Watu wenye ugonjwa wa moyo wanapaswa kupunguza ulaji wa sodiamu

Watu wenye ugonjwa wa moyo wanapaswa kupunguza ulaji wa sodiamu.

Taasisi ya Moyo ya nchini Marekani “The American Heart Association (AHA)” inapendekeza watu wazima ambao hawana au hawajulikani kuwa wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo wasitumie zaidi ya 2,300 mg ya sodiamu kwa siku. Hii ni sawa na kijiko kimoja cha chumvi.

Mtu wa kawaida aliye na ugonjwa wa moyo katika utafiti huu alizidi matumizi ya kiwango hicho kwa karibu miligramu 1,000.

Utafiti ulitumia data kutoka kwa washiriki 3,170 katika utafiti wa NHANEST  wa Kituo cha Kudhibiti Magonjwa. Sampuli hizi zilijumuisha wanaume na wanawake walio na umri wa zaidi ya miaka 20 na utambuzi wa ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu yaani cardiovascular disease diagnosis.

Kati ya kundi hili, wengi walikuwa na umri wa miaka 65 au zaidi, walikuwa wazungu, na walikuwa na kiwango cha elimu cha chini ya wahitimu wa shule ya upili. Walikuwa Wanaume, ambao walichukua zaidi ya nusu ya masomo (56.4%), walikuwa na shida ya Uzito Mkubwa(overweight) na wastani wa ulaji wa kalori 1,862 kwa siku.

Ingawa ulaji mwingi wa sodiamu mara nyingi Watu wengi huchukulia  kama matokeo ya kutokula mlo wa kutosha au Mlo kamili swala ambalo hutokea Zaidi kwa watu wenye kipato cha Chini, utafiti huu hubadilisha nadharia hiyo,

Kundi lililokuwa na ulaji mkubwa wa sodiamu walikuwa watu wenye kipato cha Juu na wenye shahada ya chuo kikuu au zaidi.

Waandishi wa utafiti wanapendekeza kwamba watu walio na viwango vya juu vya elimu na mapato wangeweza kuwa bora katika kuripoti na kudhibiti ulaji wao wa sodiamu kila Siku kuliko wengine, ila haikuwa hivo,hii imechangia matokeo kuwa ya kushangaza Zaidi.

Nini kinatokea kwenye moyo ikiwa unatumia sodiamu nyingi?

Jina la kemikali kwenye chumvi ya mezani ni Sodium chloride(Nacl). Sodiamu ni madini ya asili, ambayo ni muhimu kwa afya ya binadamu kwa kiasi kidogo.

“Sodiamu husaidia kusawazisha maji katika mwili wako,” alielezea daktari wa magonjwa ya moyo Jayne Morgan, MD, mkurugenzi wa kimatibabu katika Shirika la Afya la Piedmont huko Atlanta, GA. “Inasaidia hata utendakazi mzuri wa misuli na mishipa.” (Dk. Morgan hakuhusika katika utafiti huo.)

“Kuna msemo Unasema, ‘Mahali sodiamu huenda, maji hufuata,'” aliiambia Medical News Today.

“Hii ndiyo sababu chumvi huongeza kiasi cha damu katika miili yenu. Madhara ya hili ni kuongezeka kwa shinikizo la damu(presha). Kuongezeka kwa shinikizo la damu basi hulazimisha moyo wako kufanya kazi kwa bidii zaidi, ambayo hatimaye inakuweka katika hatari ya kupata ugonjwa wa moyo,” Dk. Morgan alisema.

Dk. Morgan alibainisha kuwa sodiamu iliyozidi kwa muda mrefu imekuwa ikihusishwa na Tatizo la ugumu wa mishipa ya damu au kwa kitaalam atherossteosis.

SOURCES:Rejea Link;

– Taasisi ya Moyo ya nchini Marekani “The American Heart Association (AHA)”

Medical News Today Cited articles from“The American Heart Association (AHA)”

– Utafiti wa NHANEST

– Daktari wa magonjwa ya moyo Jayne Morgan, MD, mkurugenzi wa kimatibabu katika Shirika la Afya la Piedmont huko Atlanta, GA.

– Creator,Editor,Reviewer; Dr.Ombeni Mkumbwa, @afyaclass

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!