Ticker

6/recent/ticker-posts

Uume unaoaminika kuwa ni wa Mtoto wakutwa ndani ya chakula



Uume unaoaminika kuwa ni wa Mtoto wakutwa ndani ya chakula.

Polisi Nchini Uganda wanawashikilia Watu wawili (Mmiliki wa Mgahawa na Muhudumu) baada ya uume unaoaminika kuwa ni wa Mtoto kukutwa ndani ya chakula walichomuuzia Mteja katika mgahawa mmoja Jijini Kampala.

Imeelezwa kuwa Mteja huyo alifika kwenye mgahawa akiwa na njaa na kuagiza chakula kitamu akipendacho ambacho kina mchanganyo wa nyama ndani yake lakini kwa mshtuko mkubwa wakati anaendelea kutafuna akahisi anatafuna kitu kinachofanana na uume na alipokagua vizuri akagundua ni uume wa Mtoto.

Taarifa ya Polisi imenukuliwa ikieleza kwa ufupi kuhusu tukio hilo ——— > “Ingawa unaonekana kabisa ni uume wa Binadamu uliopikwa lakini hatuwezi kufanya hitimisho kwa kutazama kwa macho, kwahiyo umepelekwa kwa Mkemia kwa ajili ya kuthibitisha”

Via:MillardAyoUPDATES



Post a Comment

0 Comments