Ukambi ni ugonjwa gani?
Ukambi kwa jina lingine rahisi ni surua),ambapo ni ugonjwa wa kuambukiza unaoenezwa sana kupitia mgusano, Ugonjwa huu husababishwa na virusi vya jamii ya paramyxovirus.
Dalili za Ukambi ni Zipi
Ishara na dalili za kwanza kwa kawaida hujumuisha homa, ambayo mara nyingi huwa zaidi ya °C 40 (°F 104.0), kikohozi, mafua, na macho mekundu. Siku mbili au tatu baada ya dalili kuanza, madoa madogo meupe yanaweza kuonekana ndani ya kinywa yanayojulikana kama alama za koplik.
Chunusi nyekundu, zinazoanza kwenye uso kisha kuenea kwa mwili wote, kwa kawaida huanza siku tatu hadi tano baada ya mwanzo wa dalili,
Dalili kwa kawaida huwa siku 10–12 baada ya kutangamana na mtu aliyeambukizwa kwa siku 7–10.
Matatizo zaidi yanayotokana na ukambi hutokea kwa takriban asilimia 30% na yanaweza kujumuisha kuhara, upofu, kuvimba kwa ubongo, na nimonia miongoni mwa mengine.
Rubela na roseola ni magonjwa tofauti ingawa yanafanana na surua.
#Soma Zaidi hapa kuhusu Ugonjwa wa Surua
#Soma Zaidi kuhusu Rubela
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!