WHO Ripoti mpya: kuna uhusiano wa COVID-19 na unene au utipwatipwa kwa Watoto

WHO Ripoti mpya: kuna uhusiano wa COVID-19 na unene au utipwatipwa kwa Watoto

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la afya la duniani WHO imesema kuna uhusiano baina ya COVID-19 na Watoto kukabiliwa na changamoto ya utipwatipwa au obesity barani Ulaya.

Ripoti hiyo ya WHO inasema imethibitisha ilichokuwa inakishuku kwa muda mrefu ambacho ni uhusiano baina ya janga hilo la COVID-19 na ongezeko la viwango vua utipwatipwa miongoni mwa Watoto wa kati ya umri wa miaka 7 hadi 9.”

Ripoti hiyo iliyopewa jina “Athari za COVID-19 kwa Maisha ya kila siku na tabia za Watoto wa umri wa Kwenda shule: Matokeo katika nchi 17 wanachama wa kanda ya Ulaya ya WHO”  inawasilisha utafiti unaoonyesha kwamba;

 “Janga la COVID-19 lilisababisha Watoto wengi kutumia muda mwingi kutazama vifaa vya kielecktroniki kama televisheni, Ipad , simu na vifaa vingine na kuwa na shughuli chache za mazoezi ya kimwili, na hivyo kuakisi ongezeko la watoto walio na uzito uliopitiliza katika umri ulioanishwa”

Utipwatipwa kwa watoto Ulaya

Ofisi ya Kanda ya WHO ya Ulaya ilianzisha mpango wa ufuatiliaji wa utipwatipwa kwa Watoto mwaka wa 2007 ili kukabiliana na hitaji la takwimu sanifu na sahihi za uchunguzi kuhusu kuenea kwa tatizo la uzito kupita kiasi na unene uliopitiliza miongoni mwa watoto wenye umri wa kwenda shule.

WHO imesisitiza kuwa “Upatikanaji wa taarifa kama hizo ni muhimu ili kuendeleza sera na mikakati madhubuti ya kukabiliana na unene wa kupindukia wa watoto katika Kanda ya Ulaya ya WHO.”

Awamu hii ya sita ya ukusanyaji wa twakimu za COSI inahusisha nchi wanachama 37 na ukusanyaji wa takwimu bado unaendelea katika baadhi ya nchi hizi.

Ripoti hii inawasilisha matokeo kutoka kwa majimbo 13 yaliyokusanya taarifa katika mwaka wa shule wa 2021-2022 kuhusu athari za janga la COVID-19 kwa afya ya watoto, na nne zilizokusanya taarifa katika mwaka wa shule wa 2022-2023.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo “Matokeo ya utafiti huu juu ya matokeo ya janga hili ni muhimu sana kwa Nchi Wanachama zinazoshiriki ili kusaidia kujiandaa kwa siku zijazo.”

Via; https://news.un.org/sw/story/2024/05/1174811

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!