Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa hydrocele,chanzo,dalili na Tiba yake



Ugonjwa wa hydrocele,chanzo,dalili na Tiba yake

Hydrocele ni tatizo ambalo huhusisha kuvimba kwa eneo la korodani au uvimbe ndani ya vifuko vya korodani(Scrotum) unaosababishwa na kujaa maji.

Tatizo hili ndyo kwa jina Lingine hujulikana kama “BUSHA”.

Tatizo la hydrocele ni aina ya uvimbe kwenye korodani, au mfuko wa ngozi unaoshikilia korodani. Uvimbe huu hutokea wakati majimaji yanapojikusanya kwenye kifuko chembamba kinachozunguka korodani. Hydroceles ni kawaida pia kwa watoto wachanga”

Dalili za Ugonjwa wa hydrocele

Mara nyingi ishara pekee ya hydrocele ni uvimbe usio na uchungu au maumivu kwenye korodani moja au zote mbili.

Uvimbe huo unaweza kufanya korodani ya mtu mzima kuhisi nzito. Kwa ujumla, maumivu yanaongezeka wakati uvimbe unaongezeka. Wakati mwingine, eneo lenye kuvimba linaweza kuwa dogo asubuhi na kubwa baadaye mchana.

Vitu hivi huongeza hatari ya Kupata tatizo la hydrocele

Hydroceles nyingi zipo wakati wa kuzaliwa. Tafiti zinaonyesha Angalau asilimia 5% ya wanaume waliozaliwa wana hydrocele,

Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, ambao huzaliwa zaidi ya wiki tatu kabla ya tarehe zao za kuzaliwa, wana hatari kubwa ya kuwa na hydrocele pia.

Sababu za hatari za kupata hydrocele baadaye maishani ni pamoja na:

  • Kupata Jeraha au kuvimba ndani ya korodani.
  • Maambukizi, ikiwa ni pamoja na magonjwa ya zinaa.n.k

Madhara ya Hydrocele ni yapi?

Mara nyingi si tatizo lenye hatari kubwa au madhara zaidi ni la kawaida, Na pia haliathiri uwezo wa kupata mtoto kama baadhi ya watu wanavyosema.

Ingawa pia hydrocele inaweza kuhusishwa na shida za kiafya ambazo zinaweza kusababisha madhara makubwa. Kuna uhusiano wa hydrocele na Matatizo haya:

Maambukizi au tumor.

Na matokeo yake inaweza kusababisha korodani kutengeneza kiwango kidogo cha manii au zisifanye kazi vizuri kama kawaida.

Hernia ya inguinal.

Hii inaweza kusababisha matatizo ya kiafya ambayo huweza kutishia maisha.

Chanzo cha tatizo la hydrocele

Tatizo la hydrocele au Busha ni tatizo la kujaa kwa maji kwenye mfuko wa korodani za mwanaume.

SABABU AU CHANZO CHA TATIZO LA HYDROCELE NI NINI?

Tatizo la Busha au hydrocele huweza kusababishwa na vitu mbali mbali ikiwemo;

– hali ya eneo la Kuzunguka Korodani kuwa na Maji mengi kuliko ilivyokawaida,

– Mirija ya Lymph kwenye Korodani au mishipa ya Damu inayosafirisha damu kutoka kwenye korodani kwenda maeneo mengine ikiwa Imeziba kabsa,

Vyote hivi hupelekea kupungua kwa ufyonzwaji wa maji yanayozunguka eneo la korodani. Hali ambayo hupelekea maji kujikusanya kwenye vifuko vya Korodani.

HIZI NI BAADHI YA SABABU ZA MAJI KUWA MENGI KWENYE ENEO LA KORODANI

• Mtu kupata Majeraha au kuumia kwenye Korodani(Injury)

• Mtu kupata Maambukizi ya magonjwa kwenye eneo la Korodani

• Mtu kupata Maambukizi kwenye mshipa wa-epididymis

• Mtu kupata Maambukizi yanayo sababishwa na vimelea wa filaria (filariasis) wanao sababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.

• Mtu kupata tatizo la Korodani Kujisokota ambapo kwa kitaalam hujulikana kama testicular torsion

• Mtu kupata Uvimbe kwenye korodani yaani testicular tumors,

Hii pia huweza kuchangia uzalishwaji wa maji mengi kwenye korodani.

• Mtu Kufanyiwa upasuaji ambao huweza kuathiri ufyozwaji wa maji kwenye korodani

• Mtu kupata Tiba ya mionzi kipindi cha nyuma. n.k

KUMBUKA; Watu ambao wapo maeneo ya Pwani, wapo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la Busha,

Hui ni kutokana na kuwa kwenye hatari zaidi ya kung’atwa na mbu aina ya Culex anayeeneza vimelea vya filaria.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



Post a Comment

0 Comments