  • na kuongezeka kwa matukio ya saratani.

Kwa sababu viwango vya juu vya mionzi vinaweza kusababisha saratani, kwa hivyo inachukuliwa kuwa hata kiwango cha chini kinaweza pia kusababisha saratani.

Hata hivyo kwa sasa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja wa kisayansi kwamba hii hutokea, na baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa viwango vya chini vya mionzi (kama vile vinavyotumiwa katika kupiga picha) haviongezi hatari ya saratani.(Source; Radiology)

X-rays inaweza kusababisha mabadiliko katika DNA Zetu na, kwa hivyo, inaweza kusababisha saratani baadaye maishani. Kwa sababu hii, X-rays huainishwa kama “carcinogen” na Shirika la Afya Duniani (WHO) na serikali ya Marekani. Walakini, faida za teknolojia ya X-ray ni kubwa kuliko matokeo mabaya ya kuzitumia.

Inakadiriwa kuwa asilimia 0.4% ya saratani nchini Marekani husababishwa na CT scans. Baadhi ya wanasayansi wanatarajia kiwango hiki kuongezeka sambamba na kuongezeka kwa matumizi ya CT scans katika taratibu za matibabu. Angalau uchunguzi wa CT Scans milioni 62 ulifanyika Marekani kwa mwaka wa 2007 pekee.

Ingawa X rays inahusishwa na ongezeko kidogo la hatari ya kupata saratani, kuna hatari ndogo sana ya kupata madhara ya muda mfupi.(Chanzo Kinachoaminika)

Kupatwa na viwango vya juu vya mionzi kunaweza kusababisha athari mbalimbali, kama vile;

  • kutapika,
  • kutokwa na damu,
  • kuzirai,
  • nywele kupotea na
  • kuharibika kwa ngozi na nywele.

Hata hivyo, X-rays hutoa kiwango kidogo sana cha mionzi ambayo haiaminiki kusababisha matatizo yoyote ya afya kwa haraka.

#SOMA PIA; Kipimo cha;

Rejea Link| Source Info;

https://www.medicalnewstoday.com/articles/219970

https://www.cancer.org/cancer/cancer-causes/radiation-exposure/x-rays-gamma-rays/other-health-problems.html



Post a Comment

0 Comments