Ugonjwa wa Malaria,chanzo,dalili,Madhara na Tiba yake

Ugonjwa wa Malaria,chanzo,dalili,Madhara na Tiba yake

Malaria ni Ugonjwa ambao huwasumbua watu wengi na Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ambayo huongeza idadi ya Vifo hasa kwa nchi Zinazoendelea.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO); Ulimwenguni kote mwaka 2022, kulikuwa na wastani wa visa vya malaria milioni 249 na vifo 608,000 vya malaria katika nchi 85.”

Malaria ni Ugonjwa Gani?

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vinavyojulikana kama Plasmodium.Vimelea hivi huenezwa na mbu jike aina ya anofelesi (anopheles). Lakini watu wengi huelewa kwamba malaria husababishwa na mbu. Mbu huyu husaidia katika usambazaji tu wa vimelea husika.

Aina ya vimelea ambavyo humdhuru binadamu kati ya vimelea vingi vya Plasmodium ni:

Plasmodium Vivax

• Plasmodium Falciparum

• Plasmodium Malariae

• Plasmodium Oval

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO); Ulimwenguni kote mwaka 2022, kulikuwa na wastani wa visa vya malaria milioni 249 na vifo 608,000 vya malaria katika nchi 85.”

Dalili za Ugonjwa wa Malaria

Fahamu kwamba,miongoni mwa dalili za mwanzoni kabsa kwa Ugonjwa wa malaria ni Mtu kuwa na Homa,maumivu ya kichwa na kuhisi baridi au mwili kutetemeka(fever, headache and chills).

Dalili za Ugonjwa wa Malaria kwa Mtu mara nyingi huanza ndani ya siku 10–15 za kuumwa na Mbu aliye na vimelea wa Malaria yaani infected mosquito.

Dalili zake zinaweza zisiwe kali kwa baadhi ya watu, hasa kwa wale ambao awali walikuwa na maambukizi ya malaria. Kwa sababu dalili zingine za malaria sio maalum au zinaweza zisieleweke kwa haraka, kupimwa mapema ni muhimu.

Baadhi ya maambukizi ya Ugonjwa wa malaria yanaweza kusababisha Ugonjwa mbaya na hata Vifo. Watoto wachanga, watoto chini ya miaka 5, wajawazito, wasafiri na watu wenye VVU au UKIMWI wako katika hatari kubwa zaidi.

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za Ugonjwa wa Malaria;

1. Mwili kukosa nguvu na kuchoka kupita kiasi

2. Baadhi ya Watu kuwa na dalili za kuchanganyikiwa,kama Dalili kali Zaidi za Ugonjwa wa Malaria(severe symptoms).

Dalili Zingine Kali Zaidi ni pamoja na;

  • Kupata Shida ya Kupumua
  • Kukojoa Mkojo mweusi
  • Kuwa na manjano,ngozi na macho kubadilika rangi na kuwa manjano, kwa kitaalam jaundice n.k

3. Kupata Homa

4. Mwili kutetemeka na kuhisi baridi kali

5. Kupata Maumivu makali ya Kichwa Mara kwa Mara

6. Kupata maumivu ya misuli,joints pamoja na viungo mbali mbali vya mwili

7. Kuhisi kichefuchefu na kutapika

8. Kuharisha

9. Kupata Maumivu ya Tumbo

10. Na baadhi ya Watu huanza kukohoa n.k

Watu wenye dalili kali za Malaria wanatakiwa kupata Msaada wa haraka Zaidi ili kuepusha kupata madhara Zaidi, Na matibabu ya mapema kwa Ugonjwa huu huzuia maambukizi kuwa mabaya Zaidi.

Maambukizi ya malaria wakati wa ujauzito pia yanaweza kusababisha kujifungua mtoto kabla ya wakati au kuzaliwa kwa mtoto mwenye uzito mdogo. Pia hata Vifo huweza kutokea katika kipindi hiki.

Madhara ya Ugonjwa wa Malaria(Complications)

Ugonjwa wa Malaria huweza kusababisha Vifo,  na Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani(WHO); inakadiriwa kuwa takribani asilimia 94% ya Vifo vyote vinavyotokana na Ugonjwa wa Malaria hutokea Africa — Hasa kwa Watoto wenye umri wa chini ya Miaka 5.

Na Vifo hivo vya Ugonjwa wa Malaria huweza Kutokana na  Madhara haya;

~ Malaria kuleta athari kwenye Ubongo(Cerebral malaria).   Ikiwa seli za damu zilizojaa vimelea huziba mishipa midogo ya damu kwenye ubongo wako (cerebral malaria), uvimbe wa ubongo wako au uharibifu wa ubongo unaweza kutokea. Malaria hii  inayoshambulia ubongo inaweza kusababisha kifafa na kukosa fahamu.

~ Matatizo ya Upumuaji(Breathing problems). Hii ni kutokana na Maji kuweza kujikusanya kwenye mapafu (pulmonary edema) kisha kukusababisha upate shida sana ya kupumua,

Haya pia huweza kuwa Madhara ya Ugonjwa wa Malaria.

~ Viungo vya Mwili kushindwa kufanya kazi(Organ failure). Malaria inaweza kuharibu figo au ini au kusababisha wengu kupasuka. Yoyote kati ya hali hizi inaweza kuhatarisha maisha.

~ Kusababisha Upungufu wa Damu(Anemia). Ugonjwa wa Malaria unaweza kusababisha usiwe na kiwango cha kutosha cha Seli nyekundu za damu yaani red blood cells, Hali ambayo huweza kuathiri pia usambazaji wa kutosha wa hewa ya Oxygen kwenye tishu mbali mbali za mwili.

~ Tatizo la Upungufu wa Sukari kwenye Damu(Low blood sugar). Aina kali za malaria zinaweza kusababisha sukari kuwa chini kwenye damu (hypoglycemia), Sukari kuwa chini sana kwenye damu inaweza kusababisha kukosa fahamu au kifo.

~ Pia Ugonjwa wa Malaria huweza kusababisha Madhara mengine makubwa ikiwemo;

  • Mtu kuchanganyikiwa
  • Madhara kwa mama mjamzito; Maambukizi ya malaria wakati wa ujauzito pia yanaweza kusababisha kujifungua mtoto kabla ya wakati au kuzaliwa kwa mtoto mwenye uzito mdogo. Pia hata Vifo huweza kutokea katika kipindi hiki.

Jinsi ya kuzuia maambukizi ya Malaria

1. Hakikisha unazuia mazalia ya mbu

Fyeka vichaka na ondoa madimbwi ya maji katika  maeneo yanayokuzunguka.

2. Zuia kung’atwa na mbu, Zipo njia mbali mbali ambazo huweza kutumika ili kuzuia kung’atwa na Mbu ikiwemo;

i. Matumizi ya vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu

ii. Matumizi ya dawa za kupulizia za kuua mbu majumbani

iii. Matumizi ya dawa za kupaka za kuua mmbu

3. Dawa za kuzuia malaria kwa kina mama wajawazito (IPT)

Sulfadoxine Pyrimethamine (SP) hutolewa kwa kina mama katika wiki ya 20 na wiki ya 36 ya ujauzito.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!