Kuwashwa Mwili Ni Dalili Ya Nini,Soma hapa kufahamu

Kuwashwa Mwili Ni Dalili Ya Nini,Soma hapa kufahamu

Tatizo la kuwashwa mwilini ni tatizo ambalo huweza kutokea kwa Mtu yeyote kwa Sababu mbali mbali, Na leo katika Makala hii tumechambua Sababu hizo;

Kuwashwa mwili ni hali ambayo huhusisha muwasho ambao unatokea kwenye ngozi yako,na baadhi ya watu muwasho huu huweza kuambatana na vipele kwenye ngozi au rashes,

Kulingana na chanzo cha muwasho huu,ngozi yako pia huweza kubadilika hata katika muonekano,

Unaweza kuhisi hali ya Ngozi kuwaka moto, kuwa na vipele, kuwa na matuta,kuvimba n.k. Pia kwa baadhi ya watu hupata hali ya Vidonda kwenye ngozi hii, ngozi kutoka damu, lakini pia kutengeneza mazingira rahisi ya kuambukizwa zaidi na vimelea vya magonjwa mbali mbali.

Dalili za Kuwashwa Mwili

Hali hii ya kuwashwa mwili huweza kuanza kwenye maeneo mbali mbali kama vile; Kichwani, mikononi au miguuni, kisha kuathiri mwili mzima,

Na huweza kuambatana na dalili mbali mbali kama vile;

  1. Kuhisi ngozi kuwaka Moto
  2. Ngozi kupasuka au kuwa na magamba au michirizi
  3. Ngozi kuwa na Upele au rashes
  4. Hali ya ngozi kukauka sana
  5. Ngozi kuwa na vidonda n.k

Chanzo cha Kuwashwa Mwili

Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kusababisha hali hii ya kuwashwa mwilini na Sababu hizo ni pamoja na;

– Tatizo la ngozi kukauka kupita kawaida(dry skin)

– Magonjwa yanayohisisha ngozi kama vile;

  1. Ugonjwa wa pumu ya ngozi(eczema)
  2. Fangasi wa kwenye damu au ngozi
  3. Tatizo la Scabies
  4. Pamoja na matatizo mengine ya ngozi kama vile Psoriasis n.k

– Tatizo la Allergies au mzio juu ya vitu mbali mbali ikiwemo, baadhi ya mafuta ya kupaka au kupikia,vyakula n.k

– Mashambulizi ya vimelea wengine wa magonjwa kama vile parasites n.k

– Sumu inayotokana na kung’atwa na wadudu mbali mbali

– Na wakati mwingine hali ya kuwashwa ngozi ya mwili huweza kutokana na magonjwa ya ndani(Internal diseases) kama vile;

  1. Ugonjwa wa Ini(Liver disease)
  2. Ugonjwa wa Figo(kidney disease)
  3. Tatizo la Upungufu wa damu mwilini au Anemia
  4. Ugonjwa wa kisukari
  5. Matatizo kwenye tezi la thyroid
  6. Baadhi ya Saratani
  7. Pamoja na matatizo ya mfumo wa Neva(Nerve disorders) ikiwemo; tatizo la multiple sclerosis n.k

– Mashambukizi ya Virusi,ikiwemo virusi wanaoweza kuleta hali ya mkanda wa jeshi kwenye ngozi yaani shingles au herpes zoster.n.k

– Matatizo yanayohusu afya ya akili(Psychiatric conditions). mfano; tatizo la wasi wasi au anxiety, tatizo la obsessive-compulsive disorder pamoja na depression.

– Matumizi ya baadhi ya Dawa, wakati mwingine hali ya kuwashwa mwili huweza kutokana na reactions ya baadhi ya dawa ulizotumia ili kutibu matatizo mbali mbali.

Vitu ambavyo huongeza hatari ya kupata tatizo la Kuwashwa mwili

– Kuwa na matatizo mbali mbali yanayohusu ngozi kama vile pumu ya ngozi,tatizo la Scabies, maambukizi fangasi n.k

– Kuwa na magonjwa mengine kama vile; ugonjwa wa Ini,Figo,magonjwa kwenye tezi la thyroid n.k

– Kuwa na tatizo la ngozi kukauka sana,dry skin n.k

Matibabu ya Kuwashwa Mwili

Watu wengi hupata ahueni kwa hatua za kujitunza kama vile; kwa kutumia vimiminika vya unyevu ikiwemo mafuta ya kupaka, visafishaji laini na kuoga kwa maji ya Uvuguvugu.

Lakini Tiba kamili na Msaada wa muda mrefu unahitaji kutambua na kutibu sababu ya ngozi kuwasha. Matibabu haya huhusisha matumizi ya dawa za kupaka,kunywa n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!