Ticker

6/recent/ticker-posts

FAIDA NA MADHARA YA MATUMIZI YA FENI KWA WATOTO WADOGO



 

FAIDA NA MADHARA YA MATUMIZI YA FENI KWA WATOTO WADOGO

• • • • • •

Jambo hili lina pande zote mbili, Faida na Madhara kama ifuatavyo;

?FAIDA ZA FENI KWA WATOTO WADOGO

1. Feni husaidia mzunguko safi wa hewa ndani ya chumba, Jambo ambalo litamsaidia mtoto kutopata joto kupitiliza (overheating)

2. Feni husaidia mtoto kuendelea kupumua kama itatokea atajigeuza hivyo kujibana pumzi wakati wa kulala. Takwimu zinaonesha feni zinapunguza vifo vya ghafla vya watoto (SIDS) kwa asilimia 72%

3. Pia, feni hutoa muungurumo/sauti ambayo tafiti zinaeleza husaidia katika ubembelezaji na kufanya watoto wadogo kulala muda mrefu zaidi

?MADHARA YA FENI KWA WATOTO WADOGO

1. Feni huweza kusababisha kikohozi kwa watoto wadogo

2. Pia, feni huweza kusababisha hali ya ubaridi mkubwa katika ngozi ya mtoto

SASA TUTUMIE AMA TUACHE?

Feni ZIENDELEE KUTUMIKA ila kutokana na uwepo wa mtoto ama watoto, Speed ya feni ipunguzwe, isiwekwe ile ya juu kabisa ili kuzuia kikohozi lakini pia kwa upande mwingine imsaidie kupumua na kumpunguzia joto kali. Na pia, HAIFAI kumuelekezea feni usoni mtoto mdogo kwa wale wenye feni zinazosimamishwa chini sakafuni. Kama una feni za aina hiyo jaribu kutoielekeza moja kwa moja kwa mtoto. Hivyo, muhimu ni WEKA SPEED NDOGO na USIIELEKEZEE FENI MOJA KWA MOJA KWA MTOTO.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!






Post a Comment

0 Comments