Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa Kimeta,chanzo,dalili na Tiba(Anthrax)



 Ugonjwa wa Kimeta,chanzo,dalili na Tiba(Anthrax)

Ugonjwa wa Kimeta(Anthrax)

Ugonjwa wa Kimeta au Anthrax ni ugonjwa unaosababiswa na bacteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis.

Ugonjwa huu wa kimeta unaweza kuathiri binadamu na wanyama,wanyama hao wanaweza kuwa wa porini au mifugo kama vile;

  • ng'ombe,
  • nguruwe,
  • ngamia,
  • kondoo,
  • mbuzi, nk.

Pia fahamu kwamba, Bakteria hawa wanaosababisha ugonjwa wa kimeta ambayo hupatikana kama spores, wanaweza kupatikana kwenye udongo, pamba, au nywele za wanyama walioambukizwa.

Ugonjwa wa Kimeta au Anthrax huweza kumuathiri binadamu kwa njia kubwa tatu(3);

  1. Kwa njia ya maambukizi ya ngozi(Skin infection), kwa kugusana moja kwa moja na wanyama walioambukizwa kupitia majeraha,vidonda au sehemu ya ngozi ulipokatwa
  2. Kupitia kula nyama mbichi au ambayo haijaiva vizuri kutoka kwa wanyama walioambukizwa au kupitia kunywa maziwa yao.
  3. Kuvuta pumzi yaani Inhalation, ambapo unavuta hewa ndani pamoja na Spores za bacteria wanaosababisha ugonjwa wa kimeta (Hii ni aina mbaya zaidi ya ugonjwa huu)

Maambukizi haya ya Ugonjwa wa kimeta kwa njia ya ngozi(Skin infection) kawaida ni maambukizi ya ngozi, ambapo watu huambukizwa kwa kushika wanyama au bidhaa za wanyama ambazo zina spores,

Hii mara nyingi hutokea kwa madaktari wa mifugo, wafanyakazi wa kilimo, wazalishaji wa mifugo au wachinjaji wanaoshughulika na wanyama wagonjwa, au wakati maambukizi yameenezwa na pamba au ngozi.

Dalili za Ugonjwa wa Kimeta

1. Kwa wanyama, Ugonjwa wa kimeta huweza kusababisha dalili kama vile;

  • homa kali,
  • udhaifu au kudhoofika kwa mnyama,
  • kukosa hamu ya kula,
  • kutokwa na damu kwenye matundu yote ya mwili (pua, mdomo, masikio, njia ya haja kubwa n.k.),
  • kupata shida ya kupumua
  • Pamoja na kuharisha damu.
  • Pia Ugonjwa wa kimeta unaweza kusababisha kifo cha ghafla.
  • Damu ya mnyama aliyeambukizwa kimeta HAIGANDI wakati wa kuchinja. Pia, wakati wa kuchinja, kuna uvimbe wenye alama na kuoza kwa haraka.

2. Kwa wanadamu, kulingana na aina (ilivyoelezwa hapo juu) na njia ya maambukizi, Ugonjwa wa kimeta(anthrax) kwa binadamu unaweza kusababisha dalili kama vile;

  • Kupata homa,
  • vidonda vya ngozi visivyo na maumivu
  • Kuwa na alama nyeusi inayoonekana baada ya malengelenge,
  • Mwili kukosa nguvu au kuwa na udhaifu wa jumla wa mwili,
  • Kupata shida ya kupumua.
  • Pia ugonjwa wa kimeta unaweza kusababisha ugonjwa mkali kwenye mfumo wa umeng'enyaji chakula(digestive illness) unaofanana na sumu kwenye chakula(food poisoning).

Nani yupo kwenye hatari ya Kupata Ugonjwa wa kimeta?

Watu hawa wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Ugonjwa wa kimeta;

1. Watu wanaoshughulikia wanyama, yaani,

  • madaktari wa mifugo,
  • wafanyakazi wa maabara ya mifugo,
  • wakulima,
  • wafanyakazi wa machinjio,
  • wachinjaji,
  • wafugaji wa ng'ombe,
  • wazalishaji na wafanyabiashara wa mifugo,
  • watunza wanyamapori,
  • wawindaji,
  • walinzi wa mbuga,
  • wasindikaji,
  • waagizaji na wasafirishaji wa ngozi,
  • wahudumu wa afya ya wanyama. na kadhalika.

2. Watu wanaokula wanyama (ng'ombe, kondoo, na mbuzi) waliopatikana wamekufa

3. Wafanyakazi wa afya,

4. wafanyakazi wa maabara ya uchunguzi

5. watoa huduma ambao wanahudumia vidonda vya mgonjwa aliyeambukizwa

6. Maafisa wa kutekeleza sheria (Polisi, Jeshi, Uhamiaji, Forodha, pamoja na Wafanyikazi wengine.)

7. Yeyote anayesafiri hadi eneo ambapo kuna kisa kilichothibitishwa cha ugonjwa wa kimeta.



Post a Comment

0 Comments