Ticker

6/recent/ticker-posts

Umuhimu wa lishe bora katika ukuaji na afya ya akili



LISHE IWE NI AJENDA YA KUDUMU

Na, WAF – Songea, Ruvuma

Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel amesisitiza umuhimu wa lishe bora katika ukuaji na afya ya akili kwa kuzingatia mlo wa chakula chenye virutubisho na kuwa ajenda ya kudumu katika uhamasishaji wa mlo bora

Dkt. Godwin Mollel, ameyasema hayo leo Agosti 24, 2024 akimuwakilisha Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama (Mb), katika misa takatifu ya kumbariki Abate Emmanuel Mlwilo OSB wa Abasia ya Peramiho, iliyofanyika katika mkoa wa Ruvuma.

Akizungumza wakati wa misa hiyo, Dkt. Mollel amesisitiza umuhimu wa lishe bora, hasa katika mikoa inayozalisha chakula kwa wingi kama Ruvuma, Rukwa, Songwe, Mbeya, na Njombe ya kuwa licha ya uwepo wa chakula kingi katika mikoa hiyo, kuna changamoto ya lishe bora, ambapo watu wanashiba lakini hawapati virutubisho muhimu kutoka katika vyakula wanavyokula.

“Lishe bora ina athari kubwa kwa afya ya akili na ukuaji wa mtoto, ni muhimu kuhakikisha kuwa agenda ya lishe inachukuliwa kwa uzito katika kutoa elimu kwa jamii, ili kuhakikisha kuwa chakula kinachozalishwa kinatumika ipasavyo kuboresha afya na ustawi wa wananchi”. Amesema Dkt Mollel

Hata hivyo, Dkt. Mollel amesema Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka teknolojia kwa asilimia 97 ili kuboresha huduma za afya nchini hivyo teknolojia hiyo itatumika vyema na kutunzwa ikiwa tutaendelea kuzalisha kizazi chenye afya bora kutokana na lishe.



Post a Comment

0 Comments