Vibarango-Mapunye Kichwani: Chanzo, Dalili, na Tiba
Vibarango kichwani ni maambukizi ya ngozi yanayosababishwa na fangasi wa aina ya Trichophyton na Microsporum. Fangasi hawa wanaweza kuathiri maeneo ya ngozi kama vile vinyweleo na kope za macho, na kwa jina la kitaalamu huitwa tinea capitis.
Ugonjwa huu hutokea mara nyingi kwa watoto kutokana na ukosefu wa vimelea wa kinga kama Pityrosporum orbiculare, ambao huweza kupambana na fangasi hawa. Watu wazima wana vimelea hawa, hivyo maambukizi haya ni nadra kwao.
Fangasi hawa huathiri ngozi isiyo na afya na wanaweza kuenea hadi kwenye ngozi ya kope na sehemu nyingine za mwili. Mara wanapokuwa kwenye ngozi, hukua kwa kusambaa kutoka katikati na kuunda miduara.
Baadaye, fangasi huathiri mashina ya vinyweleo chini ya ngozi, na dalili huonekana ndani ya siku 12 hadi 14 baada ya maambukizi, kama vile mduara wa vibarango kichwani. Vinyweleo vilivyoathirika huweza kukatika, na hali hii inakuwa dhahiri baada ya wiki tatu.
Ugonjwa huu hupatikana kwa wanaume zaidi kuliko wanawake, na huonekana sana kwa watoto wenye umri wa miaka 3 hadi 7.
FANGASI KICHWANI
DALILI ZA FANGASI WA KICHWANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE
Fangasi wa kichwani hupenda kuwashambulia watoto wadogo zaidi ya watu wazima, Japo hata watu wazima wanaweza kupatwa na tatizo hili la Fangasi wa kichwani. Hapa ndipo majina mbali mbali yakatokea kama vile Mapunye, vibarango N.K lakini yote yanamaanisha dalili za mashambulizi ya ugonjwa wa Fangasi wa kichwani.
Lakini kuna fangasi pia wa maeneo mengine mbali mbali ya mwili kama vile;
- – Fangasi wa Kwenye kucha
- – Fangasi wa kwenye damu
- – Fangasi wa miguuni
- – Fangasi wa kwenye Ngozi
- – Fangasi wa kwenye ulimi
- – Fangasi wa kooni
- – Fangasi wa tumboni
- – Fangasi wa ukeni
- – Fangasi wa uumeni na korodani
- – Fangasi wa mdomoni
- N.K
• Soma: Ugonjwa wa Lawalawa,chanzo,dalili na Tiba yake
DALILI ZA FANGASI WA KICHWANI NI PAMOJA NA;
1. Ngozi ya kichwani kuanza kukakamaa na kubadilika rangi kwa mafungu
2. Kuwa na vitu kama mashalingi ya rangi nyeupe kichwani
3. Kutoa kama mba eneo la kichwani
4. Na wakati mwingine eneo la mashilingi kutoa vitu kama usaha
5. Kuwa na vidonda na michubuko kwenye ngozi ya kichwani
6. Kuwashwa sana kwenye Ngozi ya kichwani
MATIBABU YA FANGASI WA KICHWANI
– Fangasi wa kichwani hutibiwa kwa kutumia aina mbali mbali za dawa za fangasi ambapo zipo dawa za kupaka na endapo tatizo litakuwa sugu na la kujirudia rudia mgonjwa atapewa dawa za fangasi wa kichwani za kunywa.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!