Tatizo la hormone imbalance,chanzo,Dalili na Tiba
Tatizo la hormone Imbalance huweza kusababisha dalili nyingi sana kwenye mwili wa Mtu, Bahati nzuri ni kwamba Hali nyingi zinazosababisha Tatizo la hormone Imbalance zinaweza kutibiwa.
Tatizo la hormone Imbalance ni tatizo ambalo huhusisha uwiano usio sawa wa Vichocheo mwilini.
KUMBUKA;Hormones ndiyo Vichocheo;Hivo basi, katika Makala hii utasikia Zaidi haya maneno, kila tunapotumia neno hormones ujue tunamaanisha vichocheo vya mwili na kila tutakapotumia neno vichocheo ujue tunamaanisha hormones.
Hormones ni nini na zinatoka wapi?
Kwa jina lingine Hormones hujulikana kama chemical Messager kemikali hizi zenye nguvu husafiri kuzunguka damu yako, zikitoa taarifa kwa tishu na viungo nini cha kufanya.
Hormones husaidia kudhibiti michakato mingi Mikuu ya mwili wako, ikiwa ni pamoja na Shughuli Zote za kimetaboliki pamoja na Uzazi yaani metabolism and reproduction.
Unachotakiwa kufahamu ni kwamba Hormones au Vichocheo vya mwili huzalishwa na tezi zinazojulikana kama endocrine glands, hivo mfumo mzima unaodhibiti vichocheo hivi hujulikana kama Endocrine System.
Tezi zinazounda endocrine system ni pamoja na:
- Hypothalamus.
- Pituitary gland.
- Pineal gland.
- Thyroid.
- Parathyroid glands.
- Adrenal glands.
- Pancreas.
- Ovaries.
- Testes.n.k
Katika Tezi zote hizi,Vipo vichocheo vya aina mbali mbali ambavyo kila Tezi huzalisha mwilini,
Tatizo la hormone Imbalance hutokea pale ambapo una kiwango kikubwa au kidogo sana cha homoni fulani. Hata mabadiliko madogo tu yanaweza kuwa na athari mbaya katika mwili wako wote.
Viwango vingine vya homoni hubadilika katika maisha yako yote na huenda ikawa tu matokeo ya Uzee ambapo ni kawaida kwa binadamu yeyote. Lakini mabadiliko mengine hutokea wakati tezi zako za endocrine zinapopata kichocheo kibaya.
Dalili Za Tatizo la hormone Imbalance
Homoni zako zina jukumu muhimu katika afya yako kwa ujumla. Kama matokeo, kuna ishara na dalili ambazo zinaweza kuashiria kuwa hakuna usawa wa homoni mwilini mwako au una tatizo la Hormone Imbalance. Ishara au dalili zako zitategemea ni homoni zipi hazipo sawa au ni tezi zipi hazifanyi kazi ipasavyo.
Kwa kiasi kikubwa Hali za homoni zinazoathiri watu wa jinsia zote zinaweza kusababisha mojawapo ya ishara au dalili zifuatazo:
- Uzito kuongezeka kwa kasi au wakati mwingine Uzito kupungua kwa ghafla
- Mwili kuchoka kupita kiasi
- Misuli ya mwili kuwa dhaifu
- Misuli kuuma,kukakamaa n.k
- Kupata Maumivu ya Joints,kukakamaa au kuvimba
- Kuongezeka au kupungua kwa Mapigo ya Moyo(Heart rate)
- Kuvuja jasho kupita kiasi
- Kuhisi baridi sana au kuhisi joto sana wakati hali ya mazingira ni tofauti
- Kukojoa mara kwa mara
- Kuongezeka kwa kiu ya Maji
- Kuhisi njaa kila wakati
- Kuhisi hali ya Hofu,huzuni,woga,Wasiwasi,Kuwa na Msongo wa mawazo n.k
- Kuona marue rue
- Hamu ya tendo la ndoa kupungua au kuisha kabsa
- Kuongezeka sana kwa nywele mwilini au kupungua sana kwa nywele mwilini
- Ngozi kukauka sana(dry skin)
- Uso kuwa na mafuta Zaidi,Chunusi n.k
KUMBUKA; Dalili hizi huingiliana kwa kiasi kikubwa na matatizo mengine ya kiafya tunasema ni nonspecific symptoms, hivo kuwa na moja ya dalili hizi haimaanishi una tatizo la hormone Imbalance pekee, Inaweza kuwa ni tatizo lingine la kiafya.
Baadhi ya dalili hizi zinaweza pia kuonyesha hali Zingine Sugu(chronic conditions). Kwa hivyo, ikiwa unapata dalili hizi, kushughulika na mabadiliko yoyote muhimu katika mwili wako au viwango vya hormones ni wazo nzuri kuzungumza na Wataalam wa afya kwanza.
Dalili za Tatizo la Hormone Imbalance kwa Wanawake
Kwa Watu wenye ovari, matokeo ya kawaida ya tatizo la hormone imbalance ni kuwa na hali ambayo hujulikana kama polycystic ovary syndrome (PCOS).
Hata hivo,Mwanamke pia hupokea mabadiliko ya Vichocheo mwilini kwenye Vipindi kama vile;
- Kipindi cha balehe
- Kipindi cha Ujauzito
- Kipindi cha Unyonyeshaji
- Pamoja na Kipindi cha Ukomo wa hedhi(menopause)
Baadhi ya Dalili za Tatizo la hormone Imbalance kwa Wanawake ni pamoja na:
1. Kuvurugika kwa Mzunguko wa hedhi,hali ambayo hupelekea Mwanamke;
- Kukosa kabsa siku zake
- Kukaa muda mrefu bila kuona hedhi au hedhi kuchelewa Zaidi
- Hedhi kutoka kidogo sana
- Hedhi kutoka mara kwa mara
- Kuvuja damu nyingi wakati wa hedhi
- Kutokuwa na Tarehe maalum ya kuona siku za hedhi n.k
2. Nywele kuota kupita kiasi kwenye maeneo mbali mbali ya Mwili ikiwemo; Usoni, kwenye kidevu au Sehemu zingine za mwili
3. Mwanamke kuwa na Chunusi Usoni,Kifuani au Sehemu ya Juu ya Mgongo
4. Nywele za mwili kupotea au unapata tatizo la hair loss
5. Uke kuwa Mkavu sana,Tatizo la vaginal dryness
6. Kupata maumivu wakati wa tendo
7. Mwanamke kuvuja sana jasho usiku
8. Kupata Maumivu ya kichwa mara kwa mara
9. Chuchu kutoa Maziwa zenyewe wakati sio mjamzito wala hunyonyeshi
10. Kushindwa kubeba Ujauzito n.k
Dalili za Tatizo la Hormone Imbalance kwa Wanaume
Hapa tutazungumzia zaidi kichocheo cha kiume ambacho hujulikana kama Testosterone. Ikiwa Mwanaume huzalishi testosterone ya kutosha, hali hii inaweza kusababisha dalili mbalimbali ikiwemo;
1. Mwanaume kuota Matiti kama Mwanamke,Tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama gynecomastia,
Kwa kiasi kikubwa,Tatizo hili la Mwanaume kuota matiti huhusisha kuongezeka kwa tishu ndani ya tezi za matiti ya Mwanaume, Pamoja na Uwiano usio sawa wa vichocheo vya estrogen pamoja na testosterone,hii ndyo sababu kubwa ya tatizo hili.
2. Mwanaume kupata Maumivu kwenye Matiti
3. Kuwa na Upungufu wa nguvu za kiume au Uume kushindwa kusimama vizuri ambapo kwa kitaalam hujulikana kama erectile dysfunction
4. Mwanaume kupungua kwa ukuaji wa ndevu na ukuaji wa nywele za mwili
5. Misuli kupungua na kukosa nguvu,loss of muscle mass
6. Mifupa kuwa dhaifu,kuvunjika kwa haraka
7. Mwanaume kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k
Zipo dalili nyingi, hizi ni baadhi tu ya dalili hizo...!!!
Chanzo cha Tatizo la Hormone Imbalance
Zipo Sababu nyingi ambazo huchangia tatizo hili na baadhi ya Sababu hizo ni pamoja na;
1. Matumizi ya vitu vyovyote ambavyo huweza kuongeza au kupunguza baadhi ya vichocheo vya mwili ikiwemo;
- Dawa mbali mbali
- Baadhi ya Njia za Uzazi wa Mpango
- Matibabu ya Saratani kama vile chemotherapy
2. Kuwa na Uvimbe au tumors hasa kwenye maeneo ya tezi kama vile pituitary tumors n.k
3. Kuumia ambako hugusa na kuathiri mfumo wa vichocheo mwilini(endocrine system)
4. Matatizo yanayotokana na Ulaji yaani eating disorders
5. Msongo wa mawazo au stress
6. Lakini pia zipo baadhi ya hali Zingine ambazo huongeza hatari ya kupata tatizo hili kama vile;
- Kuwa na kisukari aina zote mbili(type 1 and type 2 diabetes)
- Kuwa na tatizo la Tezi la Thyroid kutokufanya kazi vizuri hali ambayo hujulikana kama hypothyroidism, or underactive thyroid
- Tezi hili kufanya kazi kupita kiasi,hyperthyroidism, or overactive thyroid n.k
7. Pia hali ya kuwa na kiwango kikubwa cha cortisol n.k
Kumbuka; Nilitaja hali zingine ambazo huhusishwa na mabadiliko haya ya Vichocheo mwilini hasa kwa Mwanamke, hali hizo ni pamoja na;
>Mwanamke kufikia Ukomo wa hedhi(menopause)
>Ujauzito
>Unyonyeshaji
>Tatizo la PCOS
>Matumizi ya baadhi ya dawa, hormone medications kama vile vidonge vya Uzazi wa mpango- birth control pills n.k
Je,Unasumbuliwa na Tatizo hili na hujapata Tiba bado?
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.