Ticker

6/recent/ticker-posts

Tofauti kati ya dalili za mimba na hedhi



Tofauti kati ya dalili za mimba na hedhi

Kati ya Swali gumu miongoni mwa Wanawake wengi ni kuweza kutofautisha kati ya dalili za mimba na Dalili za hedhi,

Na Ukweli nikwamba,Dalili nyingi za mimba zinafanana na dalili za Hedhi, Kwa kuliona hilo,Leo ndani ya afyaclass tumechambua baadhi ya tofauti hizo;

Mara nyingi,Ishara na dalili za  mwanzo kwenye ujauzito pamoja na mwanzo wa kipindi chako cha Hedhi ni pamoja na;

  • Kubadilika kwa mudi,
  • Kupata maumivu ya mgongo
  • Kukojoa mara kwa mara
  • Maumivu ya matiti au chuchu
  • Chuchu au matiti kuwasha n.k

Kwa kuwa dalili nyingi zinafanana,Njia pekee ya kujua kama wewe ni mjamzito au sio mjamzito ni kufanya Vipimo(pregnancy test).

#SOMA zaidi hapa kuhusu dalili;

  1. Za Mimba
  2. Mzunguko wa Hedhi

Dalili zinazofanana kati ya Mimba na Hedhi

Kwa wanawake wengi, ishara na dalili za mwanzo za ujauzito zinaweza kufanana na za hedhi yake inayokaribia kutoka. Kwa kweli,ni ngumu kutofautisha kwenye dalili za mwanzo peke yake ikiwa mwanamke ni mjamzito au ana dalili zinazohusiana na kipindi chake cha hedhi.

Ishara na dalili zinazofanana zaidi ni pamoja na:

1. Kupata Maumivu ya kichwa:

Maumivu ya kichwa yanaweza kuwa dalili ya ujauzito, lakini wanawake wengi pia hupata maumivu ya kichwa au kipandauso kabla ya kipindi cha hedhi.

2.Maumivu ya mgongo:

Dalili hii inaweza kutokea ikiwa kipindi chako cha Hedhi kinakaribia, lakini pia inaweza kuwa dalili kwamba una Ujauzito.

3. kubadilika kwa Mudi,Mood changes:

Hapa ndyo hali mbali mbali hutokea kama vile; Mtu kuwa na wasi wasi,hofu, kuwa na vihasira vya hapa na pale, kulia n.k

Dalili hizi huweza kutokea kote,ikiwa ni mjamzito au upo kwenye kipindi cha Hedhi.

4. Kupata choo kigumu,kukosa choo(Constipation):

Homoni ya progesterone inaweza kusababisha usumbufu wa usagaji chakula ikiwa ni pamoja na kuvimbiwa,kupata choo kigumu au kukosa kabsa choo.

Kwa sababu viwango vya projesteroni hupanda katika nusu ya pili ya mzunguko wa hedhi, Hali ya Kukosa choo au kupata choo kigumu inaweza kuwapo kwa wanawake waliokaribia kipindi cha hedhi. Vivyo hivyo, mabadiliko ya homoni katika ujauzito yanaweza pia kusababisha tatizo hili la constipation.

5. Kuongezeka kwa hali ya kukojoa sana:

Unaweza kukojoa mara kwa mara ikiwa una Ujauzito, lakini hali hii huweza kutokea pia ikiwa unakaribia kupata hedhi.

6. Maumivu ya matiti:

Maumivu ya matiti, kuwasha,kuvimba, au kuongezeka kwa ukubwa kunaweza kutokea katika ujauzito na pia kabla ya kipindi chako cha Hedhi kuanza.

Tofauti kati ya dalili za mimba na hedhi

Hizi hapa ni baadhi ya tofauti kati ya dalili za mimba na dalili za Hedhi;

✓ Aina ya Damu inayotoka(Bleeding or spotting):

Mara nyingi mwanamke hupata vitone vya damu(Mild spotting) wakati mtoto anajishikiza kwenye ukuta wa mji wa mimba kitendo ambacho hujulikana kama implantation, Hii ni tofauti na damu ya kawaida ya hedhi ambayo hutoka nyingi hasa wakati unaanza hedhi yako ukilinganisha na vitone hivi.

✓ Uchovu wa Mwili:

Ni kweli kwamba uchovu huweza kutokea ukiwa mjamzito lakini pia hata ukiwa kwenye kipindi chako cha Hedhi,

Tofauti ni kwamba; Uchovu wa kipindi cha Hedhi huisha mara tu hedhi inapoanza kutoka, lakini uchovu wa ujauzito ni wa muda mrefu zaidi(haushi).

✓ Kuchagua vyakula,kukosa hamu ya kula:

Unaweza kupata hali hii hata ukiwa kwenye hedhi, Lakini hali hii huzidi zaidi ikiwa wewe ni mjamzito

✓ Kupata kichefuchefu na kutapika

Hii ni Ishara kubwa kwa Mwanamke mwenye Ujauzito, ni mara chache sana kwa Mwanamke anayekaribia hedhi kupata kichefuchefu na kutapika.

Bonus Points:

Dalili za Kipekee kwa Ujauzito;

(i) Kukosa Hedhi

Kutokuwepo kwa hedhi ni dalili kuu ya ujauzito.

(ii) Kutokwa na vitone vya damu(Light spotting)

Kutokwa na vitone vya damu huweza kutokea wakati mtoto anajishikiza kwenye ukuta wa mji wa mimba,

Kama tulivyoeleza hapo awali, kunaweza kuwa na kutokwa na damu kidogo wakati wa kupandikizwa kwa kiinitete kwenye uterasi wakati ujauzito ukiwa kwenye hatua za mapema. Hii ni tofauti sana na mtiririko wa kawaida wa damu ya hedhi.

(iii) Kutokwa na majimaji ukeni:

Kuongezeka kwa uzalishwaji wa estrojeni wakati wa ujauzito kunaweza kusababisha ongezeko la kutokwa kwa uchafu mweupe kama maziwa ukeni.

Tofautisha na Uchafu wa maambukizi ya magonjwa kama vile Fangasi; SOMA Zaidi hapa aina za Uchafu Ukeni na maana zake

(iv) Weusi kwenye eneo la kuzunguka chuchu(areola):

Weusi huongezeka Zaidi kwenye eneo la kuzunguka chuchu ambalo kitaalam hujulikana kama areola, hali hii huweza kutokea mapema wiki moja au mbili baada ya mimba kutungwa. Inaweza pia kuendeleza baadaye katika ujauzito wako. Hii sio ishara kabsa ya kukaribia kwa hedhi.

Ni matumaini yangu umepata kujua tofauti ya dalili za hedhi na dalili za mimba angalau kwa Ufupi, Asante kwa kusoma Makala hii…!!!!



Post a Comment

0 Comments