Ticker

6/recent/ticker-posts

Sindano ya Anti-d Pamoja Doses Zake



Sindano ya Anti-d Pamoja Doses Zake

Sindano ya Anti-D ni sindano ambayo hutoa Anti-D immunoglobulin kwenye damu ya mama Mjamzito na mama baada ya kujifungua,

Kazi kubwa ya anti-D immunoglobulin ni kusaidia kuneutralises Antigens zozote zinazotokana na Rhesus factor(RhD) positive,

Antigens hizi huingia kwenye mzunguko wa damu wa mama wakati wa Ujauzito,

Endapo antigens hizi zimefanikiwa kuzimwa au kufanyiwa neutralization,haziwezi tena kusababisha damu ya Mama kutengeneza antibodies kwa ajili ya mapambano,

KUMBUKA: matatizo yote huanza pale ambapo Damu ya mama imeshatengeneza antibodies kwa ajili ya mapambano kwa kila kitu kigen(antigen) kinachoingia,

Na madhara zaidi huonekana kwa mtoto hasa kwenye Ujauzito wa Pili.

JE NINI KINASABABISHA DAMU YA MAMA KUTENGENEZA ANTIBODIES,

je kitu gani kinasababisha Damu ya mama kutengeneza antibodies mpaka kufikia hatua ya kuhitaji kuchoma sindano ya Anti-D Ili madhara yasitokee kwa mimba na Mtoto kwa ujumla?

IPO HIVI;

Endapo Mama Mjamzito ana ana Kundi(group) Lolote la damu rhesus factor NEGATIVE, mfano; A-, AB-,B- au O-

Wakati baba wa Mimba hyo ana kundi au group lolote La Damu rhesus factor POSITIVE,mfano; A+,AB+,B+ au O+

Hapo asilimia Kubwa Mtoto aliyetumboni mwa mama atakuwa na Rhesus factor POSITIVE,

Hali hii kwenye mzunguko wa damu wa Mama mjamzito huchukuliwa kama kitu cha kigen(Antigens) kwani hakipo kwa damu ya mama,

Hivo basi Damu ya mama itatengeneza antibodies(Kama Ulinzi) na kupambana na antigens zinazoingia,

Na hapa ndyo madhara hutokea kwa Ujauzito na mtoto baada ya kuzaliwa,

Mtoto huweza kupata matatizo mbali mbali baada ya kuzaliwa,kama vile kuishiwa na damu,kukosa hewa ya oxygen na kupoteza maisha muda mfupi baada ya kuzaliwa.

Utapewa Sindano ya Anti-D immunoglobulini iwapo itadhaniwa kuwa kuna hatari yoyote ya antijeni za RhD kutoka kwa mtoto wako Kuingia kwenye damu yako,

Lakini vile vile utoaji wa dose ya Anti-D immunoglobulin kwa kawaida hutolewa kuanzia kwenye kipindi cha third trimester kwenye Ujauzito wako,

Na hapa tunazungumzia Ujauzito ukiwa na umri wa kuanzia Miezi 7 au wiki 28,

Hii ni kwa Sababu,katika kipindi hiki,kuna uwezekano wa kiwango kidogo cha damu kutoka kwa mtoto kupita kwenda kwenye damu ya Mama.

DOSE ZA SINDANO YA ANTI-D(Rho) KWA MAMA MWENYE BLOOD GROUP AMBAZO ZINA MATATIZO NILIYOELEZEA HAPO JUU

Haya hapa ni maelekezo kuhusu doses za Sindano ya Anti-D

  1.  Dose ya kwanza ya sindano za Anti-D, huchomwa kwa mama mjamzito ambaye ujauzito wake una umri wa kuanzia MIEZI SABA(7) au Wiki 28-30 za ujauzito,Hivo basi, mama mjamzito atachomwa sindano yenye 1500 IU~300mcg IV/IM,ujauzito ukiwa na miezi saba au kuanzia wiki 28-30 za ujauzito
  2. Dose ya pili ya Sindano ya Anti-D huchomwa ndani ya Masaa 72 baada ya mama kujifungua,

Hivo basi, mama Baada ya kujifungua atachomwa sindano yenye 1500 IU~300mcg IV/IM,ndani ya MASAA 72 baada ya kujifungua,

Lakini wataalam wa afya hushauri kwamba,endapo mama hakufanikiwa kuchoma sindano ya ANTI-D ndani ya masaa 72 baada ya kujifungua anatakiwa ahakikishe kachoma hyo sindano Ndani ya siku 28,ila asiache kabsa kuchoma.

KUMBUKA; mama kuchoma dose zote mbili yaani wakati wa ujauzito na ndani ya masaa 72 baada ya kujifungua hutoa matokeo mazuri zaidi kuliko kwa mama ambaye kachoma dose moja tu ya Anti-D.

SOMA ZAIDI HAPA; Kuhusu Dose ya Sindano ya Anti-D







Post a Comment

0 Comments