Tatizo La Tonses,chanzo Na Tiba

Tatizo La Tonses,chanzo Na Tiba

#1

Tatizo La Tonses,chanzo Na Tiba

Tatizo la tonses au wengine huliita tatizo la Tonsil ni tatizo ambalo huhusisha kuvimba kwa tonses kwa kitaalam Tonsillitis Tatizo hili mara nyingi huathiri watoto ingawa hata watu wazima huweza kupata pia.

Tatizo hili huambatana na Dalili mbali mbali, Sasa katika makala hii tuangalie Dalili Zake,Chanzo pamoja na Tiba Yake.

Dalili za Tatizo la Tonses

Dalili kubwa za Tatizo la Tonses ni pamoja na:

  • Eneo la Tonses kubadilika rangi na kuwa jekundu
  • Kuvimba eneo la tonses
  • Kupata shida ya kumeza kitu
  • Au kupata maumivu wakati wa kumeza kitu
  • Homa
  • Kuhisi hali ya Vidonda kooni,Sore throat
  • Tezi za shingoni maarufu kama Lymph nodes kuongezeka ukubwa,kuuma n.k
  • Sauti kukwaruza
  • Kutoa harufu mbaya Mdomoni au puani
  • Kupata maumivu ya Shingo
  • Shingo kukakamaa
  • Kupata maumivu ya Kichwa n.k

Chanzo cha Tatizo la Tonses

Tatizo la Kuvimba kwa Tonses husababishwa na maambukizi ya Vimelea vya magonjwa kama vile bacteria au Virusi. 

Na jamii ya bacteria inayohusika Zaidi ni pamoja na Streptococcus pyogenes au group A streptococcus, Pia jamii zingine za Streptococcus pamoja na bacteria wengine huweza kusababisha tatizo la tonses kuvimba.

Vitu ambavyo huongeza hatari ya Kupata Tatizo la Tonses

-Umri; Tatizo la kuvimba kwa Tonses mara nyingi huathiri watoto, Kuvimba kwa tonses kunakosababishwa na maambukizi ya bakteria ni kawaida sana kwa watoto wa miaka 5 hadi 15.

- Kuwa kwenye Mazingira ya kupata Vimelea vya Magonjwa kwa Urahisi mara kwa mara(Frequent exposure to germs). Mfano;Watoto wanaokwenda shule wanakuwa na mawasiliano ya karibu na wenzao, Hii inawafanya mara kwa mara wakabiliwe na maambukizi ya virusi au bakteria ambayo yanaweza kusababisha tatizo la kuvimba kwa tonses.

Je, ni Kwanini Tonses hushambuliwa?

Tonses ni safu ya kwanza ya mfumo wa kinga ya Mwili dhidi ya bakteria na virusi Wanaoingia kinywani mwako.  Kazi hii inaweza kufanya tonses kuwa katika hatari Zaidi ya kuambukizwa na kuvimba.  

Hata hivyo, kazi ya mfumo wa kinga kwa tonses hupungua baada ya kubalehe - jambo ambalo linaweza kuchangia matukio ya kuvimba kwa tonses kupunguza Zaidi kwa watu wazima.

Matibabu ya Tatizo la Tonses

Kwa matibabu ya tatizo la kuvimba kwa Tonses, Tiba kamili hutegemea na chanzo husika, Mfano kama chanzo ni maambukizi ya bacteria Mgonjwa atapewa Dawa jamii ya antibiotics, Lakini kama Chanzo ni maambukizi ya Virusi kuna uwezekano mkubwa wa shida hii kuisha yenyewe ndani ya Siku 7 mpaka 10, pamoja na njia Zingine huweza kutumika ikiwemo; kupata muda wa kutosha wa kupumzika na kulala, kunywa maji ya Kutosha, kutibu dalili zingine kama Maumivu,Homa n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

WEKA COMMENT HAPA..!!!


image quote pre code